One kilogram of cashews can cost $10 wholesale — over seven times as much as peanuts. And in the US, retail prices for raw whole cashews can reach $15 per pound. But cashews are more complex than most other nuts. Each cashew kernel grows inside a toxic shell. It must be carefully extracted from this shell and rigorously processed to ensure that the caustic liquid inside the shell is completely destroyed. So, how are cashews processed? And is this what makes them so expensive? The processing of cashews is becoming widely automated, though it is still done by hand in many factories in Sri Lanka.
Naona ndiyo maana Vietnam, Sri Lanka, India wameamua siku nyingi korosho zinazozalishwa nchini mwao wanazisindika ili kuongeza thamani na kuuza korosho zilizo tayari kuliwa.
Pia nchi hizo tatu ndiyo wanunuzi wakubwa wa korosho ghafi toka nchi za kiAfrika halafu wanazisindika na kuuza kimataifa tayari kuliwa huku wakinufaika na bei kubwa ya korosho iliyosindikwa.
Hili suala la korosho halina tofauti na madini ya Tanzanite yanayopatikana nchi Tanzania pekee, kama ilivyo kwa korosho Tanzania inauza madini hayo yakiwa hayajachongwa kwenda India, Thailand, Belgium n.k ambapo wanayachonga na kuyaongeza thamani maradufu tayari kuuzwa ktk soko la dunia.
Lini tena tutarejea kuwa tayari kusindika mazao na kuchonga / gharisha madini ili viwanda vidogo vingi vyenye watu waTanzania wenye ujuzi ili kutengeneza bidhaa zilizo ongezwa thamani kubwa tayari kuliwa ktk soko la dunia badala ya kuuza malighafi na kuzipelekea nchi zingine ajira nyingi ili waongeze thamani pia ajira kwa wingi huko ngambo.
Nchi hii inahitaji visheni / vision kubwa vyuo vya VETA, faculty za vyuo vikuu sehemu ya uhandisi mitambo n.k kutoa mafunzo wanachuo kuweza ku design, kuendesha na kukarafati mitambo ya kubangua korosho, kuchonga tanzanite, almasi n.k ili kwa kuanzia sekta ya mazao zipate uwezo wa kusindika mazao yao ili kuongeza thamani pia madini yachongwe tayari kuuzwa kwa bei kubwa kama vito vilivyokamilika.
19 - 22 October 2022 Kongamano la 7 la WaHandisi wa Mitambo lafanyika chuo kikuu cha UDSM
Mh. Omani Kipanga naibu waziri wa elimu aelezea azma ya serikali kutengeneza muunganiko baina ya yale wahandisi wa mitambo (mechanical engineering) wanayofundishwa vyuoni na hali halisi iliyopo nje ya vyuo vikuu ili wahandisi hao wakaweze kuleta mabadiliko katika jamii mfano kuunda mitambo, kuifanyia service n.k
Source: mlimani tv