Wakulima wanapata posho gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakulima wanapata posho gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 21, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Baada ya kikundi cha watu wachache kujitengenezea mfumo wa posho kama mastahili ya kujikimu watu pekee ambao hawapokei posho japo ndio wanafanya kazi kubwa zaidi ni wakulima.

  a. Mkulima anapolima mazao na kuyahifadhi anapata posho gani ya kufanya kazi yake kama mkulima? - farming allowance? alipwe na nani?

  b. Mkulima anapopata upungufu wa mazao kutokana na hali mbaya ya hewa, soko n.k anapewa posho gani ya kujikimu kwa siku? Ili kumsaidia kumudu gharama za maisha? au hizi gharama za maisha zinawagusa watu wenye ajira rasmi tu?

  c. Mkulima analeta mahindi, ndizi, nafaka nyingine, matunda hadi kwenye masoko makubwa say Kariako, Tandale n.k au Ngamiani pale Tanga je anapoouza mazao hayo analipwa posho ya kusafirisha (transportation allowance); je anaweza kudai "transportation allowance" au yeye anabeba gharama ya kusafirisha na kuiingiza kwenye bei ya vitu anavyouza? Vipi allowance ya vikao vya majadiliano ya bei (negotiation allowance) kwa muda anaotumia kufanya dili na wanunuzi?

  d. Mkulima wetu huyu ambaye tunaambiwa ndiye anayeshikilia nchi kwa jasho lake anapotumia usafiri wake kuleta mazao kutoka shambani hadi sokoni au kwenye sehemu ya mauzo analipwa posho ya mafuta (gas allowance)? Au hatujali mazao hayo yanafikishwaje sokoni?

  e. Hakuna kazi ngumu kama ukulima hasa ukulima wetu ambao bado unategemea sana jembe la mkono. Maandalizi ya shamba, kulima, kulinda mazao na hata kuja kuvuna ni kweli ni kazi ya "jasho" la mtu literally. Lakini mbona wanapoenda kuuza hasa wanapoiuzia serikali kwanini pamoja na kununua mazao serikali haiwalipi hardship allowance? Au wao hawastahili?

  Ninachouliza hasa ni kuwa kwanini ni watumishi walioajiriwa katika sekta rasmi tu ndio wanalipwa hizi allowance ambazo hawataki kuziachia? Wakulima wetu mbona hata ruzuku hawapati (wenyewe wanapewa vocha! siyo fedha!). Kwanini hatuwapi ruzuku wakulima - ya fedha au allowance kusaidia kumudu maisha yao kama tunavyowapa watumishi wa umma na hata wengine wa sekta binafsi ambao tunaambiwa ati maisha ni magumu kweli kwao? Hivi wakulima wa Tanzania wanapata maisha mazuri kuliko ya watu wengine?

  Jamani vipi kuhusu wanakijiji wenzangu wakulima? Tunawapa ahueni ipi katika mapato yao? au ndio yale yale "tutaboresha soko la mazao yetu ili wakulima wapate bei bora za mazao?".. Really? Au ni kwa sababu wao hawana uwezo wa kuiba waziwazi kama hawa wengine?
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  wauza kahawa walikuwa wanapewa kitu kinaitwa mabaki..sema kahawa ishakufa
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ndio maana vijana wengi sana wanachukia kilimo....Unapata pesa baada ya kumenyeka kwa mwaka mzima na wakati mwingine mvua zinakufanyia mtima nyongo unaambulia patupu. Ila ukiwa machinga au mfanyakazi ....una uhakika wa kuiona msimbazi wakati wowote!!

  Ila kwa mwendo huu wa kuwanyonya wakulima, ipo siku wote watagombea ubunge....Naamini hapo ndipo kila mtu atakapolijua jiji na joto lake!!
   
 4. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tatizo haiko kwenye Katiba na Kanuni za Watawala.....what a shame reasoning!!!

  Ndio maana kila jibwa lililochoka ku-fight kwa kanuni halisi linakimbilia kugombea ubunge
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kinachoniudhi mimi ni kuwa kuna kakikundi cha watu ambacho kanaamini kuwa kanastahili zaidi kwenye hii keki ya taifa kwa sababu tu kenyewe ndio kamepewa visu na uma kuikata keki hiyo.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwa Tanzania kuwa mkulima ni aina ya adhabu na kazi ya dhalili!
  Hata tenda kubwa za kusupply pembejeo za Kilimo wanapewa watu walioko pale mtaa wa Azikiwe!
  Posho?....ya nini kwa mshamba?
   
 7. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  Unajua Mwanakijji kama hawa watu wangekuwa wanajali basi wangefanya hivi

  Kwenye viti maalum vya ubunge kungewa na nafasi moja au mbili ya wakulima bora kila mkoa au wilaya. kama kuna nafasi maalum za wanawake na walemavu nadhani si vibaya wakulima ambao ni disdavantage but important group ingekuwa na muwakilishi japo mmoja kila mkoa.

  Kila mwaka kutokna a na uzalishaji wa mazao au mifugo basi mkulima fulani agekuwa anachaguliwa kuwailisha kila mkoa kwenye bunge la kila mwaka. Nao waonje posho . teh teh teh .
   
 8. Bob

  Bob JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 10, 2007
  Messages: 277
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mfano wabunge, ndio wenye jukumu la kutunga sheria.
  Sasa wanapotunga sheria ya kujilipa posho ya kikao, hii sio ndio inayoitwa "the conflict of interest"?
  Swali, ni nani atakuwa mtatuzi wa hii conflict?
  I'm just cooking my brain ............!
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Naomba nitoe maelezo tofauti kwa ufahamu wangu..... BAKI haikuwa posho hata chembe. Ilikuwa ni malipo halali kutokana na price flactuations kwenye soko la dunia. Ni hivi, wakulima wa kahawa (wooote) walikuwa wanauza kahawa yao kwenye vyama vya ushirika i.e KNCU. Sasa KNCU ananunua kwa bei ya wakati huo (current price) lakini wakati wa mauzo bei inabadilika kwenye soko la dunia na kuwa juu hivyo anapata faida zaidi ya initial projections. Ni kutoka kwenye hiyo nyongeza ya faida ndiyo BAKI inalipwa na ndio maana BAKI ilikuwa ina-flactuate mwaka hadi mwaka hata kama kiasi cha kahawa ulichouza kinalingana. Kumbuka kahawa iko kama oil. price kwenye soko la dunia inabadilika kila mara. Hata hivyo hii concept na implementation ya BAKI naweza kusema iliwezekana tu kwa sababu ya uaminifu/ethics za watawala wetu kipindi hicho. Sasa hivi kahawa ikinunuliwa ni kimoja!
   
 10. G

  GEOMO Senior Member

  #10
  Jun 22, 2011
  Joined: Jul 11, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kwakweli umelitolea ufafanuzi mruri na ambao ndio ukweli wenyewe. na jingine la kuwa ilikuwa iknawezekana kwa sababu ya uaminifu wa wakati huo nalo ni ukweli mwingine uliotukuka. na kwa sasa wanafanya hivo baada ya kuwa wameishajihakikishia kuwa wameua kila kilichokuwa kinasimamia haki ya mkulima iwe ni vyama vya ushirika hata kama vipo si kwa manufaa ya mkulima tena, miiko ya uongozi ndio hiyo waliizikia zanzibar na hata wale waliokuwa wanaiamini na kuisimamia waliisha wazika wote sasa ni utawala ndio umeshika hatamu hakuna uongozi wala utumishi wa umma ni UTAWALA MTINDO MMOJA
   
 11. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  hata mimi utingo nawasaidia wakulima na wachoma mikaa kuuingiza mjini wengine nawafungia juu ya malori kwa TOZO dogo sana, sihitaji posho, nahitaji ruzuku!
   
 12. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,229
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Hata km nina ajira rasmi siwezi kushabikia uroho huu na ulafi uliobarikiwa kwa kupewa jina la kiungwana...maana kwa kufanya hivyo nitakua nimemsaliti mama yangu aliyebinafsisha nguvu zake za mwili bila posho kwa kukakamata jembe sawasawa hadi leo hii walao najua nini tofauti ya ujira na posho...ni broilers pekee wanaoweza ku support hizi 'what so ever allowance' lakini kwa sisi watoto wa kienyeji si jambo la kusherehekea hata kidogo!
   
 13. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Swali zuri bwana Mwanakijiji. Ni wapi hayo uliyoauliza yanafanyika? Tupe uzoefu maana wewe mwenzetu exposure yako ni kubwa sana!
   
 14. M

  Maganiko Senior Member

  #14
  Jun 22, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji,

  Wenzako watakwambia kwenye Income tax Act (na pia VAT) kuna allowances, sijui wanayaita capital goods au stuffs like that kwenye pembejeo na kilimo. Swali langu ni hili, hivi hawa watunga sheria zetu kwelu wanaamini mzee wangu wa huko Ikungulyabashashi anaweza kufunua "schedule" ya Income tax Act kuona hizo allowances?

  Pili utatofautiana sana na hao "wakulima". Wenzako wakiongelea wakulima ni makampuni, au kwa lugha yao "wawekezaji". All of sudden it comes to one certaion thing, makampuni ya madini (wawekezaji) ndio wafaidika wakubwa kwa sera za nchi hii, wakulima (makampuni & wawekezaji) ndo wafaidika wakubwa, wachimba madini wadogo ni wezi na/au wavamizi so wanachostahili ni kufukuzwa tu, "wakulima" wetu wengine hawajui hata kuna hizo allowance, wanachojua ni mbolea, bei bora, mvua ipo au haipo basi.

  Conclusion: Nchi hii usipokuwa mmoja wa waheshimia kujilipa posho, au kampuni ya madini/ukulima au kufanya kazi katuika maeneo hayo, nakuhakikishia you're guarantee to live on hell. Tazama wamachinga, hao wakulima, walimu, etc na uniambie
   
 15. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda kulingana na vyama vya ushirika husika,kule kwetu Nanyumbu kwa mwaka jana wakulima walilipwa korosho kwa awamu tatu. yaani kwanza walilipwa malipo yao halisi.korosho zilipouzwa nje ile faida (ziada) ilipelekwa kwa wakulima wakalipwa kwa mara ya pili, chama tena kikatoa posho (malipo ya tatu) kwa wakulima. Mwaka huu mkuu wetu wa wilaya ya Nanyumbu aliongoza wakulima katika kilimo cha choroko,tena kwa vitendo, yaani yeye mwenyewe alilima takriban hekari 8 za choroko na kwa hakika alipigana kufa na kupona kufuatilia masoko ya choroko, ambapo mafanikio yameonekana kwani kilo moja ya choroko mwaka huu imeuzwa kwa shilingi 1500/= cash. japo baadae bei ilipungua kutokana na quality kupungua katika miezi ya mwisho mwa msimu wa mvua.hapo utasema serikali haiwajali wakulima? Big up Dada yetu Fatma. Nanyumbu oyeeeeeee!
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145

  MM,

  Sikio la kufa halisikii dawa. Hawa wabunge wa CCM wameamua kufunga masikio na kuangalia maslahi yao binafsi. Ukiwauliza uhalali wa hizo posho unaweza kuvunjika mbavu kuna anatokea kisiwa cha kule kusini nilimuuliza je wavua samaki nao mnawakatia kidogo hizo posho akanijibu lazima ati!!! nikasema kweli wameenda kutetea maslahi yao binafsi. Hao ndio watunga sheria wetu.

  Isipokuwa usiwe na wasiwasi mkuu waangalie tu Ugiriki wanavyoteseka hadi wale wabunge waliokuwa wakitetea posho bungeni sasa hivi wanapiga kura wapunguziwe mishahara yao. Kufilisika sio mchezo!!!!! Tanzania muda ukiwadia utajionea mwenyewe.
   
Loading...