Kwa maoni yako nini kifanyike?Kama ukiwa unaangalia umbali wa mita moja kutoka usawa wa macho yako utaona hili ni jambo jema. Lakini kwa hakika hili ni jambo la hatari na la kulaaniwa kabisa. Tukianza kugawana bucha, tutakuja kugawana maduka, baadaye tutagawana hata visima vya kuchota maji, na mwisho wa siku hata barabara tutatakiwa kutengeneza za waislam na wakristo. Nasikitishwa sana na silence ya serikali juu ya jambo hili.
Hapo awali tuliishije? kwanini tusirudi kwenye maisha ya tangu mwanzo. Ni nini kilichotufikisha hapa? Kuna mtu alileta hapa ushahidi wa Quran kwamba waislamu hawazuiliwi kula nyama iliyochinjwa na Mkristo. If that is the case, wana sababu gani ya kuleta ugomvi kwenye masuala ya kuchinja? Kwa hakika serikali ichukue maamuzi magumu kumaliza tofauti na choko choko hizi zisizo na maana.Kwa maoni yako nini kifanyike?
Tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa Rais Jakaya Kikwete, kwa uzembe wa Bunge na kwa sababu ya upuuzi wa CCM. tafakari kisha chukua hatua
Imetulia hii, tena inafaa mabucha yote yabandike lebo ya aina hii ili kila mtu achague nyama aipendayo vinginevyo tutalishana vubudu tuu, watu miaka yote wananyonga leo wanadai wachinje.
Tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa Rais Jakaya Kikwete, kwa uzembe wa Bunge na kwa sababu ya upuuzi wa CCM. tafakari kisha chukua hatua
hapa kijana ustadh juma sidhani kama ataweza kusogelea..
Hii c dalili nzuri hata kidogo.. Tumeanza na mabucha.. Nini kitakachofuata baadae..? Maana tunashabikia lakini hebu tuangalie huko mbele kwa mwendo huu.. Ninawafikiria wanangu wanaokuwa katika mkanganyiko huu.. Ninawatengenezea mazingira gani ya kuishi kama Watanzania..? Naogopa sana.. Serious..
Safi sana.. Kwa sababu JK alikuwa anafikiri anaikomoa CDM sasa atavuna upuuzzzi aliupanda...
yaani mpaka inakera kabisa, hivi kwa nini uongozi hauchukua hatua zinanoeleweka? jibu ninalo "tuna rais dhaifu sana"
Sasa tugawane kila kitu: shule, hospitali, Mabasi, mikoa, nyumba za kupanga, maduka, vyuo vikuu etc
"Tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa Rais Jakaya Kikwete, kwa uzembe wa Bunge na kwa sababu ya upuuzi wa CCM." tafakari kisha chukua hatua
toba...naiyonea huruma tanzania yangu....
udhaifu wa viongozi wako ndo uliotufikisha hapa.
Sasa tugawane kila kitu: shule, hospitali, Mabasi, mikoa, nyumba za kupanga, maduka, vyuo vikuu etc
bora kuwepo HALAL waislam na hiyo UNHALAL wakristo butcher
Tunaishi kwa upendo sisi ni jamii mmoja, ki-historia waislam ndo wanachinja miaka yote, na hata kijijini kwetu ikiwa kuna sherehe kwa mkiristo anaitwa muislam achinje ili sisi ambao tunaamini mkiristo hawezi kuchinja tule nyama hiyo..! Hatufanyi mashindano ya kuchinja au kitu cha aina hiyo na ndo maana mabucha ya kiti moto yapo kibao na tunayaheshimu..! Ni suala la kiimani kwamba nyama akichinja muislam mkiristo anao uwezo wa uila bila shida wakati muislam hali nyama aliyochinja mukristo. Hili siyo suala la jana wa juzi ni tokea enzi na enzi, labda uniambie kuwa mnataka mabadiliko sasa
Hakuna haja ya kuwa na hofu.....duniani kote kwenye mchanganyiko wa imani huu ndio utaratibu.......kumbuka suala la kuchinja kiislamu ni la waislamu tu na halihusu imani zingine......mazoea tulokuwa nayo hayakuwa sahihi