Wakuu msaada wa mawazo tafadhari

Mjusi Sharobalo

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2025
Posts
8,371
Reaction score
14,733
Wakuu salamu....

Moja kwa moja ndani ya mada wakuu.

Kuna mdafa alinipenda sana na mimi nilimpenda, mimi nilizoea kumuita mshangazi sababu kanizidi kama miaka 5 hivi.

Alikuwa na kazi yake na mimi kazi yangu, wakati huo tunaanza dhambi zetu alisisitiza sana kupata mimba huenda likawa janga ila mimi nilimwambia hizo ni baraka mazee.

Sasa kama mwezi wa saba hivi hapo nyuma akaipata kweli kazi akashindwa kufanya kabisa maana ilikuwa ni mimba kisirani inataka kulala tu. sijui ndo nini yaani na mimi mwenyewe gafla boss kawa kapuku kiufupi kapoteza mali zote.

Sasa hapo mzigo mzima ukatua kwangu, gafla wakuu nimepoteza ramani na sina dira mazima hadi nashindwa kuelewa. Hapa nawaza nimtoloke tu huyu mshangazi nisepe zangu ubushini nikachunge tu mikia wakuu.

Mnanishauri nini hapa.
 
Mzee wewe si ulimuambia hizo ni baraka mbona unakimbia baraka mzee baba

Unajua saa nyingine sisi wanaume ndiyo chanzo cha matatizo
Komaa na matatizo yako uliyoanzisha
 
Hiyo ni baraka
 

Mara kadhaa kabla ya kupata baraka kubwa. Unaweza kupata misukosuko kadha wa kadha. Ila ukivuka hiyo misukosuko. Huwa hiyo baraka inakuwa kwa namna hukuwez hata kudhania.

Je mnakaa na huyo Dada pika pakua?..au kila mtu anakaa kivyake.

Kwanamna yoyote ile. Usimkimbie huyo dada wa watu. Fikiria namna ingne.
 
Bwana mdogo sizani kama kukimbia ni tatizo. najua ukikimbia atateseka na huo uja uzito, utamuongezea fedheha katika maisha yake, atajiona kama amelaaniwa, atatokwa machozi ya kukutakia mabaya.. akijifungua, ipo siku mtoto atamuuliza "Mama baba yuko wapi" atashindwa kumpa jibu sahihi, labda atamdanganya mtoto.
ipo siku utasema "damu yangu haipotei bure, nikamchukue mwanangu", hapo unakuta alishajitokeza mwanaume mwenzako amekaa na huyo mshangazi, amemenyenyekea na amemsaidia kumlea mtoto. hafu unajitokeza tu from nowhere unabana pua yako "Yule ni damu yangu naenda kumchukua"

kama unahitaji mfumo wowote wa shule, biashara , ofisi, basi nipigie hapa 0620224372 au whatsapp.
tembelea tovuti yangu uone mifumo iliyopo tayari BONYEZA HAPA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…