Wakuu Uzee wa sasa ni ulemavu

Wakuu Uzee wa sasa ni ulemavu

Mi mashine ikiacha kupiga kazi kabisa, naomba Mungu anichukue tu. Kama itaendelea fanya kazi hata nikiwa na miaka 70 basi bado nitaishi huku nikiyaonea maisha wivu mkubwa
Mkuu labda uwe umewekeza ila kama ukiwa mzee alafu haujawekeza hata kama mashine inapiga kazi huwezi pata wakumpigisha kazi.
 
Ni sahihi Ila hata ukiwa na pesa kwa nchi km zetu labda uwe na usaidizi asa huku nani yupo tyr umlipe alee mzee kwa kila kitu, inakuwa na ugumy fulani

Hapo kwenye kuwekeza ndo muhimu zaidi
Ukiwa na pesa niraha Mkuu.

Wapo wa mama wanapewa kazi ya kuhudumia(hii niliona kwenye nyumba moja pale mikocheni wamama wawili wamepewa makazi na mshahara mnono wanahudumia mzee yupo kwenye wheel chair).
 
Hellow JF.

Naomba niseme uzee wa sasa ni ulemavu inaumiza sana.

Inawezekana kwa sasa kwenye ujana tuna fanya kila aina ya mambo(Umalaya, kunywa pombe za aina zote, kula kila aina ya vyakula, kuruka kila aina ya viwanja na night clubs, ufisadi, mabinti wadogo kuanza ngono za hovyo hovyo mapema, vijana wakiume kutoka na mashangazi n.k).

Hayo yote na mengineyo tufanye kwa kiasi wakuu uzee wa sasa ni ulemavu.

Pia katika kula starehe tusisahau kuwekeza hata kidogo ili kama ukibahatika kuuona uzee usiteseke kwa umasikini na ulemavu.
Ushauri mzuri sana mkuu.

Kupanga ni kuchagua.
 
Back
Top Bottom