Mkulima na Mfugaji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,013
- 1,634
Salam wakulima na wafugaji,
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, michungwa ni Miongoni mwa mazao yanayowapa kipato wakulima.
Usishangae mtu mwenye ekari moja ya michungwa aina ya Valencia kutengeneza zaidi ya milioni 6 kama msimu utakua mzuri.
Kwani kuna kipindi chungwa moja linauzwa mpaka Tsh 100 bei ya shambani na ekari moja kama shamba limezaa vizuri unaweza kutoa machungwa zaidi ya 60000.
Cha ajabu serikali ipo kimya na wala haitoi kipaumbele kama kwenye mazao mengine kama korosho, chai nk.
Ni kawaida kupita mashambani hasa kipindi hiki kukuta machungwa yameanguka na kuoza na mkulima hana cha kufanya.
Kwa kifupi mkulima wa machungwa anajipigania mwenyewe.
Kama serikali ingetia angalau nusu ya nguvu inayotoa kwenye kilimo cha korosho, chai, mkonge nk basi wakulima wa machungwa wangeishi kifalme kuliko wakulima wa mazao yote Tanzania