Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,354
- 23,760
Ndugu Zangu Watanzania,
Wakristo Mbalimbali Wamekesha na kushinda Makanisani Wakimuombea Heri Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Ambapo waumini hao ambao wanasherehekea Sikukuu ya Chrismas Ikiwa Ni kumbukumbu ya kUzaliwa Kwa Yesu kristo.
Ambapo wengi wameonyesha kuridhishwa ,kufurahishwa na kukoshwa na hali ya Amani na utulivu vilivyo tawala na kutamalaki hapa Nchini. Ambavyo vimetoa nafasi kwa wakristo wote kufanya ibada zao kwa utulivu mkubwa bila bugudha wala hofu wala wasiwasi wala kitisho chochote kile cha kiusalama.
Hali iliyopelekea na kuwafanya kumshukuru sana Mungu kwa kuwainulia Ama kuliinulia Taifa Rais Samia Kama Mkuu wa Nchi , serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama. Ambapo wamesema na kudai kuwa uimara ,ushupavu , umadhubuti,uhodari na umakini wa Rais Samia ndio Umelifanya Taifa kuendelea kuwa katika hali ya amani na utulivu na hivyo kutoa nafasi kwa watu wote walio na Dini na wasio na Dini kufanya shughuli zao kwa amani.
Kwa hakika Rais Samia anaendelea kudhihirisha ya kuwa yeye ni chaguo la Mungu aliyeinuliwa kwa mkono wa Mungu Mwenyewe kulitumikia Taifa hili na watanzania wote kwa ujumla wake. Ndio Maana tumevuka milima na mabonde na kubakia salama. Ndio maana tumevuka na kukwea vilele vyote vilivyojitokeza mbele yetu kama Taifa.
Tuna kila sababu ya kuendelea kumuunga mkono Rais wetu Mpendwa na kuendelea kudumisha amani na utulivu wetu ambavyo ndio msingi wa maendeleo ya Taifa letu. Tunaumaliza Mwaka na kuingia mwaka mpya tukiwa Tumeungana na kushikamana kwa pamoja Kama Taifa.
Mama anatuvusha salama na kutufikisha Ng'ambo ya pili salama salimini. Tunaelekea Nchi ya ahadi , Nchi ya asali na Maziwa ,Nchi ya Matumaini na yenye kumfanya kila mmoja wetu kutimiza ndoto zake. Rais Wetu Mpendwa anabakia kuwa Shujaa wetu na Jemedari hodari.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.