Wakonta Kapunda: Binti mlemavu wa kupigiwa mfano kwa walemavu na jamii kwa ujumla

Complicator

JF-Expert Member
Aug 23, 2013
2,198
3,566
Kwa wasiojua historia ya huyu binti kwa kifupi ni kwamba alipata ajali ya kugongwa na gari akiwa katika mahafali yake ya elimu ya sekondari, ajali iliyompelekea kupata jeraha kwenye uti wa mgongo kisha ulemavu wa kupoza sehemu ya mwili wake.....

Kwenye siku ya walemavu ameandika haya

"Nilivyopata (JUM) jeraha la uti wa mgongo (ulemavu) ambao kupona kwake bado kunafanyiwa utafiti, ilinibidi niikubali hali hii mpya kwangu ya ulemavu.

Ilinibidi nianze kusoma na kujifunza kuhusu jerala la uti wa mgongo na yote yanayoizunguka hali hiyo. Mengine yalikuwa magumu kumeza lakini ndio tayari yalikuwa ya kwangu so nikayaelewa kama yalivyo bila ku-judge wala kuweka critics.

Ikafika muda nikawa najielewa na naujua mwili wangu kuliko nilivyowahi kuujua kabla sijapata JUM. JUM imefanya afya yangu iwe mgogoro lakini baada ya kujijua nikawa naitunza afya niliobaki nayo (A) naitunza mimi mwenyewe (B) naitunza kwa umakini mkubwa sana.

Mikono yangu haishiki, miguu haitembei, siwezi kukaa wala kujilaza mwenyewe, siwezi kwenda haja kawaida kama zamani hivyo kujitunza mimi mwenyewe ni ngumu kimtindo.

Lakini ndugu na jamaa mnaoona hii post, niliruhusiwa na wazazi wangu kuhamia kwangu nijitegemee mwenyewe kwa sababu hii kubwa; NAWEZA KUJITUNZA MWENYEWE. Sio kifedha wala sio ki-material.

Hivi sasa sasa naweza nikaishi na msaidizi yeyote yule ili mradi ana utayari. Najua kila kitu kuhusu mimi. Saa ngapi nilale, nile kipi, nipumzike staili gani, niogee sabuni gani, ninywe maji gani, nikalie kochi lipi, nioge mara ngapi nk nk.
Hio mifano niliyotaja inahitaji utayari wa mtu.

Mimi nikisema mama siwezi kuishi bila wewe sidanganyi ni kweli ni ngumu sana kuishi bila mama, nikisema siwezi kuhakikisha usafi wa mwili wangu umeenda sawa ni kweli kwasababu ni kweli sijisafishi mimi. LAKINI nilipokubali kujihusisha na maisha niliyonayo sasa, nimejikuta nikiweza yasiowezekana. Mimi pia narudisha utukufu kwa Mungu kwasababu sijui bado inawezekanaje lakini wapendwa Imewezekana mimi kujihudumia mwenyewe kwa HALI hii takribani miezi 13 sasa.

Tukiwa tunaadhimisha #internationaldisabilityday napenda kutoa wito kwa wenzangu wenye ulemavu ku-take part kwenye maisha yetu. Tuwe mstari wa mbele kujipenda na kujitunza. Tuwape ushirikiano wazazi na wapendwa wetu, na wote waliochagua kuwa upande wetu, tuwape wepesi.

Ni ngumu sana mwanzoni - ILA INAWEZEKANA. Na baadae ukizoea mimi ni shuhuda namba 1 nakuhakikishia sio ngumu kama tunavyodhani kabla hatujajaribu."
FB_IMG_1575368749478.jpeg
 
Miezi 13..!? bado sana kwa kutoa bandiko_Japo anahitaji faraja ya watu wa karibu
 
Pole kwake. Hakika kila mwanadamu anayo mitihani yake, inatofautiana kwa namna inavyokuja.
Mingine ni migumu zaidi na kuhitaji uvumilivu wa hali ya juu.

Jambo moja pekee unaloweza kusema kwa hali kama hiyo ni kwamba .......MUNGU pekee ndiye anajua na hakika mpango wake ilikuwa lazima utimie.

Zawadi pekee uliyosalia nayo ni UHAI na utajiri wa HEKIMA &na MAARIFA.

MUNGU akupunguzie maumivu.
 
Ujinga na ushamba ulimsababishia mtoto wa watu kitu cha kudumu na kuondoa ndoto zake zote.
Mkuu samahani, Unaweza kuelezea kidogo ajali hiyo ilikuaje maana binafsi sikuisikia?
 
Mara nyingi nilimtazama huyu dada kama role model wangu,kuna wakati nilijitahidi kufanya kila kitu kwa usahihi lakini bado sijafanikiwa.


Kuna watu walikuja katika maisha yangu wakiwa na ahadi za matumaini lakini wakapotea kama barafu juani.


Nimetazama support aliyoipata huyu dada ikawa ni kubwa kumtosha yeye kusimama na hali aliyonayo,nikasema njia haziwezi kufanana nami napaswa kuwa na njia yangu ya pekee haijalishi ni kiasi gani itakuwa ngumu.


Nikapata marafiki wachache wenye disability ili tubadilishane mawazo nione nachoweza kujifunza kwao na hatimaye nipate funzo litakalonipanua ubongo.


akini bado walikuwa ni matajiri vya kutosha kumudu kwemda abroad kusoma na kupata matibabu,waliwategemea wazazi na wadhamini,haikufaa kwani nilihitaji kujifunza kutoka kwa wasio na wategemezi,sponsor wala ndugu wenye moyo wa upemdo na hekima.


Ilinipasa kutenda kwa namna yangu kuweza kusonga mbele,ilinipasa kusimama mwenyewe bila wategemezi,sponsor wala ndugu,nalipata kuomba shauri katika mtandao huu pia.


Yalikuwa ni matusi kejeli na dhihaka,nikahisi dunia inanitenga,dunia inanielemea,dunia inakwenda kinyume nami kabisa,nikatafakari watoa kejeli na dhihaka kwanini wanatenda hivyo,ni wenye shibe,wametosheka na au wana uchungu mkubwa na maisha?


Kwanini wanidhihaki na kunikejeli,mwisho nikakata tamaa nikapoteza kiasi,nikalalamika sana,nikajikatia tama na kuona maisha yangu yamefika mwisho nikakosa ari ya kuishi.

Nikanung'unika na kumlaumu Mungu,mbona huna usawa!,hunioni?,mbona nakuomba kila siku? Bwana wewe hunisikii? Basi na unichukue sasa!..


Siku moja ukaingia ujumbe,alikuwa ni mwanamume,akanipa habari za Mungu,akanitia moyo na kunitaka kutokukata tamaa,nikamtafakari.

Nikapata moyo wa ujasiri,nikatazama mbele kwa matumaiji,nikaingia katika juhudi tena,ilihitaji moyo na ujasiri lakini nilijikaza na kupita ambamo kwa moyo mwepesi usingedhubutu.

"Ungekuwa huna huo ulemavu,ningekusaidia,ungekuwa mbali sana" kauli hizi zilitamalaki sana,nilimtazama mtoa kauli nikatabasamu na kukosa la kumjibu,nitamjibu nini ilhali halikuwa kusudio langu kuwa hivi?.


Kwa njia zote zipitazo,pasi na kujali mabonde na milima sitokuwa na chaguo zaidi ya kuzipita ,hakuna atakayejali wala kuumia na haya yanipitayo zaidi yangu mwenyewe.


Siku ya walavu duniani ni kwa ajili ya nani? Mbona wengi haitugusi? Inawagusa wenye njia zao na neema zao,pole sana na hongera sana Wakonta,sijawahi kusita kukutumia jumbe si wewe tu,bali walemavu wote walioendelea,niliowachukulia kama role models wangu,hamzijibu,naamini mtakuwa bize na siku ya walemavu duniani,lakini ni za siku nyingi,miezi mingi.
 
Marehemu Reginal Mengi hv alimzawadia sh.ngapi huyu mrembo?

Ukiingia page yake ya insta huyu bibie anawaka bwana,hapo tumu ana ki baby face

plus filter plus make up then kitu kinapostiwa insta "lazima uwehuke",wanamvalishaga michuchumio

ya maana, napenda sana kuona anavyokua treated.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Back
Top Bottom