kerubi afunikaye
JF-Expert Member
- May 20, 2013
- 1,183
- 1,061
Nimezaliwa na kukulia Dar lakini sasa imenishinda.Dar es salaam haifai tena.Imejaa watu kuzidi uwezo wake,huduma muhimu kama maji na umeme sasa ni kama lulu,joto kali hali ya hewa mbaya ni kuvuta vumbi na moshi wa magari tuu!usafiri hapo ndio usiseme.Gari yako huoni umuhimu wa kuitumia ni kusota foleni hadi unasinzia na kustuliwa kwa honi za walioko nyuma yako.Unaamka saa tisa unalala saa sita.No time to play with your kids,no apetite with your tv,music system,mkeo anarudi kachoka kama wewe mnabaki kutazamana na kusinzia tu,no story everybody is tired!Ugumu wa maisha unasababisha watu wawe si waaminifu,matapeli kibao,malezi ya watoto yamekuwa magumu,kila kitu gharama,na watu wa mikoani wanazidi kuja tu,jamani mtakaa wapi?hivi huko kwenu mbona kuzuri zaidi ya Dar?nani anawadanganya Dar pazuri?hili ndilo tatizo la kupenda easy money hamtaki kufanya kazi,mnajua Dar pesa haramu nyingi,matokeo yake mji umejaa watu wengi kupita kiasi,hawafanyi kazi za kueleweka zenye athari nzuri kwa jamii,hawana maadili,hawana taratibu nzuri za maisha,wamefuata easy money tu hivyo hata kuutunza mji huu hakuna,mchafu,kila mtu anafanya anavyojua,matokeo yake mji hauna order,umejaa vurugu na uovu mwingi,kuanzia viongozi wa ngazi za juu hadi machinga na mama ntilie mtaani wote ni corrupt,wabinafsi,hakuna anayejali mwingine,ndio maana Dar haina mwenyewe leo.Kukosa utaratibu huku kwa jamii ya wakazi wa Dar kunaleta very negative effects kwa vijana wetu wadogo kwa kiwango cha kutisha.Kizazi chao sasa wanajiongoza wenyewe na wana mambo ya ajabu yaani sijui wakija kuitwa baba na mama hii nchi itakuwaje.Dar si salama kwa watoto na vijana wadogo kabisaaa,hapawafai kabisaaaaaa!Bandari hii si salama tena nashauri mtafute jina lingine hili la Dar es salaam mliache!na mie najiandaa kuuhama mji huu.Nimezaliwa na kukulia hapa Dar lakini hii Dar ya leo si ile ya kwetu wenyeji wa hapa.Dar imevamiwa,haifai!Pesa tunapata wala hatuzionei raha kwa njia unavyolazimika kuzipata na kuzitumia mji huu.Bora kuishi mkoani na kuridhika na maisha ya kawaida lakini yenye amani kuliko kuwa tajiri Dar.Tunawaachieni Dar yenu mpya lakini nasema OLE WAKO DAR ES SALAAM,siku mbaya zinakujia huko mbele,naam na nyingine zimefika.Nimechoka.Nakumbuka sana nabii mmoja aliyesema miji mikubwa haitafaa kwa maisha mazuri yenye maadili katika siku za mwisho wa dunia.Ngoja tu nijiondokee mji huu because more is about to come!