Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Wakulima wa zao la tumbaku kutoka Chama Cha Msingi Cha Ushirika Cha Wakulima wa Tumbaku Mpanda Kati, Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamelalamika kutolipwa fedha zao hadi hivi sasa licha ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kutoa maagizo kwamba kabla ya siku kuu ya Nanenane Wakulima wote wanatakiwa kulipwa.
Leo Jumatatu August 11, 2025, Baadhi ya Wakulima hao wakiwa katika Ofisi ya Chama Cha Msingi hicho mbali na kulalamikia kutolipwa fedha zao na kuwa chama pekee mkoani Katavi ambacho Wakulima wake hawajalipwa pia wamelalamikia nyongeza ya makato ya fedha ya asilimia 3 kinyume na utaratibu wa vikao.
Meneja wa Chama cha Msingi hicho baada ya kutafutwa alisema yuko benki kwa ajili ya kushughulikia matatizo hayo ya wakulima.
Kusoma ufafanuzi zaidi, bofya hapa ~ Zaituni Tembo: Kweli hatujawalipa Wakulima wa Tumbaku, kwa sasa hivi tuna Bima ya Mkopo kutoka Benki ya NMB
Pia soma ~ DC Tanganyika aagiza Wakulima wa Tumbaku walipwe haraka iwezekanavyo fedha zao