maria pia
JF-Expert Member
- Jul 24, 2012
- 516
- 118
wewe ni mzaramo?
Same qn?
wewe ni mzaramo?
sawa lakini msilete na wajomba zenu,shangazi,kaka,dada wabaki huko huko Simiyu,Mpwapwa na kwingineko.Mkibaki huko mie niko serikalini nawaahidi tutakuja kuwajengea hospitali,madarasa na hata maduka pia ila muonyeshe uzalendo na miji yenu kwanza kabla ya utaifa unaanza ukanda kwanza.Mvua zimesimama siku mbili tu wote mnakimbia kuja Dar yaani hamna ubunifu mwingine zaidi ya kilimo?mmesikia Dar kuna kilimo?mtalima kwenye paa za maghorofa?mtamwagilia na maji ya vyoo?au ubunifu wenyewe ndo huu wa kudandia malori huku umevaa viatu vya matairi(skiing) hadi dar?na hii biashara ya bodaboda,kuuza maji na juice,mitumba na kupiga debe zote tunajadili tuzipige marufuku hapa manake ndio gia yenu ya kuhalalisha kuja huku kumbe usiku mnatukaba!waangalie wanavyotoka povu humu!nimepiga ikulu eeh?na mtarudi tu!subirini vikao vyetu viishe.
nalijua jiji hili kitambo sana mkuu hata kabla sijazishika pesa hadi sasa nazishika.Hata mie nilidhani kuwa na pesa Dar mji ntauona mzuri lakini nimegundua pesa sio kila kitu kwenye maisha.Labda wewe ndugu yangu mwenye pesa za mawazo na limited knowledge and education ndio unafikiri siku ukizipata mambo yote yatakwenda sawa na hata maji na umeme vitashuka kwako vyenyewe toka mbinguni! ila kwetu sie wengine tuliopata bahati ya kusoma na kwenda huko na huko duniani,we know that money isn't everything in life,BRAIN IS!
Sasa yakifanyika hayo huoni kuwa hao wakuja ndiyo watakaobaki mjini peke yao?kwa sababu wao ndiyo wenye uwezo wa kugharimia yote hayo kutokana na wengi wao kuwa na uchumi mzuri kidogo tofauti na wazaramo?hapa tu tayari maisha ni mzigo kwenu nyie mnaojiita wa hapahapa,je gharama ikiongezeka?si ndiyo kabisa mtawaachia kina Mangi hadi wake zenu?na hao wakuja ndiyo wanayoistawisha Dar kwa taarifa yako!na siku serikali ikiwa fair kwenye mgawanyo wa rasilimali dar itabaki uchi.Ni kweli usemayo ndugu.mji umejaa sana.ukienda kkoo ni vurugu hamna pa kukanyaga.bugurun ndo acha kabsa ni watu ambao wanazurura tu.yote tisa kumi nenda mbagala ndo utajua kuwa mji umevamiwa yaan kuna watu balaa ni kwa sababu kule maisha ni cheap chumba buku 3 japo hakina dirisha wala mlango yan pagale.ila unaposema mji una kero kwa kujaa watu si kila eneo hebu kaangalie mitaa kama masaki, osterbay mbezi beach hamna watu kulee mitaa imekaa fresh na hamna mbanano.mm nawashauri jiji ili kupunguza hii nyomi wapandishe gharama za maisha hasa vyakula watakimbia wenyewe hawa wazurulaji.pia better soln ni kuanzisha kodi ya kichwa na hii iwe inalipwa through systems.yan kwa wafanyakazi tukwatwe kwenye mishahara na kwa wafanyabishara waanzishiwe utaratibu mzuri and then ziwekwe road block pale labda chalinze au hata mizan na kwenye njia zote zinazoingia dar, kama ni mwenyeji onyesha id yako ya kodi na watacheki kwenye system kujua kama ni kweli na kwa wageni wapigwe charges za kuingia mjini nakwambia hili likianza wakuja wengi watarudi makwao na pia tutadhibiti kwa kiasi kikubwa watu wanaokuja hapa dar na hawana wanachokuja kufanya
Salute bro!! Hapo umemgonga kichwani hasa.Mzaramo zake ngoma/mdundiko.....
Mzaramo nyumba zake si mnazijuwa....
Mzaramo idadi ya watoto....
Mzaramo biashara akifanya lazima ife baada ya muda mfupi...
In short, wakuja ndo wanaobadirisha na kukuza uchumi wa eneo husika
Wakuja ndo huwa wanajenga majengo mazuri ya eneohusika
Hao wakuja akina Mengi, Bakhresa, Manji, Mwaibula, Keenja, Mkapa, Jk Kikwete, JK Nyerere, Leodiga Tenga, Mwingira, Wahindi, Wale wa mlimani city, wale wa Jmall, wale wa ..... Et etc ndo walioibadirisha Dar na ikawa na muonekano akalau wa jiji....
Dhambi ya ubaguzi huwa haiishi, ni kama kula nyama ya mtu, ukishaanza kuila hutaacha. So long as wa kuwabagua wapo, utaendelea tu kuwabagu.
Wakiisha wa nje ya Dar, utaanza we wa Msanga, wewe wa mbagala hivyo si mzaramo sana.. Etcetc
Sasa yakifanyika hayo huoni kuwa hao wakuja ndiyo watakaobaki mjini peke yao?kwa sababu wao ndiyo wenye uwezo wa kugharimia yote hayo kutokana na wengi wao kuwa na uchumi mzuri kidogo tofauti na wazaramo?hapa tu tayari maisha ni mzigo kwenu nyie mnaojiita wa hapahapa,je gharama ikiongezeka?si ndiyo kabisa mtawaachia kina Mangi hadi wake zenu?na hao wakuja ndiyo wanayoistawisha Dar kwa taarifa yako!na siku serikali ikiwa fair kwenye mgawanyo wa rasilimali dar itabaki uchi.Ni kweli usemayo ndugu.mji umejaa sana.ukienda kkoo ni vurugu hamna pa kukanyaga.bugurun ndo acha kabsa ni watu ambao wanazurura tu.yote tisa kumi nenda mbagala ndo utajua kuwa mji umevamiwa yaan kuna watu balaa ni kwa sababu kule maisha ni cheap chumba buku 3 japo hakina dirisha wala mlango yan pagale.ila unaposema mji una kero kwa kujaa watu si kila eneo hebu kaangalie mitaa kama masaki, osterbay mbezi beach hamna watu kulee mitaa imekaa fresh na hamna mbanano.mm nawashauri jiji ili kupunguza hii nyomi wapandishe gharama za maisha hasa vyakula watakimbia wenyewe hawa wazurulaji.pia better soln ni kuanzisha kodi ya kichwa na hii iwe inalipwa through systems.yan kwa wafanyakazi tukwatwe kwenye mishahara na kwa wafanyabishara waanzishiwe utaratibu mzuri and then ziwekwe road block pale labda chalinze au hata mizan na kwenye njia zote zinazoingia dar, kama ni mwenyeji onyesha id yako ya kodi na watacheki kwenye system kujua kama ni kweli na kwa wageni wapigwe charges za kuingia mjini nakwambia hili likianza wakuja wengi watarudi makwao na pia tutadhibiti kwa kiasi kikubwa watu wanaokuja hapa dar na hawana wanachokuja kufanya
Ulichokiongea na ulichopost ni vitu tofauti kabisa! Hii inadhihirisha bongo yako isivyo na ushirikiano!:banplease:
Vp mkuu kerubi afunikae leo umeenda kwenye ibada?
aah wapi!kanisani nikienda nitaishia kukaa nje tu maana ndani kumejaa wakuja tuu,wametuharibia na ibada zetu siku hizi badala ya kuhubiri biblia ni kucharaza ndombolo ya solo na kelele nyiiiingi,mtu umetembea kwenye bar wiki nzima ukikesha na ndombolo jpili unaenda ibadani ukakae na Mungu wako utubu madhambi huku kamuziki ka huzuni huzuni kanazidi kukutia uchungu utubu ghafla ni ndomboloo ilee na kelele zaidi ya bar unazikuta humo.Hawa ni wakuja tu akina Mwisege,Mwaisabula,Mwakerubi yaani fujo tu ah!murudi kwenu bwana!
Nimezaliwa na kukulia Dar lakini sasa imenishinda.Dar es salaam haifai tena.Imejaa watu kuzidi uwezo wake,huduma muhimu kama maji na umeme sasa ni kama lulu,joto kali hali ya hewa mbaya ni kuvuta vumbi na moshi wa magari tuu!usafiri hapo ndio usiseme.Gari yako huoni umuhimu wa kuitumia ni kusota foleni hadi unasinzia na kustuliwa kwa honi za walioko nyuma yako.Unaamka saa tisa unalala saa sita.No time to play with your kids,no apetite with your tv,music system,mkeo anarudi kachoka kama wewe mnabaki kutazamana na kusinzia tu,no story everybody is tired!Ugumu wa maisha unasababisha watu wawe si waaminifu,matapeli kibao,malezi ya watoto yamekuwa magumu,kila kitu gharama,na watu wa mikoani wanazidi kuja tu,jamani mtakaa wapi?hivi huko kwenu mbona kuzuri zaidi ya Dar?nani anawadanganya Dar pazuri?hili ndilo tatizo la kupenda easy money hamtaki kufanya kazi,mnajua Dar pesa haramu nyingi,matokeo yake mji umejaa watu wengi kupita kiasi,hawafanyi kazi za kueleweka zenye athari nzuri kwa jamii,hawana maadili,hawana taratibu nzuri za maisha,wamefuata easy money tu hivyo hata kuutunza mji huu hakuna,mchafu,kila mtu anafanya anavyojua,matokeo yake mji hauna order,umejaa vurugu na uovu mwingi,kuanzia viongozi wa ngazi za juu hadi machinga na mama ntilie mtaani wote ni corrupt,wabinafsi,hakuna anayejali mwingine,ndio maana Dar haina mwenyewe leo.Kukosa utaratibu huku kwa jamii ya wakazi wa Dar kunaleta very negative effects kwa vijana wetu wadogo kwa kiwango cha kutisha.Kizazi chao sasa wanajiongoza wenyewe na wana mambo ya ajabu yaani sijui wakija kuitwa baba na mama hii nchi itakuwaje.Dar si salama kwa watoto na vijana wadogo kabisaaa,hapawafai kabisaaaaaa!Bandari hii si salama tena nashauri mtafute jina lingine hili la Dar es salaam mliache!na mie najiandaa kuuhama mji huu.Nimezaliwa na kukulia hapa Dar lakini hii Dar ya leo si ile ya kwetu wenyeji wa hapa.Dar imevamiwa,haifai!Pesa tunapata wala hatuzionei raha kwa njia unavyolazimika kuzipata na kuzitumia mji huu.Bora kuishi mkoani na kuridhika na maisha ya kawaida lakini yenye amani kuliko kuwa tajiri Dar.Tunawaachieni Dar yenu mpya lakini nasema OLE WAKO DAR ES SALAAM,siku mbaya zinakujia huko mbele,naam na nyingine zimefika.Nimechoka.Nakumbuka sana nabii mmoja aliyesema miji mikubwa haitafaa kwa maisha mazuri yenye maadili katika siku za mwisho wa dunia.Ngoja tu nijiondokee mji huu because more is about to come!
Uandishi mwingine bhana ........ sijui ni ngonjera!!!!!!!!??:noidea: