Wakuu nipeni mbinu kupunguza wivu wa mapenzi

Tafuta maisha mpaka ufikie stage uone future na furaha yako ni muhimu sana kuliko kitu chochote...

At least uwe na uwezo wa kuwa na furaha peke yako hata bila mpenzi wako.

Jua kabisa hauna kinga yeyote dhidi ya usaliti unaweza kusalitiwa mda wowote na siku yeyote na sio wewe peke yako hata natajiri wanasalitiwa hivyo kubali kuna risks zipo ukiwa kwenye mahusiano na moja wapo ni kusalitiwa.

Kama upo Dar nenda Posta pale kaa sehemu angalia jinsi wanawake waZuri walivyo wengi na wanavutia halafu jipe moyo km akikusaliti huyo basi utapata nafasi ya kupata mzuri zaidi na bora zaidi.

Hakikisha unajua direction ya maisha yako hata ikitokea umesalitiwa basi ujisemee nitatumia mda mwingi ku focus na maisha yangu na hobbies zangu...

Usikose hobbies,Hobbies ni muhimu sana sana sana.
Mungu akubaliki mnooo mnoo mkuu, nimevutiwa sana na andishi lako. limenipa nguvu
 
Uyu mpenzi wangu hatujagombana ata kidogo, tupo kwa amani ila nimekuwa na wivu kupindukia, kuna siku kuna mtu aliniambia anamuonaga anaongozana na mtu fulani niliisi maumivu mnoo
 
Jifunze kupotezea vitu vidogo kama hivyo mkuu.
Yani kumkutw busy unakasirika kwani simu yake ni kwa ajiki ya kuwasiliana na wewe tu hana marafiki,wazazi watu wanaomtongoza nk nk. Inavoonekana unambana sana uyo mchumba wako (na hujamuoa aisee).
Tusiende mbali huyo ndo mpenzi wako wa kwanza??
Una kazi ya kufanya?? Kama una kazi na unafanya hayo nitakushangaa kidogo ila kama huna job inakufanya uwe busy basi hicho ni kisirani na mara nyingi wanakuaga nacho wanawake.
Tafuta kazi ikuweke busy mkuu hope wivu wako unamboa mchumba wako.
 
Jamani wakuu nina mpenzi wangu, nimetoka kumpigia simu muda huu nimekuta inatumika, ninahisi wivu umenijaa sana nikatamani kumuambia alikuwa anaongea na nani ila nikapotezea, hebu naombeni mbinu ya kupunguza wivu nilionao maana nahisi unaweza kuja kuniangamiza wakuu.

Ni mpenzi wangu, nipo nae mwaka wa 4 sasa.

Nipo chini ya miguu yenu naombeni ushauri wa haraka sana.
Kuwa busy na kutafuta pesa, usimpigie sim Mpaka akupigie yeye, hio ni kawaida kwa mwanaume.
 
Jifunze kupotezea vitu vidogo kama hivyo mkuu.
Yani kumkutw busy unakasirika kwani simu yake ni kwa ajiki ya kuwasiliana na wewe tu hana marafiki,wazazi watu wanaomtongoza nk nk. Inavoonekana unambana sana uyo mchumba wako (na hujamuoa aisee).
Tusiende mbali huyo ndo mpenzi wako wa kwanza??
Una kazi ya kufanya?? Kama una kazi na unafanya hayo nitakushangaa kidogo ila kama huna job inakufanya uwe busy basi hicho ni kisirani na mara nyingi wanakuaga nacho wanawake.
Tafuta kazi ikuweke busy mkuu hope wivu wako unamboa mchumba wako.
asante sana kwa mawzo yako mkuu, nimeyapokea
 
Mzee Kuna jicho la nyama na jicho la kiroho .

Hivyo ningependa kukusihi sio Kila hisia ni za kuzipuuza. Ila sio kwenye Kila hisia basi ufanye maamuzi.

Kama hizo hisia za wivu zinakujia ukiwa haupo lonely sio za kuzipuuza na sio za kuzichukulia maamuzi kwa kukurupuka.


Kuna hisia nyingine zinakupa tahadhari hivyo ni wajibu wako kuanza kufuatilia kimya kimya bila muhusika kujua Kama anaguatiliwa. Vijana wa sasa wengi wetu tunamihemko Kama wanawake mwanaume kuumbiwa kifua sio Cha kwenda kubebea vyuma vizito jimu.

Mimi binafsi kabla sijaoa nilikua napiga simu ila kuna simu nyingine ukikuta mtu yupo busy lazima moyo ukuume na ushikwe na wivu hapa huwa naamini katika ulimwengu wa kiroho kuwa mambo hayapo sawa kwa nn moyo uume wakati sometimes moyo hauumi hata nikute busy masaa matatu.

Kama jicho lako la kiroho ni Safi na linaona basi we jua tu huko mambo si shwari. Najua kuna mijitu italeta ujuaji hapa na kujifanya ndio imesoma Sana na vielimu vyao vinamajibu ya Kila kitu.

Lkn hili jicho la kiroho Lina majina mengi wahuni wa kitaa wanaita machale ....ndio maana utasikia machale yalinicheza.... Waganga huita mizimu....wachungaji huita roho mtakatifu. Nk

Sometimes unaweza ukawa tu officn unafanya mambo yako lkn roho yako inastuka na haituliii juu ya mpenzi wako yaani unajikuta tu inauma bila sababu za msingi we jua tu katika ulimwengu wa kiroho mambo hayapo sawa mtu ulifungamana nae huko usaliti unaendelea.


Hivyo upatapo hisia Kama hizo usikurupuke kuchukua maamuzi zifanye Kama ndio chanzo Cha kuanza kufanya utafiti ili kubaini ukweli na sio kuanza kukurupuka kuuliza au kutukana na kufoka utapoteza ushahidi hivyo bila kumstua victim wako Anza kumfuatilia taratibu ili kutafuta ushahidi ambao utaonekana katika jicho la nyama .

Mara nyingi nimekua nikifanya hivyo na nimefanikiwa Sana na sijawahi jutia.
 
Back
Top Bottom