Wakubwa zangu, nisaidieni!

Wakubwa zangu, nisaidieni!

::
Kaka,,usisahau kuwa yule umpendae HUKUPANGA WEWE awe wako,,ila MUNGU PEKEE ndiye anajua amekupangia nani.
::
Wakati mwingine tunapenda saana hadi tunasahau kujipenda na kujua kuwa hao tuwapendao sana sio tiketi ya kudumu nao.
Watu wanabadilika na ni haki yao kubadilika kwani wanafikiri.
::
Kuna haja gani ya kuchukia watu wasio na hatia na pengine hawajui lolote kuhusu mapito yanayokuumiza? Zungumza na moyo wako.
=
 
Nakaribia Kufikisha Mwaka, toka niwe na rafiki wa kike ambae siku moja nilitegemea tuje kuishi pamoja na kujenga familia bora, nilimpenda sana na hata nilijitoa kwa ajili yake ili awe katika sehemu salama. Siku chache alipo ludi chuoni ( yeye bado anasoma ) alianzisha uhusiano na mtumishi wa kanisa lao, na ameniambia mwenyewe kua ana mpenda mtumishi zaidi yangu, Nimekubali matokeo kwasababu ameamua yeye ingawa hajui ni jinsi gani naumia na niliumia kwa ajili yake. Tatizo ambalo ninalo ni kwamba najikuta imani niliyo nayo inatoka na kunipelekea kuya chukia mambo ya Mungu, watumishi na hata waumini wa Dini zote kwani naona ni ubatili mtupu hizi dini. Naombeni ushauri wenu wa jinsi gani naweza epukana na haya mawazo na kuanza maisha yangu mapya, kwani napata mawazo ya kuzuru mtu, na kuasi Mungu alie niumba.

''nilimpenda sana''hii inamaanisha ni hapo zamani na sio sasa hivi basi kwa maana hiyyo ni rahisi kumpotezea na haina haja ya kuwachukia watumishi wa Mungu kwani haitasaidia kitu kwani si watumishi wote wako hivyo, pia mshukuru tu Mungu kwani huwezi jua amekuepusha na nini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom