Sijui haya maelezo yako unayatoa kama sarcasm au unamaanisha kweli
Magufuli alisema waziri mkuu atafute wanunuzi watakaonunua kwa bei isiyopungua 3000, waziri mkuu akapata makampuni kadhaa ambayo yangetoa bei hiyo ya juu ya 3000 kidogo, yakatoa bei zao kama vile 3080, 3,100 n.k
Magufuli akakataa akasema bei hizo ni za chini mno akafoka vibaya, akasema serikali ndio utanunua hizo korosho na jeshi ndio litabangua hata kwa mabomu, mwisho wa siku naye akaja kutoa ofa ya 3000 kwa wakulima na zaidi ya nusu ya watu hawakulipwa sababu waliambiwa ni walanguzi (kangomba) na hata hao waliolipwa ni wachache sana walilipwa kwa bei ya 3000, wengi walilipwa kwa bei ya 2600
Mwisho wa siku jeshi halikuweza kubangua zile korosho kwa mabomu na zilikosa wanunuzi na tetesi ni kuwa zilitupwa baharini