Wakulima wagomea bei ya Korosho

Wakulima wagomea bei ya Korosho

Mshtuko umewakuta wakulima baada ya Kuletewa bei ya Tsh 1680 kabla ya makato ambapo baada ya makato huenda mkulima ikamfikia 1380, Zoezi hilo la mauzo ya Korosho liliendeshwa wilayani Tandahimba katika kijiji cha Mitondi.

Wakulima wamegomea bei hiyo hivyo korosho hazijauzwa leo.
Ni hivi na bado, Magufuli kasemwa sana kwamba aliharibu biashara ya korosho, ngoja tuone nani zaidi
 
Soko la dunia, demand ikiwa kubwa bei inakuwa kubwa
Magufuli had nothing to do with it
Kumbukumbu zako hazikuoneshi kwamba Magufuli alikataa bei ya shilinngi 2,800 akasema Serikali litanunua kwa bei ya shilingi 3,000 na kwamba soko litakuwa hapa nchini kwa kila mtanzania kununua kilo mbili za korosho?

Mbona tunakuwa wasahaulifu kirahisi hivi? Unasemaje Magufuli hausiki wakati alimpiga kejeli mpaka aliyekuwa Waziri Mkuu wake kuwa kama Kusini wangeandamana angepiga shangazi zao!!?

Wale wanajeshi waliokwenda kusomba zile Korosho umeshasahau ni nani aliyewaamrisha waende kuzisomba??
 
Utasikia mtu flani anasema "mwacheni mkulima auze mazao yake kwa bei anayotaka'! Kwa uhalisia mkulima hana maamuzi na bei zote za mazao yawe ya chakula au biashara, mara zote wanaoamua bei huwa ni wafanya biashara
Mfanyabiashara nae hawezi kuamua bei, soko ndio linaloamua, kukiwa na uhitaji mkubwa wa bidhaa na hiyo bidhaa ikawa haipatikani kwa wingi basi bei yake itakuwa kubwa

Vivyo hivyo, bidhaa ikiwa haihitajiki sana na upatikanaji wake sio mgumu basi itauzwa bei ya kutupwa
Hii sio economics hii ni common sense
 
Kumbukumbu zako hazikuoneshi kwamba Magufuli alikataa bei ya shilinngi 2,800 akasema Serikali litanunua kwa bei ya shilingi 3,000 na kwamba soko litakuwa hapa nchini kwa kila mtanzania kununua kilo mbili za korosho?

Mbona tunakuwa wasahaulifu kirahisi hivi? Unasemaje Magufuli hausiki wakati alimpiga kejeli mpaka aliyekuwa Waziri Mkuu wake kuwa kama Kusini wangeandamana angepiga shangazi zao!!?

Wale wanajeshi waliokwenda kusomba zile Korosho umeshasahau ni nani aliyewaamrisha waende kuzisomba??
Sijui haya maelezo yako unayatoa kama sarcasm au unamaanisha kweli

Magufuli alisema waziri mkuu atafute wanunuzi watakaonunua kwa bei isiyopungua 3000, waziri mkuu akapata makampuni kadhaa ambayo yangetoa bei hiyo ya juu ya 3000 kidogo, yakatoa bei zao kama vile 3080, 3,100 n.k

Magufuli akakataa akasema bei hizo ni za chini mno akafoka vibaya, akasema serikali ndio utanunua hizo korosho na jeshi ndio litabangua hata kwa mabomu, mwisho wa siku naye akaja kutoa ofa ya 3000 kwa wakulima na zaidi ya nusu ya watu hawakulipwa sababu waliambiwa ni walanguzi (kangomba) na hata hao waliolipwa ni wachache sana walilipwa kwa bei ya 3000, wengi walilipwa kwa bei ya 2600

Mwisho wa siku jeshi halikuweza kubangua zile korosho kwa mabomu na zilikosa wanunuzi na tetesi ni kuwa zilitupwa baharini
 
Mfanyabiashara nae hawezi kuamua bei , soko ndio linaloamua, kukiwa na uhitaji mkubwa wa bidhaa na hiyo bidhaa ikawa haipatikani kwa wingi basi bei yake itakuwa kubwa

Vivyo hivyo, bidhaa ikiwa haihitajiki sana na upatikanaji wake sio mgumu basi itauzwa bei ya kutupwa
Hii sio economics hii ni common sense
Unafikiri huyo soko ni nani? Kwani hujawahi kusikia wafanyabiashara wanaficha bidhaa au wanapunguza uzalishaji ili bei zipande? Hiyo economics uliyandika wenzako tumeisoma kama topic kwenye somo la siasa.
 
Mwisho wa siku jeshi halikuweza kubangua zile korosho kwa mabomu na zilikosa wanunuzi na tetesi ni kuwa zilitupwa baharini
Serikali makini iko radhi kuhamisha hasara kutoka kwa raia wake flani kuipeleka serikalini. Tendo kama hilo likifanyika kwa uwazi linaitwa ruzuku, yaani serikali imebeba hasara ili wananchi wapate unafuu
 
Unafikiri huyo soko ni nani? Kwani hujawahi kusikia wafanyabiashara wanaficha bidhaa au wanapunguza uzalishaji ili bei zipande? Hiyo economics uliyandika wenzako tumeisoma kama topic kwenye somo la siasa.
Wafanyabishara ndio wanaolima? Wakulima si ndio wazalishaji?

Sasa hiyo ya kuficha bidhaa wanaficha kwa sababu wanajua bidhaa ni adimu, na wanajua itapanda bei kutokana na uadimu wake.

Bidhaa ikiwa inapatikana kuificha utakuwa unajitafutia hasara tu

Mfano sasa hivi ufiche sukari wakati ipo ya kutosha si utaingia hasara?
 
Serikali makini iko radhi kuhamisha hasara kutoka kwa raia wake flani kuipeleka serikalini. Tendo kama hilo likifanyika kwa uwazi linaitwa ruzuku, yaani serikali imebeba hasara ili wananchi wapate unafuu
Hakuna mwananchi aliyepata faida kwenye ule uharamia, wengi hawakulipwa, na zile korosho zilizotaifishwa zilitupwa baharini
 
Kataaa CCM ni adui wa taifa, tuwe na serikali za majimbo yaani korosho zako halafu mjinga kutoka Pemba apange bei.
 
Huna akili dogo hivi unajua gharama za kuhudumia shamba ...!! Hiyo Bei ni ya hasara mpk kwa mkulima.
Gharama gani kama pembejeo zilitolewa bure..mbole nako kuna ruzuku.?

Mkulima hana hasara..wenye hasara na wanao kataaga bei wengi ni wafanyabishara sio wakulima.

#MaendeleoHayanaChama
 
Fuatilia takwimu. Ilizidi. Kuna wakati ilifika 4200 na haikuwa kushuka chini ya 3000 hadi anakufa.

Hiyo bei iliyoletwa sasa ni bei za zamani kabla Magu hajawa rais. Naomba ufuatilie records.
Mbona mkulima wa mahindi naye anauza gunia 70,000 wakati kipindi cha Magufuli aliuza hadi 10,000

Bei za mazao zinaamuliwa na soko sio Rais, acheni uzezeta
 
Tunaposemaga Magufuli ndio aliipandisha korosho thamani kwa kuondoa urasimu uliokuwepo watu huwa hawaelewi. Sasa angalia bei ya 2015 wakati JK anamaliza na baada ya JPM kuingia.

Kinachofuatia kwa sasa ni bei za JK kurudi. Yaani chini ya tzs 2000.View attachment 2393894View attachment 2393895
Screenshot_20221021-190717_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom