Wakuu nini itakuwa mbadala wa mifuko ya plastiki?

Wakuu nini itakuwa mbadala wa mifuko ya plastiki?

Kawaulize Zanzibar wao wameshasahau kama kuna kitu kinaitwa mifuko ya plastic
 
Hofu yangu isiwe tunamtengenezea supplier wa mifuko flani kutoka Kenya
 
Mama anaenda kuvuliwa nguo huyu hadharani, ngoja tusubiri time will tell!
 
Wana Kagera hawatapata shida
IMG-20190508-WA0014.jpeg
 
Wenye capital ndo muda muafaka wa kutengeneza ile mifuko ya kaki na local vikapu kwa wingi
Kumbuka hiyo mifuko ya kaki ni zao la miti kwahiyo tutegemee uvunaji mkubwa wa misitu. Hii nayo after a long run yaweza kuwa tatizo lingine la kimazingira
 
Leo asubuh I nimepata ujumbe unaopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastic kuanzia June 1 na unasomeka hivi...

"Serikali imekataza mifuko ya plastiki kuanzia tarehe 1 JUNI 2019. Faini au Vifungo vitatolewa kwa atakayezalisha, kuuza au kutumia mifuko hiyo. Achana nayo leo!"

Je mbadala wa hii mifuko ni upi, maana naona wengi wakienda kupiga faini, kufirisika na wengine kama sio kufungwa!

Waliopiga marufuku akili yao ni kuzuia tu, mbadala hawana. Ila itabidi utumie vikapu vya ukindu au bahasha za kaki kwa vitu vikavu.
 
Mtajua wenyewe sisi tunajua kupiga marufuku bila kujali elimu wala yafuatayo... ndio maana kuna zao linabanguliwa kwa meno siku hizi.. 😀 😀
 
Waliopiga marufuku akili yao ni kuzuia tu, mbadala hawana. Ila itabidi utumie vikapu vya ukindu au bahasha za kaki kwa vitu vikavu.
Wakiulizwa watajibu "ni amri kutoka juu..." athari ikishajitokeza Bwana Mkubwa atainuka kusema "wananchi wasibughudhiwe..."
 
Nafanya Uzalishaji wa mifuko ya Khaki, na-brand na kuweka logo.
Haya PM ipo wazi kazi kwenu.
 
TANZANIA PLASTIC BAGS BAN.

For all travelers coming to Tanzania its imperative to note the information below to avoid delays on arrival at any one of our airports. Please share with your fellow agents, operators, clients, colleagues, guests and friends so the transition is seamless.

Effective 1st June 2019: All passengers arriving at any Tanzania airport including tourists can possibly face very heavy fines for using plastic bags in any way, shape or form. Using, manufacture or importation of plastic bags, including garbage bags and shopping bags is illegal. Offenders, including tourists, could face very heavy fines.

Visitors/Citizens and Residents alike are advised to avoid packing any plastic bags in their suitcases or in carry-on hand luggage before flying to Tanzania. Items purchased at the airport before boarding the aircraft should be removed from plastic bags. Please check hand luggage before disembarking at entry points and any plastic bags should be left in the plane.

Similarly the transparent "zip-lock" plastic bags that some airlines require passengers to use for keeping liquids, cosmetics, toiletries etc separately in hand luggage are also not permitted to be brought and should be removed and left on the plane before disembarking."
...................................................................................................................................................................................................................
Wazungu wanamsemo "beggars cant be choosers"

Na sisi tunamsemo "maskini jeuri"

Mpaka dakika hii wazalishaji walishatakiwa wana supply hizo bidhaa in large quantities, wauzaji walishatakiwa kuwa wame adapt, watanzania washaanza kutumia hiyo mifuko mbadala na wenye plastic bags inventory washamalizia.

Sasa kama kuna mtu anauliza swali la mbadala leo ina maana wenye maduka bado hizo bidhaa awajaanza kuzipata na zuio lenyewe ni kama wiki tatu lianze.

Anyway wenyewe wanasema wamelifikiria vya kutosha na wamejipanga strategically kuona kuna smooth transformation.

Sie wengine tunasema this is a bad idea, nothing personal but the whole thing is just a bad idea; time will tell.
 
Naomba kuuliza kwa sisi tunaofanya biashara ya kuuza ubuyu, karanga, icecream na bisi? Je mifuko hii ya kufungia bidhaa hizo imepigwa marufuku pia?
 
Sasa hivi watu wanabeba majagi bakuli sufuria kwenda dukani, na kama mtu alizoea kupitia mtake hanunui tena.

Huyo mbadala wala hatakuwa na soko tayari walaji wameshajeruhiwa kisaikologia.

Lakini tumejiuliza ni kodi kiasi gani itapotea? Biashara nyemelezi ngapi zitakufa? Zile chips za kufungiwa kwenye rambo hazipo tena.

Kwanini wasingewajengea uwezo wamiliki wa viwanda vya plastic kununua mitambo ya kuchakata hizo plastic na kutengeneza ndoo viti bakuli sahani?
 
Kama kweli mifuko ina madhara kwanini ilengwe inayotumiwa na masikini tu? Kwanini mifuko ya sukari cement mbolea iendelee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom