Wakulima wagomea bei ya Korosho

Wakulima wagomea bei ya Korosho

Mshtuko umewakuta wakulima baada ya Kuletewa bei ya Tsh 1680 kabla ya makato ambapo baada ya makato huenda mkulima ikamfikia 1380, Zoezi hilo la mauzo ya Korosho liliendeshwa wilayani Tandahimba katika kijiji cha Mitondi.

Wakulima wamegomea bei hiyo hivyo korosho hazijauzwa leo.
Mungu wabariki wakulima
 
Gharama gani kama pembejeo zilitolewa bure..mbole nako kuna ruzuku.?

Mkulima hana hasara..wenye hasara na wanao kataaga bei wengi ni wafanyabishara sio wakulima.

#MaendeleoHayanaChama
Unalitia Taifa hasara maana hamna kitu kabisa...unampa mtu chupa kimoja Cha dawa ili umuibie kirahisi ...kupitia Bei uchwara....nimepuliza Mara 7 ..hicho kichupa chenu sikuchukua ....
 
hovyo kabisa... nimekuuliza ulishawahi uza hiyo bei au ulimuona nani kalipwa bei hiyo
Ungekuwa uko Mtwara au Lindi usingebisha.
Korosho ilipanda bei 2016 ikawa inauzwa 3000+ na 2017 ifika 4000 kwa kilo. Wakulima walilipwa 3000+ kwa kilo miaka hiyo.

2018 hali iliyumba, tangia hapo kila mtu anajua pumzi ya moto wanayovuta wakulima.
 
Mshtuko umewakuta wakulima baada ya Kuletewa bei ya Tsh 1680 kabla ya makato ambapo baada ya makato huenda mkulima ikamfikia 1380, Zoezi hilo la mauzo ya Korosho liliendeshwa wilayani Tandahimba katika kijiji cha Mitondi.

Wakulima wamegomea bei hiyo hivyo korosho hazijauzwa leo.

Waachane nao wawatafute wavietnam watanunua kwa bei nzuri tu, yaani huku mtaani processed korosho robo karibia Tsh 8000(Zile packed).
 
US$ 14.78 kwa gramu 850gms ya korosho katika supermarket za America ya Kaskazini. Sawa na shilingi 33,994 za Tanzania (US $1 = Tshs 2,330) kwa gramu 850. Kilo moja ni gramu 1,000. Mkulima anauza korosho ghafi gramu 1,000 kwa shilingi?

1666384869323.png

Tujiulize kwanini korosho iliyosindikwa na unauzwa ktk supermarkets na maduka ya walaji bei huwa haishuki ipo palepale lakini bei ya korosho ghafi huwa inaporomoka na kupanda.

Nini kifanyike ili Bodi ya Korosho Tanzania iweze kuhakikisha wakulima bei wanayoipata 'haiporomoki' kama ilivyo kwa walaji wa korosho zilizosindikwa na kutiwa ktk vifungashio bei huwa juu kila siku ktk soko la ndani na nje ya Tanzania.
 
Gharama za usafirishaji kwa container moja ni ghali sana EAC ukilinganisha na nchi za Asia

EAC TRANSPORT & LOGISTIC COST HIGH AT 1.8 USD PER KM PER CONTAINER

Miongoni mwa masoko muhimu la kimataifa kwa wajasiriamali ni Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) ambalo ni makubaliano ya biashara huru ya Afrika kati ya nchi 54 wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

Kutokana na hali hiyo, nchi za EAC zinaagiza zaidi bidhaa mbalimbali kutoka nje na kulazimika kusafirisha malighafi kama mazao ya kilimo ili yakachakatwe nje na kurejeshwa tena katika nchi zao.

Pamoja na hayo amesema kuna umuhimu wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara na wajasiriamali wakubwa kwa wadogo katika michakato yao yote ya utengenezaji bidhaa kuhakikisha suala la viwango vya ubora haliachwi nyuma. Njia nyingine itakayosaidia wazalishaji wa bidhaa kushindana na wenzao wa Afrika na kimataifa ni kuwaondolea vikwazo mbalimbali ikiwemo kodi na masharti magumu ya kusafirisha bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Frank Dafa, Meneja Sera za Viwango wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) amesema katika jumuiya hiyo wanaendelea kuondoa vikwazo vinavyowarudisha nyuma wafanyabiashara na kuwafungulia fursa za kufaidika na masoko ya bidhaa ya kimataifa.

“Afrika Mashariki tumekuwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa kuweka mifumo ya kuoanisha sheria zetu za bidhaa ili kuhakikisha haziwi kikwazo kwenye biashara,” amesema Dafa
OSBP-Malaba.jpg

  • EABC Calls for the formulation of EAC transport and logistic charter/framework to boost the competitiveness of the region
SOMA ZAIDI :
Source : EAC TRANSPORT & LOGISTIC COST HIGH AT 1.8 USD PER KM PER CONTAINER
 
Hakuna mwananchi aliyepata faida kwenye ule uharamia, wengi hawakulipwa, na zile korosho zilizotaifishwa zilitupwa baharini
Shida ilikuwa Ucheleweshwaji wa malipo tu, ila kila aliyestahili kulipwa ALILIPWA. Tena wale waliokuwa na mzigo mkubwa walilipwa karibia kabisa na Msimu wa 2019.

Serikali ilinunua sh 3000 kwa kilo, pasipo kuwekwa tozo yoyote.

Unachokiita uharamia, Leo Tandahimba wanaombea kingejirudia kuliko huu Unyang'anyi unaotaka kufanyika.

Wakati gharama za pembejeo zinapanda, kila bidhaa inapanda, korosho inapotezaje thamani yake?

Mnapaswa Kujifunza Bepari hanaga huruma, Ukiishi naye kinyonge ndivyo unavyoongeza kina cha makucha yake. Pumbavu!
 
US$ 14.78 kwa gramu 850gms ya korosho katika supermarket za America ya Kaskazini . Sawa na shilingi 33,994 za Tanzania (US $1 = Tshs 2,330) kwa gramu 850. Kilo moja ni gramu 1,000. Mkulima anauza korosho ghafi gramu 1,000 kwa shilingi ?

View attachment 2394175

Tujiulize kwanini korosho iliyosindikwa na unauzwa ktk supermarkets na maduka ya walaji bei huwa haishuki ipo palepale lakini bei ya korosho ghafi huwa inaporomoka na kupanda.

Nini kifanyike ili Bodi ya Korosho Tanzania iweze kuhakikisha wakulima bei wanayoipata 'haiporomoki' kama ilivyo kwa walaji wa korosho zilizo sindikwa na kutiwa ktk vifungashio bei huwa juu kila siku ktk soko la ndani na nje ya Tanzania.

12 Juni 20201

Why Cashew Nuts Are So Expensive | So Expensive

One kilogram of cashews can cost $10 wholesale — over seven times as much as peanuts. And in the US, retail prices for raw whole cashews can reach $15 per pound. But cashews are more complex than most other nuts. Each cashew kernel grows inside a toxic shell. It must be carefully extracted from this shell and rigorously processed to ensure that the caustic liquid inside the shell is completely destroyed. So, how are cashews processed? And is this what makes them so expensive? The processing of cashews is becoming widely automated, though it is still done by hand in many factories in Sri Lanka.
Source : Business Insider
 
US$ 14.78 kwa gramu 850gms ya korosho katika supermarket za America ya Kaskazini . Sawa na shilingi 33,994 za Tanzania (US $1 = Tshs 2,330) kwa gramu 850. Kilo moja ni gramu 1,000. Mkulima anauza korosho ghafi gramu 1,000 kwa shilingi ?

View attachment 2394175

Tujiulize kwanini korosho iliyosindikwa na unauzwa ktk supermarkets na maduka ya walaji bei huwa haishuki ipo palepale lakini bei ya korosho ghafi huwa inaporomoka na kupanda.

Nini kifanyike ili Bodi ya Korosho Tanzania iweze kuhakikisha wakulima bei wanayoipata 'haiporomoki' kama ilivyo kwa walaji wa korosho zilizo sindikwa na kutiwa ktk vifungashio bei huwa juu kila siku ktk soko la ndani na nje ya Tanzania.
Mmamo miaka ya 70 Mwalimu Nyerere alijenga viwanda vikubwa vingi vya kubangulia korosho mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Ruvuma ili kuongeza thamani ya zao, hivyo viwanda kwa sasa vimeyeyuka. Wawekezaji wa hapa nchini wako busy kujenga stadium ya Namungo wakati mazao yao korosho ghafi yamerundikana ghalani hayana soko.a.Kupanga ni kuchagua.
 
Shida ilikuwa Ucheleweshwaji wa malipo tu, ila kila aliyestahili kulipwa ALILIPWA. Tena wale waliokuwa na mzigo mkubwa walilipwa karibia kabisa na Msimu wa 2019.

Serikali ilinunua sh 3000 kwa kilo, pasipo kuwekwa tozo yoyote.

Unachokiita uharamia, Leo Tandahimba wanaombea kingejirudia kuliko huu Unyang'anyi unaotaka kufanyika.

Wakati gharama za pembejeo zinapanda, kila bidhaa inapanda, korosho inapotezaje thamani yake?

Mnapaswa Kujifunza Bepari hanaga huruma, Ukiishi naye kinyonge ndivyo unavyoongeza kina cha makucha yake. Pumbavu!
Wewe hujielewi, huelewi uchumi

Korosho ni luxury good, sio sawa na mahindi au mchele, kukiwa na mtikisiko wa kiuchumi watu hawanunui luxury goods bali wanahifadhi fedha zao kununua basic goods
Ni kama kipindi cha mitikisiko wa uchumi baa zinakosa wateja sababu bia ni luxury good

Wakulima wachache sana walilipwa bei ya 3000, wengi waliporwa korosho zao wengine wakalipwa 2600
Sisi tulikuwa ground tunajua haya mambo
 
US$ 14.78 kwa gramu 850gms ya korosho katika supermarket za America ya Kaskazini . Sawa na shilingi 33,994 za Tanzania (US $1 = Tshs 2,330) kwa gramu 850. Kilo moja ni gramu 1,000. Mkulima anauza korosho ghafi gramu 1,000 kwa shilingi ?

View attachment 2394175

Tujiulize kwanini korosho iliyosindikwa na unauzwa ktk supermarkets na maduka ya walaji bei huwa haishuki ipo palepale lakini bei ya korosho ghafi huwa inaporomoka na kupanda.

Nini kifanyike ili Bodi ya Korosho Tanzania iweze kuhakikisha wakulima bei wanayoipata 'haiporomoki' kama ilivyo kwa walaji wa korosho zilizo sindikwa na kutiwa ktk vifungashio bei huwa juu kila siku ktk soko la ndani na nje ya Tanzania.

One kilogram of cashews can cost $10 wholesale — over seven times as much as peanuts. And in the US, retail prices for raw whole cashews can reach $15 per pound. But cashews are more complex than most other nuts. Each cashew kernel grows inside a toxic shell. It must be carefully extracted from this shell and rigorously processed to ensure that the caustic liquid inside the shell is completely destroyed. So, how are cashews processed? And is this what makes them so expensive? The processing of cashews is becoming widely automated, though it is still done by hand in many factories in Sri Lanka.
Mmamo miaka ya 70 Mwalimu Nyerere alijenga viwanda vikubwa vingi vya kubangulia korosho mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Ruvuma ili kuongeza thamani ya zao, hivyo viwanda kwa sasa vimeyeyuka. Wawekezaji wa hapa nchini wako busy kujenga stadium ya Namungo wakati mazao yao korosho ghafi yamerundikana ghalani hayana soko.a.Kupanga ni kuchagua.

Naona ndiyo maana Vietnam, Sri Lanka, India wameamua siku nyingi korosho zinazozalishwa nchini mwao wanazisindika ili kuongeza thamani na kuuza korosho zilizo tayari kuliwa.

Pia nchi hizo tatu ndiyo wanunuzi wakubwa wa korosho ghafi toka nchi za kiAfrika halafu wanazisindika na kuuza kimataifa tayari kuliwa huku wakinufaika na bei kubwa ya korosho iliyosindikwa.

Hili suala la korosho halina tofauti na madini ya Tanzanite yanayopatikana nchi Tanzania pekee, kama ilivyo kwa korosho Tanzania inauza madini hayo yakiwa hayajachongwa kwenda India, Thailand, Belgium n.k ambapo wanayachonga na kuyaongeza thamani maradufu tayari kuuzwa ktk soko la dunia.

Lini tena tutarejea kuwa tayari kusindika mazao na kuchonga / gharisha madini ili viwanda vidogo vingi vyenye watu waTanzania wenye ujuzi ili kutengeneza bidhaa zilizo ongezwa thamani kubwa tayari kuliwa ktk soko la dunia badala ya kuuza malighafi na kuzipelekea nchi zingine ajira nyingi ili waongeze thamani pia ajira kwa wingi huko ngambo.

Nchi hii inahitaji visheni / vision kubwa vyuo vya VETA, faculty za vyuo vikuu sehemu ya uhandisi mitambo n.k kutoa mafunzo wanachuo kuweza ku design, kuendesha na kukarafati mitambo ya kubangua korosho, kuchonga tanzanite, almasi n.k ili kwa kuanzia sekta ya mazao zipate uwezo wa kusindika mazao yao ili kuongeza thamani pia madini yachongwe tayari kuuzwa kwa bei kubwa kama vito vilivyokamilika.

19 - 22 October 2022 Kongamano la 7 la WaHandisi wa Mitambo lafanyika chuo kikuu cha UDSM

Mh. Omani Kipanga naibu waziri wa elimu aelezea azma ya serikali kutengeneza muunganiko baina ya yale wahandisi wa mitambo (mechanical engineering) wanayofundishwa vyuoni na hali halisi iliyopo nje ya vyuo vikuu ili wahandisi hao wakaweze kuleta mabadiliko katika jamii mfano kuunda mitambo, kuifanyia service n.k
Source: mlimani tv
 
Wewe hujielewi, huelewi uchumi

Korosho ni luxury good, sio sawa na mahindi au mchele, kukiwa na mtikisiko wa kiuchumi watu hawanunui luxury goods bali wanahifadhi fedha zao kununua basic goods
Ni kama kipindi cha mitikisiko wa uchumi baa zinakosa wateja sababu bia ni luxury good

Wakulima wachache sana walilipwa bei ya 3000, wengi waliporwa korosho zao wengine wakalipwa 2600
Sisi tulikuwa ground tunajua haya mambo
Safi kabisa Mwanauchumi mbobezi.... Haya ungekuja huku Nanyamba au Nanyanga au Mahuta utuhubirie tukuelewe.

Tunachojua wauzao nchi yetu ni ninyi mjionao kuwa wasomi.

Hope unajua vema sasa kwamba ground haukuwa peke yako, na ni sisi kwenye vijiwe vyetu vya kahawa na bao tukumbukao enzi zile.

Kila la heri katika Kulambishwa kwako Asali, tuliao tunatosha hatuhitaji msaada wenu.
 
Korosho ndio inaenda kudidimia..nchi ya walamba asali hii sasahivi wamejipanga kumnyonya mkulima..ukute bei ni kubwa tu huko kwenye masoko ya nje.

Ila wao wanawapanga wafanyabiashara kisha wanaenda kuuza kwa faida kubwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom