Wakuu hivyo nataka kuuliza hii michezo Unapata hela kweli?

Abbasfarudume

JF-Expert Member
Feb 14, 2017
1,625
1,324
63aef97eb9d79969e94cdc10a90f8a04.jpg
690cb75f8144b085b1f73a70069c41a2.jpg
 
Maana Utaona mtu anakurushia link na kukwambia jiunganishe na hii link fuata maelekezo Utapata Pesa ebu wenye Uelewa wa huu mchezo tafadhali msaada kidogo mtueleweshe
 
Unaibiiiwa....
Lkn hiyo link Utoi pesa yako mfukoni kucheza wala card ya benk wao wanataka Ujaze email address yako jina lako namba yako ya simu vigezo na masharti yao ya mchezo Ukizingatia wanakutumia email yao Uende westion union money ukachukue hela
 
Binafsi sijajishughulisha na hizo link ila kuna watu zaidi ya watatu nimeambiwa kuwa kweli unapata hela coz wameshafanikisha kulipwa. Mengine zaidi sifahamu kwakweli
 
Kumbe unajua basi fanya hivyo halafu uje utuletee mrejesho mkuu
 
Hela inapatikana mtu akifanya kazi tu, sio online.... Watanzania hebu tuanze kufunguka akili sa sa.
 
Lkn hiyo link Utoi pesa yako mfukoni kucheza wala card ya benk wao wanataka Ujaze email address yako jina lako namba yako ya simu vigezo na masharti yao ya mchezo Ukizingatia wanakutumia email yao Uende westion union money ukachukue hela
Hapo ni kwenye kujiunga,itafika wakati wakutoa hizo hela feki utaambiwa ujaze hizo ac number either ni bank or credit card au paypall ambapo utatoa email yako ya paypall . Hiyo ni scam mkuu kweli upate $ 1000 kwa kuclick tu tena kwa siku kadhaa unadhani ingekuwa kweli watu wangekuwa wanatafuta ajira. Piga kazi.
 
Ni kupotezeana muda na ziko nyingi lakini muonekano ni ule ule.
Hutokaa utoe hiyo ela ukimaliza utaambiwa invite 40 referrals, ili uweze kutoa ela au lipia 5-10 usd.
Ukiwapata hao wengine 40, utaambiwa ela imetumwa lakini hutokaa uione.
Wanaokwanbia wamelipwa ela ni waongo na wengine wanadiriki hadi kukuonyesha picha eti ela imepokelewa mpesa na wote wanaofanya hivyo wanatumia screenshot ile ile.
 
Binafsi sijajishughulisha na hizo link ila kuna watu zaidi ya watatu nimeambiwa kuwa kweli unapata hela coz wameshafanikisha kulipwa. Mengine zaidi sifahamu kwakweli
Hao wote waliokwambia wamekudanganya hiyo ni SCAM na hautokuja kupata hata shilingi, lengo la hizo website na nyinginezo ni kupata e-mails na pia kufanya site yao kuwa popular, unajua kwa nini wanahitaji info zako? kaa chini na uchunguze usipende tu kwa kuambiwa.
 
Usijaribu kuprovide detail zako mtandaoni kupitia link zinazosambaa kweny magrup ya whatsapp. Wezi wa mtandaoni hutengeneza link hizo na kuzisambaza kwenye magrup ya wanavyuo wakiamini kwenye grup la watu 100 lazma 10 watanaswa na kuamini kuwa wataearn money, ukishajaza tu pale namba ako na email ujue taarifa zako haziko salama. Kwan _hackers_ hutumia mfumo wa kukufatilia kupitia system ya computer _typing stroke drawer_ yaan kila ukibonyeza tu keyboard ya device yako kule wanaona kupitia pattern za system zao, baada tu ya kujaza taarifa hizo wanaweza kujua kila unachofanya kweny cm yako.

Cha kufanya epuka kujaza taarifa za benk, email, na kuingiza password unazoelekezwa kupitia link hizo, hakikisha unaletewa verification code unapojaza taarifa za transaction, usipopewa ujue taarifa zako zipo mikononi mwa mahackers.
Kuthibitisha hili jaribu kuingia kweny link hizo baada tubya kujaza taarifa kama account ya benk utailona step inayofuata haieleweki mara matangazo ujue ushanaswa.
‌‌‌‌‌‌‌ email ina kazi kubwa kuliko unavyoifikilia, na mtu yeyote anaetumia mitandao ya kijamii kama whatsapp huwa nayo hiyo kitu. Na inauwezo wa kutoa taarifa zako zote unazofanya kupitia simu yako kwamtaalamu wa internet.
_"Delete" futa kabisa by Brado
 
Back
Top Bottom