Wakulima debe la mpunga hutoa kilo ngapi za mchele?

Huo mpunga wa kwenu ni mwepesi sana mkuu juzi nimekoboa gunia la mpunga lenye debe 8 nimepata kilo 72 za mchele.
Itakua watu wa mbarali waliniibia mkuu😅😅 thou baada ya kuona comment za watu kwenye huu uzi nikafanya kauchunguzi kangu wanasema mwaka huu mpunga ulikua mwepesi kiasi.
 
Kuna factors nyingi zinazoamua idadi ya kilo/debe.

*Debe lenyewe (wengine hupimia ndoo 1 ya Lita 20 na wengine ndoo 2 za lita 10 ndiyo debe etc)

*Aina ya mbegu za mpunga.

Mpaka kilo 10/debe hufika
 
Itakua watu wa mbarali waliniibia mkuu😅😅 thou baada ya kuona comment za watu kwenye huu uzi nikafanya kauchunguzi kangu wanasema mwaka huu mpunga ulikua mwepesi kiasi.
Ni kweli mpunga mwaka huu ni mwepesi ila huwezu kukoboa gunia la debe 9 ukapata kilo chini ya 60 never huo sio mpunga labda. 🫵🤣 Yaani kwa debe 9 au 8 hapo mnakimbizana na 75+ Kg
 
Nadhani pia upimaji utakua kuna namna wanafanya hasa ukiwa si mwenyeji sana kwenye mambo hayo.
 
Wakulima debe la mpunga hutoa kilo ngapi za mchele?
Apa nilipo debe la mpunga ni 15,000 nataka kujua hutoa kilo ngapi ili nijue gharama ipo wapi, mchele dukani kilo ni 2,400-2,600
Kilo 20 za debe la mpunga hutoa kilo 10 za mchele uliokobolewa. Fomula ni kwamba kilo moja ya mpunga huwa ina nusu kilo ya pumba na nusu kilo ya mchele
 
Mbarali ni kwa madoni kule. Wana lima mpaka wana lima. Wale watu hapana kwa kweli. 🙌✊

Ila pamoja na kuwepo kwa wakulima wa kubwa kuna wakulima wa dogo pia. Kuhusu kupigwa ni kawaida hasa ukiwa unaanza katika masuala kama hayo.
Yeah Mbarali huwa hawategemei mvua wao so iwe mvua iwe jua msimu ukifika wanalima na wanavuna vizuri tu.

Ipi ni nzuri kwa mtu ambae labda anataka kuwa serious na business hii kati ya kuanza kwenye zero margin yaani kulima moja kwa moja au kuanzia katikati ya kwamba watu walime wewe ununue mpunga?
 
Mimi bado nipo balance kwasababu yote uliyo ya sema yana uzuri wake na ubaya wake. Mfano una weza ukaanza kulima moja kwa moja wewe mwenyewe na ukauza wewe.

Ila hii ita hitaji uwe na mtaji mkubwa sana kwa maana gharama za kilimo ni kubwa sana kama utaamua kufuata protocol zote pia ukiwa na shamba kubwa mfano ukiwa umeanza hata na acre 5 pia sio mzoefu ni ki mbembe hapo ila una weza kufanikiwa, pamoja na changamoto zote hasa shamba lako likiwa kwenye mkondo mzuri wa maji au ukiwa una water pump pia maji yawe karibu hapo uhakika wa kuvuna ni 90%

ii) una weza pia ukaanza kununua kwa wakulima mpunga au mchele na wewe unaenda kuuza kwenye masoko yako popote unapo jua wewe.(mchuuzi) ila hii ina weza kukuletea noma kama soko likiwa gumu mfano mwaka huu mpunga upo juu sana una weza kununua gunia la mchele lenye kg 100 Mbarali kwa T250k then uje uuze bei gani Dar?hapo kuna ushuru,usafiri, mifuko, makuli pia. Yaani ni ina ugumu wake mkuu. Japo kama una mtaji mkubwa hata wa gunia 300 una weza kupiga kazi kwa kukubali kupata faida hata ya 20k kwa kila gunia ila ili ku return hela yako ita tegemea na mzunguko wa biashara yako kama ina enda kasi au la!? Ni hayo tu kwa leo (Thecoder)
 
Aisee hii biashara inatakiwa uwe na mahesabu makali sana lakini pia uwe na soko la uhakika bila hivyo inaweza ikawa habari nyingine.

Huwa najiuliza huwa mnapataje faida kwenye hii biashara aisee😅😅
 
Kuna sehemu nimeuliza jana uko mashambani wanasema debe 7 ni laki na kumi na kama ukisema ukoboe bei ya mbeya town debe au 20kg ni shilling 48 - 50 elfu na gunia la mpuga zuri utapata debe 3.5 ninavoelewa mimi
 
Gunia la mpunga lililoshiba Lina kg 90 na 30 ni Pumba na 60 ni mchele. Sasa gunia Lina debe 6 hivyo kila debe linakupa kg 10 za mchele.
Mkuu gunia halishibi kwa debe 6,
Gunia likiwa limeshiba ni debe 7-8.
 
Half for half
yaani nusu kwa nusu
yaani debe likiwa na mpunga kilo 20 utapata mchele kilo 10.
 
Maoni mengi yamekuwa ya uongo sijajua waliojibu wengi hawaujui mpunga au vipi..

Debe 1 la mpunga ukiliweka kwenye mzani linatoa kilo 15 ukikoboa mchele ukatoka vizuri (usikatike) lazima litoe kilo 10 za mchele,ukikatika linataa 8 kushuka chini...

Vilevile ukiachana na mchele kutoka vizuri pia aina ya mbegu inaweza fanya mchele utoke na kilo nyingi au chache,mfano morogoro kuna mbegu inaitwa MBAWA MBILI au jina lingine KIKOTI ni mbegu yenye mchele super ila haina uzito hivyo debe unaweza ishia 9kg halafu kuna mbegu 2 zinaitwa KALIMATA na MZAMBIA hizo ni mbegu zenye mpunga mzito kama ukitoka vizuri basi hapo lazima ipige kilo10

Cha kuongeza mpunga mzito na mwepesi unaweza utofautisha hata ukiuweka kwenye mkono na ili mpunga ukupe uzito wake wa mwisho inategemea na huduma na maji shambani wakati wa mpunga unakaribia kuchanua...
 
Ni kweli mpunga mwaka huu ni mwepesi ila huwezu kukoboa gunia la debe 9 ukapata kilo chini ya 60 never huo sio mpunga labda. 🫵🤣 Yaani kwa debe 9 au 8 hapo mnakimbizana na 75+ Kg
Kwa bede 9 alitakiwa atoe kilo 72+ bonde la usangu wanalima saro 5 hiyo mbegu ikikutana na ukosefu wa maji wakati wa kuchanua inatoa kilo 8 tu kwa bede na mwaka huu mbarali imekumbwa na hiyo changamoto ya ukame
 
Back
Top Bottom