ukichokozana na mwenzako unamwambia tutapigana saakumi
nakulikuwa na sehemu ya kupigania
Wandugu,
Thread hii ni mahususi kwa chochote unachokumbuka enzi unasoma shule ya msingi.
Mimi binafsi nakumbuka enzi zile nasoma Issale primary school kule wilayani Mbulu miaka ya 1986-1991 wanafunzi tulikuwa nadhifu, tunaopenda shule, wenye heshima sana. Pia nakumbuka tulikuwa tunacheza halaiki shuleni na hata kwenye matukio kama ya mbio za Mwenge au Kiongozi wa kitaifa akitembelea wilaya yetu. Moja ya nyimbo za halaiki zinazonikuna mpaka leo ni hii hapa;
" Chama chetu kilituongoza hadi uhuru tulipoupata na kinaendelea kuongoza kufikia lengo ujamaa... Mwenyekiti Mwl. Nyerere mwenye hekima na wingi wa Sifa Tanzania..."
Ama kwa hakika enzi hizo zilikuwa tamu sana na tulipokuwa tukiimba nyimbo hizi tulikuwa tunanyoosha mkono kuelekea kwenye picha ya Baba wa Taifa wakati huo akiwa mwenyekiti wa chama na Raisi wa Tanzania.
Pia nakumbuka kuna waalimu fulani ambo walikuwa wamepitia mafunzo wa JKT basi zamu zao zikifika wanapiga magwanda na wiki hiyo inakuwa mchaka mchaka sio mchezo. Bila kusahau kukimbia mchaka mchaka asubuhi au tukienda kuchota maji Lambo na madumu ya lita tano huku tukiimba nyimbo za uhamisishaji kama;
" Mchaka mchaka chinja... Aliselema....na Mbuga za wanyama Tanzaniaaaah ya kwanza ni Serengetiii Ngorongoroooh Manyaraaa na Mikumiii oooh Tanzania hoooye....
Ni hayo tu kwa leo je na wewe ulisoma shule gani ya msingi na wakumbuka nini???
Kulikuwa kuna kitu inaitwa bong'oa,ukiinama tu mzee teke la adabu litakuhusu then kulikuwa na kupinga kuhusu vitu vya kula kula ukishika vibaya tu wamepokonya na unaachiwa masikitiko tumi nakumbuka uketo, yaan ikua lazima kila siku nikaange mahindi na kuyaloweka kama msosi saa nne.
mi nakumbuka uketo, yaan ikua lazima kila siku nikaange mahindi na kuyaloweka kama msosi saa nne.
Aisee mimi mchezo ulinitawala sana kufua nguo ilikua ni JUmapuli SAA moja usiku nakausha navpasiWandugu,
Thread hii ni mahususi kwa chochote unachokumbuka enzi unasoma shule ya msingi.
Mimi binafsi nakumbuka enzi zile nasoma Issale primary school kule wilayani Mbulu miaka ya 1986-1991 wanafunzi tulikuwa nadhifu, tunaopenda shule, wenye heshima sana. Pia nakumbuka tulikuwa tunacheza halaiki shuleni na hata kwenye matukio kama ya mbio za Mwenge au Kiongozi wa kitaifa akitembelea wilaya yetu. Moja ya nyimbo za halaiki zinazonikuna mpaka leo ni hii hapa;
" Chama chetu kilituongoza hadi uhuru tulipoupata na kinaendelea kuongoza kufikia lengo ujamaa... Mwenyekiti Mwl. Nyerere mwenye hekima na wingi wa Sifa Tanzania..."
Ama kwa hakika enzi hizo zilikuwa tamu sana na tulipokuwa tukiimba nyimbo hizi tulikuwa tunanyoosha mkono kuelekea kwenye picha ya Baba wa Taifa wakati huo akiwa mwenyekiti wa chama na Raisi wa Tanzania.
Pia nakumbuka kuna waalimu fulani ambo walikuwa wamepitia mafunzo wa JKT basi zamu zao zikifika wanapiga magwanda na wiki hiyo inakuwa mchaka mchaka sio mchezo. Bila kusahau kukimbia mchaka mchaka asubuhi au tukienda kuchota maji Lambo na madumu ya lita tano huku tukiimba nyimbo za uhamisishaji kama;
" Mchaka mchaka chinja... Aliselema....na Mbuga za wanyama Tanzaniaaaah ya kwanza ni Serengetiii Ngorongoroooh Manyaraaa na Mikumiii oooh Tanzania hoooye....
Ni hayo tu kwa leo je na wewe ulisoma shule gani ya msingi na wakumbuka nini???
Umenikumbusha hako kamchezomm kwakweli nakumbuka kuwekea watu vioo chini ili niwachungulie,pia nakumbuka siku ya usafi likuwa ni j3 na alhamisi nilikuwa nafua lesso ili kucha zing'ae
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mm kuanzia darasa la tano hadi la saba nilikuwa napangiwa mwanafunzi wa kike, hafu mwalimu alikumshenzi anampanga ambaye uwezo wake darsani upo chini ili nimsaidie, ila yule binti hakufaulu ingawa aliolewa hadi Leo anakijana wake yupo Chuo kikuuNakumbuka kukalishwa benchi moja na mtoto wa kike afu nahama nilikua naona ujinga ila saivi nikiona picha za huyo binti naumia mno roho, kumbe mwalimu wangu alikua na nia njema
Sent using Jamii Forums mobile app