SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,136
- 7,904
Kelele na malalamiko yamekuwa mengi kwenye klabu ya Simba. Kuanzia kwenye masuala ya usajili wa wachezaji, matokeo uwanjani, malalamiko ya kuonewa ndani na nje ya uwanja, hadi utendaji wa kila siku wa klabu kote huko malalamiko yamekuwa mengi mno.
Kwa muda sasa Simba imekuwa inahangaika huku na huko kutafuta viwanja vya kuchezea mechi zake na msimu huu pekee imebadili uwanja wake wa nyumbani si chini ya mara 4. Niliwahi kusema mara nyingi Simba imepoteza ushawishi ndani na nje ya uwanja na lawama zote zinaangukia kwa uongozi. Niliwahi kusema Simba inavyojipambanua kwa ukubwa wake, inatakiwa iweze kushinikiza kutumia uwanja wa Mkapa angalau kwa mechi chache za ligi, kuna watu wakanijibu wakifanya hivyo na timu nyingie itabidi zipewe ruhusa. Leo nimesikia mechi ya Azam vs Yanga imehamishiwa uwanja wa Mkapa wakati tuliambiwa uwanja umefungwa kwa mechi za ndani hadi October 2024 isipokuwa derby ya Simba vs Yanga pekee. Inakuwaje hili limewezekana? Ushawishi!
Sasa hivi kumekuwa na kelele kuhusu ufadhili na ushawishi wa GSM kwa timu 6 za ligi lakini, jambo ambalo kuna wanaona linaweza kuashiria uwezekano wa upangaji wa matokeo kuisaidia Yanga. Haijalishi kama hilo jambo linaruhusiwa kisheria au ni kinyume cha sheria zilizopo, ila kama GSM wameweza kulifanya hilo ni kwamba wana ushawishi wa kutosha kwa mamlaka husika, hata kwa njia zisizo halali kuweza kulifanikisha. Ushawishi! Ushawishi! Kama mwenzio anafanya uhuni halafu na wewe una uwezo wa kufanya uhuni ila unajibalaguza, lazima itakula kwako tu.
Simba imejaribu kuiiga Yanga kwa kuweka ukaribu na wanasiasa mbalimbali. Kuna tukio kabisa lilifanyika la kufungua tawi la Simba Bungeni, klabu inaonekana kujipendekeza kwa hawa wanasiasa, hadi wakaweza kumualika Rais kwenye Simba Day. Haya yote yana faida gani kama mwisho wa siku klabu inaendelea kushuka viwango na kupoteza ushawishi nje ya uwanja? Inawezekana huu ukaribu kwa wanasiasa ndiyo unaivuruga timu maana inaonekana sasa kupata matokeo ya hovyo kimipango mipango tu.
Mimi nafikiri uongozi mzima kuanzia Management ya Imani Kajula, Bodi nzima chini ya Salim Abdallah na Mwenyekiti wa Klabu Murtaza Mangugu wote wanastahili kuachia ngazi ili watu wapya wenye maono na nguvu mpya waje kuokoa jahazi.

Naunga mkono hoja, twenzetu Rwanda ila tujiandae kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi.
Simba imekaa kinyonge sana wakati mwingine. Hivi pamoja na kujipendekeza kote kwa wanasiasa, viongozi wameshindwa kushawishi mamlaka husika ili Simba iendelee kutumia uwanja wa Mkapa hata kipindi cha marekebisho?