mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Ukianzia Msata hadi Bagamoyo kupitia Kiwangwa na Fukayose kuna mashamba-pori mengi tu. Ukianzia Mlandizi hadi Chalinze hapo kuna shamba-pori za kufa mtu.
Ulielekea Mtwara kutokea Mbagala huko ndio usiseme utadhani kuna kilimo cha vichaka.
Tunaomba mkoa wa Pwani uwe mfano. Zile sifa eti nina hekari 300 mwingine 3000 wakati zaidi ya matunda pori hakuna hata mpapai zifike mwisho.
Nimesema karibu na Jiji kwa sababu jiji la DSM ni lenye watu wengi wenye rasilimali fedha lakini hawana hata shamba 1/8 ya heka.