Wakuu wa mikoa kuwa sehemu ya nidhamu ya mahakama

UNDULE ROBERT

Member
Jan 24, 2011
27
2
Katika bunge lililopita ilipendekezwa wakuu wa mikoa kuwa sehemu ya nidhamu ya mahakama. Tundu lissu alipinga kwa nguvu zote lakini hakusikilzwa. Wana jf mbona kimya? Pia hatujasikia maoni ya tls. Je tunaelekea wapi na huu mhimili muhimu?
 
The MPs who do not have tha love of this country have facitated the passing of the bill. It is very shameful to use the party (CCM) leaders to buldose the court of Law. I am fed up with this kind of paliamentarians. Let us educate people how useless they are.:nerd:
 
Umbumbu na ubabe wa speaker na wabunge vihiyo wa chama chake ndiyo ulipelekea ile hoja kupitishwa, pamoja na kwamba hata MP hakuwaunga mkono.
 
Mmh!huku sasa ni kuua kabisa uhuru wa mahakama,kwa mantik hii i wapi dhana ya kila muhimili kuwa huru na kutoingiliwa na mwingine!Ama kweli hatuna bunge.
 
Tuna wabunge wa ajabu sana, mimi binafsi nianza kupata hofu kama hata wanatua akili kidogo kufikiri kabla ya kuunga mkono hoja. Naomba CV ya mwanasheria mkuu wa serikali, amenifadhaisha sana.:spy:
 
Mmh!huku sasa ni kuua kabisa uhuru wa mahakama,kwa mantik hii i wapi dhana ya kila muhimili kuwa huru na kutoingiliwa na mwingine!Ama kweli hatuna bunge.
Nashauri chama cha wanasheria TLS kitoe tamko juu ya suala hili.
 
Kabla ya hapo wakuu wa Mikoa na Wilaya wlikuwa wenyeviti wa Bodi za Mahakama za Mikoa na Wilaya, respectively. Mbona hatukuona mwingiliano wowote? Au Sheria hii mpya imewapa RCs mamlaka zaidi?
 
Katika kupitisha bill hii waziri mkuu aliungana na wapiganaji kupinga wakuu wa mikoa kuhusiswa na masuala ya mahakama, nadhani kwa kutumia taaluma yake pm aliona busara ya kutowahusisha wanasiasa kwenye mambo ya mahakama. Kilichonishangaza sana ni pale watu ambao wenzetu humu wanawaita wapambanaji kama Samuel Sitta ambae ni mwanasheria kuungana na hao wabunge mbumbumbu wa sheria kuunga mkono upitishwaji wa ile bill!! Mara zote mimi ninawatahadhalisha wanajanvi kuwa huyu Sitta sio mpambanaji wa ukweli bali ni mchumia tumboni. Nawasilisha.
 
Naaaaaaaaaaaaaam time will tell,hakika drama hizi zitakosa watizamaji na watizamaji watakua wachezaji.Hakuna sehemu haki zinachezewa kama kwenye MAHAKAMA zetu,ambako hukumu inaingiliwa na Wanasiasa,bado wachache wanaamini kwenye kushika HATAMU.Pale wengi watakaposhika HATAMU hao wachache watatafuta kujua ilikuaje awakujua awali.ITAKUWA IMECHELEWA hiyo.
 
Katika kupitisha bill hii waziri mkuu aliungana na wapiganaji kupinga wakuu wa mikoa kuhusiswa na masuala ya mahakama, nadhani kwa kutumia taaluma yake pm aliona busara ya kutowahusisha wanasiasa kwenye mambo ya mahakama. Kilichonishangaza sana ni pale watu ambao wenzetu humu wanawaita wapambanaji kama Samuel Sitta ambae ni mwanasheria kuungana na hao wabunge mbumbumbu wa sheria kuunga mkono upitishwaji wa ile bill!! Mara zote mimi ninawatahadhalisha wanajanvi kuwa huyu Sitta sio mpambanaji wa ukweli bali ni mchumia tumboni. Nawasilisha.

Sasa kama pinda naye ana mashaka na hili alichukua hatua gani kama waziri mkuu na pia kiongozi wa shughuli za serikali bungeni?Ama alitaka kutupa ujumbe gani?Au alikuwa anatuambia kuwa serikali yao imeundwa na watu mbumbumbu,wasioweza kuchanganua mambo?
 
Katika kupitisha bill hii waziri mkuu aliungana na wapiganaji kupinga wakuu wa mikoa kuhusiswa na masuala ya mahakama, nadhani kwa kutumia taaluma yake pm aliona busara ya kutowahusisha wanasiasa kwenye mambo ya mahakama. Kilichonishangaza sana ni pale watu ambao wenzetu humu wanawaita wapambanaji kama Samuel Sitta ambae ni mwanasheria kuungana na hao wabunge mbumbumbu wa sheria kuunga mkono upitishwaji wa ile bill!! Mara zote mimi ninawatahadhalisha wanajanvi kuwa huyu Sitta sio mpambanaji wa ukweli bali ni mchumia tumboni. Nawasilisha.
Kinachonishangaza kuhusu Pinda ni kwamba, kabla muswada kutua Bungeni hupitia ktk Baraza la Mawaziri. Je huko hakuweza kutumia veto yake kuainisha madhara ya muswada huu na kumshawishi bosi wake kutoidhinisha kutua Mjengoni??

Wanazungumza lugha moja hao
 
Watanzania tuamke sasa tuachane na mifumo inayokanganya muhimili wa sheria kuwa kibaraka wa wanasiasa. Hawa wakuu wa mikoa wamekua wakiteuliwa bila hata vigezo maalamu na wengi wao wamekua wanajeshi wastaafu na makada wa CCM mfano mzuri ni Yusufu Makamba ambaye amevuliwa kama gamba huko CCM. Sasa tukiwaachia hawa waithibiti mahakama je hatuoni ni kuiingilia uhuru wa mahakama? Mbona Bunge lina kamati yake pekee ya nidhamu? Mbona hawakuwapa wakuu wa mikoa uwezo wa kuwaadibu wabunge? Huu mswada kila mwenye akili alijua ni mbovu lakaini hata MB Tundu Lissu alipowafumbua macho wa Bunge walikataa kuona ubovu kwa sababu ya kushabikia u-CCM. TLS na wanasheria wengine wapaaze sauti kupinga muswada huu kabla haujasiniwa kuwa sheria nasi wananchi tutawaunga mkono. Ushauri wangu pia rais asiusaini kuwa sheria.
 
Mahakama zetu hazipo huru kabisa.
Yaani wakuu wa mikoa ndiyo wanasimamia nidhamu ya mahakimu. Sasa naelewa ni kwa nini nako mahakamani kuna rushwa. CCM kinachotoa hao wakuu wa mikoa ni chama kinachoabudu rushwa kiasi kwamba usipokuwa mla rushwa unatengwa na wanachama wenzako.
 
Watanzania tuamke sasa tuachane na mifumo inayokanganya muhimili wa sheria kuwa kibaraka wa wanasiasa. Hawa wakuu wa mikoa wamekua wakiteuliwa bila hata vigezo maalamu na wengi wao wamekua wanajeshi wastaafu na makada wa CCM mfano mzuri ni Yusufu Makamba ambaye amevuliwa kama gamba huko CCM. Sasa tukiwaachia hawa waithibiti mahakama je hatuoni ni kuiingilia uhuru wa mahakama? Mbona Bunge lina kamati yake pekee ya nidhamu? Mbona hawakuwapa wakuu wa mikoa uwezo wa kuwaadibu wabunge? Huu mswada kila mwenye akili alijua ni mbovu lakaini hata MB Tundu Lissu alipowafumbua macho wa Bunge walikataa kuona ubovu kwa sababu ya kushabikia u-CCM. TLS na wanasheria wengine wapaaze sauti kupinga muswada huu kabla haujasiniwa kuwa sheria nasi wananchi tutawaunga mkono. Ushauri wangu pia rais asiusaini kuwa sheria.
Sikwaraisi huyu kiburi na ubabe ndo vinamwongoza haoni maumivu ya watanzania kwa kupitisha sheria mbovu .... Ameshapitisha sheria nyingi ambazo nikandamizi.... Hata anaposhauriwa nawatanzania hatakikuskia yeye akimshauri mpinzani anaona hatakikuelewa..... Naomba msihangaike kumshauri mwachenitu...... Twende naye hivihivi mwisho tutafika......
 
Back
Top Bottom