Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Dah ly walikuwa wanatutesa sana madogo kipindi hicho yaan walikuwa wakubwa kwa saiz ni vitoto tu eti la saba. Kipindi kile hadi maticha walikuwa wagwaya baadhi ya wanafunz
 
Rishure baya nilisomea yaani kule ni kilugha tupu.kiswahili ni msamiati.
Utakisomea tu.

karibu robo tatu ya drs hawajui kusoma na kuandika hkn hata mtoto mmoja aliwahi shinda kwenda sec. Mpaka leo

Hata humu sijawahi sikia mtu kutoka Shule yangu hiyo ya...

Kibumaye Shule ya Msingi
SLP 172
Tarime Mara.

Japo mazingira ya shule ni mazuri.mitafi mingi lkn
mputyuuu! Km yumo humu aliyesoma hapo aseme kitu.

Mie nilihama nikiwa drs la nne huko niliko kwenda palikuwa tofauti kabisaaaa.....
 
Nilichapwa viboko 109 kisa kukamatwa na msichana
Wandugu,

Thread hii ni mahususi kwa chochote unachokumbuka enzi unasoma shule ya msingi.

Mimi binafsi nakumbuka enzi zile nasoma Issale primary school kule wilayani Mbulu miaka ya 1986-1991 wanafunzi tulikuwa nadhifu, tunaopenda shule, wenye heshima sana. Pia nakumbuka tulikuwa tunacheza halaiki shuleni na hata kwenye matukio kama ya mbio za Mwenge au Kiongozi wa kitaifa akitembelea wilaya yetu. Moja ya nyimbo za halaiki zinazonikuna mpaka leo ni hii hapa;

" Chama chetu kilituongoza hadi uhuru tulipoupata na kinaendelea kuongoza kufikia lengo ujamaa... Mwenyekiti Mwl. Nyerere mwenye hekima na wingi wa Sifa Tanzania..."

Ama kwa hakika enzi hizo zilikuwa tamu sana na tulipokuwa tukiimba nyimbo hizi tulikuwa tunanyoosha mkono kuelekea kwenye picha ya Baba wa Taifa wakati huo akiwa mwenyekiti wa chama na Raisi wa Tanzania.

Pia nakumbuka kuna waalimu fulani ambo walikuwa wamepitia mafunzo wa JKT basi zamu zao zikifika wanapiga magwanda na wiki hiyo inakuwa mchaka mchaka sio mchezo. Bila kusahau kukimbia mchaka mchaka asubuhi au tukienda kuchota maji Lambo na madumu ya lita tano huku tukiimba nyimbo za uhamisishaji kama;

" Mchaka mchaka chinja... Aliselema....na Mbuga za wanyama Tanzaniaaaah ya kwanza ni Serengetiii Ngorongoroooh Manyaraaa na Mikumiii oooh Tanzania hoooye....

Ni hayo tu kwa leo, je na wewe ulisoma shule gani ya msingi na wakumbuka nini?
 
Siwezi sahau nimekula njiti sana

Tafadhali mwenye mawasiliano au mwenye kujua alipo aliyekuwa headmaster wa wa Mirambo sec. Tabora huko, aliitwa LC MUSSATA, miaka ya 1987.
 
Niliwah fungiwa kwenye maktaba kisa balua aliyoandika rafiki yangu afu akaweka jina hapo ilinibidi niwapiga kitabu
 
Back
Top Bottom