Wakuu nini itakuwa mbadala wa mifuko ya plastiki?

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
13,142
27,103
Leo asubuh I nimepata ujumbe unaopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastic kuanzia June 1 na unasomeka hivi...

"Serikali imekataza mifuko ya plastiki kuanzia tarehe 1 JUNI 2019. Faini au Vifungo vitatolewa kwa atakayezalisha, kuuza au kutumia mifuko hiyo. Achana nayo leo!"

Je mbadala wa hii mifuko ni upi, maana naona wengi wakienda kupiga faini, kufirisika na wengine kama sio kufungwa!
 
Mzee hiyo ni fursa
 
Hii nchi ya hovyo kabisa watu wanamzigo mwingi viwandan then wanatoa siku 60 walitakiwa kutoa miezi 6 wao wanaona kuwaumiza wananchi ni jambo zuri.
 
Lakini serikali huko ilishawahi kutoa tamko zito juu ya mifuko hii (Kama sikosei Dr.Shein na Dr.Kikwete) sijui hilo tamko liliishia wapi.Ila mifuko ya plastic ni kero na hasa kwny kuziba mitaro ya maji
 
Yaani hata mm sielewi, ukisema mifuko ya khaki, misitu itaisha.. Nadhani hii tabia ya kuzuia product moja kabla hujapata mbadala wake ni kosa kabisa
 
Lakini serikali huko ilishawahi kutoa tamko zito juu ya mifuko hii (Kama sikosei Dr.Shein na Dr.Kikwete) sijui hilo tamko liliishia wapi.Ila mifuko ya plastic ni kero na hasa kwny kuziba mitaro ya maji

Sasa mbadala wake ni nn?
 
Kwa jiwe anavyopenda sifa huu utakuwa mwisho wa uwaziri wa january makamba,atatengua kauli.

Hili la jiwe kujitwalia kiki naliona linakuja..
Kuzuia mifuko ya plastiki ni jambo jema sana kufanyika...
Lakini huwezi kukataza matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kutoa toa matamko.. Bila kujipa muda wa kutosha kuuelimisha umma!
Hayo matamko yalishawahi kutoka siku za nyuma lakini hakuna matokeo chanya yaliyopatikana..
Serikali kama kweli ina dhamira ya dhati kabisa kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki ni vyema ingejielekeza katika kuelimisha umma na kuibua bidhaa (mifuko) mbadala..
Bidhaa (mifuko) itakayokidhi vigezo iainishwe na kutafitiwa kwa kina tusije tukawa tunaruka maplastiki alafu tunaibua changamoto nyingine nyingi!
Uhamasishaji na matumizi ya bidhaa (mifuko) itakayokidhi vigezo yaende sambamba na mifuko iliyopo ya plastiki kwa kipindi chote hiki cha mpito..
Tukumbuke kitu kimoja.. Serikali ipo kwa ajili ya wananchi.. Ni wajibu wao kubuni vitu na mbinu mbali mbali za kuwapunguzia adha, kero, karaha ama mizigo isiyokuwa ya lazima..!!

Hivi kweli unasitisha mifuko ya plastiki ifikapo Juni 01; alafu wananchi watumie nini? Je, hayo watakayotumia ni salama zaidi kuliko hii miplastiki..!!
Tujipe muda wa kutosha!
 
Leo asubuh I nimepata ujumbe unaopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastic kuanzia June 1 na unasomeka hivi...

"Serikali imekataza mifuko ya plastiki kuanzia tarehe 1 JUNI 2019. Faini au Vifungo vitatolewa kwa atakayezalisha, kuuza au kutumia mifuko hiyo. Achana nayo leo!"

Je mbadala wa hii mifuko ni upi, maana naona wengi wakienda kupiga faini, kufirisika na wengine kama sio kufungwa!

Samahani Mkuu naomba Kuuliza hivi ' Condoms ' nazo ni Mifuko ya ' Plastiki ' au?
 
Bongo nyoso,viongozi wanakurupuka,mahitaji ya mifuko ya plastic ni makubwa sana daily,wangeanza mchakato wa kutengeneza mbadala wake zamani ,then hiyo mifuko ita be replaced automatically
 
Back
Top Bottom