Mwigulu ni kirusi kwenye soka letu

vvvv

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
395
687
Huyu mheshimiwa alianza kujulikana kwenye soka pale Singida United ilipopanda daraja, wote na Mo Dewji walikuwa Singida United, Mo akiwa sponser huku Mwigulu akiwa mwenyekiti, wakashindwana ikabidi Mo aachane na Singida na Baada ya muda akaingia Simba. Mwigulu akaanza kuihujumu Singida kwa ajili ya ushabiki wake kwa Yanga na hivo kuwapa Feisal.

Baada ya muda Singida United ikashuka daraja kwa ukosefu wa hela baada ya Mo kujitoa, Singida United mambo yakawa magumu hadi kutupwa daraja za chini kabisa kwenye ligi.

Baada ya Mwigulu kuteuliwa tena Uwaziri akanunua timu daraja la kwanza DTB, wakanunuliwa wachezaji wa kimataifa na wa ndani wenye uwezo, DTB ilipoingia ligi kuu ikabadilishwa jina na kuitwa Singida Big Star.

Singida Big Stars ilinunua wachezaji wa nje na wale wazuri ligi kuu na kufanya vizuri hadi kufanikiwa kupata nafasi ya kushiriki kombe la shirikisho, kanuni za CAF zilipobadilika na kutaka timu shiriki ziwe na timu za wanawake basi Singida Big Stars wakaungana Fountain Gate na kubadilishwa jina kuitwa Singida Fountain Gate.

Baada ya mda Singida Big stars wakaanza kushindwana na Fountain Gate, mishahara ya wachezaji kucheleweshwa na baadhi ya wachezaji wa kimataifa kuachwa tu na Singida fountain gate ikakabiliwa na madeni makubwa kulipa wachezaji na kudhoofika na sasa kuburuza mkia kwenye ligi kuu.

Mwigulu baada ya kuona madeni akaikimbia Singida fountain gate na kwenda kuinunua Ihefu na uwanja wa nyumbani wa Ihefu ukawa Singida (Liti).

Huyu mheshimiwa ni kirusi cha kuvuruga vilabu, je baada ya Ihefu ataenda wapi?

TFF na wapenda soka tukemee huu ujanja ujanja kwenye soka na huyu mheshimiwa aangaliwe kwa jicho pevu.
 
Mwigulu ni wa hovyo sana, huu ujinga huwa anaufanya kwa manufaa ya vyura wala sio kukuza mpira wetu.

Akija Rais mwingine akambana, ataacha kuifadhili hiyo Ihefu, ni kiongozi corrupt sana anayebebwa na taasisi dhaifu ya urais.
 
Mwigulu hata akiamua kuifirisi Nchi, Kwa sababu ya Yanga atapigiwa makofi.Hii Nchi watu wake wanatembea akili zikiwa kwenye visigino vya miguu.
 
Mwigulu ni wa hovyo sana, huu ujinga huwa anaufanya kwa manufaa ya vyura wala sio kukuza mpira wetu.

Akija Rais mwingine akambana, ataacha kuifadhili hiyo Ihefu, ni kiongozi corrupt sana anayebebwa na taasisi dhaifu ya urais.
Toa sababu zako za msingi ni vipi Yanga inanufaika kwa Mwigulu kuwa na timu
 
Huyu mheshimiwa alianza kujulikana kwenye soka pale Singida United ilipopanda daraja, wote na Mo Dewji walikuwa Singida United, Mo akiwa sponser huku Mwigulu akiwa mwenyekiti, wakashindwana ikabidi Mo aachane na Singida na Baada ya muda akaingia Simba. Mwigulu akaanza kuihujumu Singida kwa ajili ya ushabiki wake kwa Yanga na hivo kuwapa Feisal.

Baada ya muda Singida United ikashuka daraja kwa ukosefu wa hela baada ya Mo kujitoa, Singida United mambo yakawa magumu hadi kutupwa daraja za chini kabisa kwenye ligi.

Baada ya Mwigulu kuteuliwa tena Uwaziri akanunua timu daraja la kwanza DTB, wakanunuliwa wachezaji wa kimataifa na wa ndani wenye uwezo, DTB ilipoingia ligi kuu ikabadilishwa jina na kuitwa Singida Big Star.

Singida Big Stars ilinunua wachezaji wa nje na wale wazuri ligi kuu na kufanya vizuri hadi kufanikiwa kupata nafasi ya kushiriki kombe la shirikisho, kanuni za CAF zilipobadilika na kutaka timu shiriki ziwe na timu za wanawake basi Singida Big Stars wakaungana Fountain Gate na kubadilishwa jina kuitwa Singida Fountain Gate.

Baada ya mda Singida Big stars wakaanza kushindwana na Fountain Gate, mishahara ya wachezaji kucheleweshwa na baadhi ya wachezaji wa kimataifa kuachwa tu na Singida fountain gate ikakabiliwa na madeni makubwa kulipa wachezaji na kudhoofika na sasa kuburuza mkia kwenye ligi kuu.

Mwigulu baada ya kuona madeni akaikimbia Singida fountain gate na kwenda kuinunua Ihefu na uwanja wa nyumbani wa Ihefu ukawa Singida (Liti).

Huyu mheshimiwa ni kirusi cha kuvuruga vilabu, je baada ya Ihefu ataenda wapi?

TFF na wapenda soka tukemee huu ujanja ujanja kwenye soka na huyu mheshimiwa aangaliwe kwa jicho pevu.
kuwa na mawazo na mtazamo wa eti mtu Fulani ni tatizo la soka mahali fulani ni upotoshaji 🐒

mambo ya socar yamebadilika, football imebadilika uwanjani hadi nje ya uwanja. Football imekua biashara kubwa na inayolipa sana Duniani 🐒

Imani potofu, ushirikina na uchawi, visicheleweshe mafanikio ya socar Tz, nadhani vibaki huko huko vijijini 🐒
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom