Zero One Two
JF-Expert Member
- Sep 16, 2007
- 9,346
- 3,033
Nakaribia Kufikisha Mwaka, toka niwe na rafiki wa kike ambae siku moja nilitegemea tuje kuishi pamoja na kujenga familia bora, nilimpenda sana na hata nilijitoa kwa ajili yake ili awe katika sehemu salama. Siku chache alipo ludi chuoni ( yeye bado anasoma ) alianzisha uhusiano na mtumishi wa kanisa lao, na ameniambia mwenyewe kua ana mpenda mtumishi zaidi yangu, Nimekubali matokeo kwasababu ameamua yeye ingawa hajui ni jinsi gani naumia na niliumia kwa ajili yake. Tatizo ambalo ninalo ni kwamba najikuta imani niliyo nayo inatoka na kunipelekea kuya chukia mambo ya Mungu, watumishi na hata waumini wa Dini zote kwani naona ni ubatili mtupu hizi dini. Naombeni ushauri wenu wa jinsi gani naweza epukana na haya mawazo na kuanza maisha yangu mapya, kwani napata mawazo ya kuzuru mtu, na kuasi Mungu alie niumba.