Wakongo na Watanzania tuna asili moja?

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Hivi sisi Wakongo na Watanzania hua tuna asili moja au?

Yaani mkongo kama mimi hivi

Nikiwa safarini nikikutana na raia wa INCH nyingine tofauti na Tanzania hua nahisi mwili wangu una kabaridi fulani hata kama tunaongea lugha moja utakuta sina shauku kabisa ya kuona nipo na mwenzangu.

Na hata kwa majanga mengi ambayo yanatukuta mara nyingi wa Tz wamekuwa mstari wa mbele kutufuta macho au kutuonea huruma.
 
Huwa ninafurahi sana kuwa na Waganda, Wakenya (hasa waluo au kwa lugha yetu wajaloa) na wakongo kuliko mataifa mengine yoyote ya Afrika. Waganda ni waungwana sana.
Kinacho fanya Waganda kua tofauti na wengine ni wasomi wastarabu na ni watu wanao penda tamaduni zao sana hasa lugha yao ya kiganda wana ichanganya na kiingereza inavutia sanaa
 
Kinacho fanya Waganda kua tofauti na wengine ni wasomi wastarabu na ni watu wanao penda tamaduni zao sana hasa lugha yao ya kiganda wana ichanganya na kiingereza inavutia sanaa
Siyo kwamba waganda wote ni wasomi; ni kwamba desturi zao ni za kijumuia, siyo za kibinafsi kwa hiyo wanajua sana kuishi kwenye jumuia yoyote bila kutanguliza ubinafsi.
 
Watanzania wakarimu sana nakumbuka niliwahi kuwa moro pande fulani kuna m south tulikuwa tunakunywa nae tungi hajui kiswahili misosi tunamsaidia kuagizia na kumsaidia kumpanga demu wa kutafuna jamaa aliishi kwa amani sana.
 
Noma sana!
 
Hivi sisi wakongo na watanzania hua tuna asili moja au?

Yaani mkongo kama mimi hivi
Nikiwa safarini nikikutana na raia wa INCH nyingine tofauti na Tanzania hua nahisi mwili wangu una kabaridi fulani hata kama tunaongea lugha moja utakuta sina shauku kabisa ya kuona nipo na mwenzangu

Na hata kwa majanga mengi ambayo yanatukuta mara nyingi wa Tz wamekuwa mstari wa mbele kutufuta macho au kutuonea huruma
Mie mwenyewe hua naumia sana nikisikia wananchi wasiokua hatia wameuwawa kwa kukatwa mapanga na waasi huko DRC raia kukimbia miji yao kuokoa maisha yao
 
Mie mwenyewe hua naumia sana nikisikia wananchi wasiokua hatia wameuwawa kwa kukatwa mapanga na waasi huko DRC raia kukimbia miji yao kuokoa maisha yao
Mimi mwenyewe naumia kuona PK anajimwambafy pale Kivu na M23 yake, hadi nikajiuliza watz tumeshindwa kabisa kuwasaidia rafiki zetu akina Fiston Mayele, Christain Bella, Pacho Mwamba n.k? Maana kongo ikistawi Tanzania ina neemeka.
 
Watanzania wakarimu sana nakumbuka niliwahi kuwa moro pande fulani kuna m south tulikuwa tunakunywa nae tungi hajui kiswahili misosi tunamsaidia kuagizia na kumsaidia kumpanga demu wa kutafuna jamaa aliishi kwa amani sana.
Kwamba mlisaidia kutenda dhambi si ndio?!
 
Back
Top Bottom