Wako wapi watu wako mliosoma wote

Mwanang side toka 2002 hadi leo japokua maisha yametutenga baada ya yye kuoa,John mjumbe toka 2008,mwanang wa chuo basilio! Life goes on …kifo kikiwa mbele yetu.
 
Aisee mmoja alikuwa ndezi saizi ni captain jwtz alikuwa anaitwa Mangulu yeye tumemaliza six Kaunga jeshi support ya familia ya kutosha saizi anakula mema ya inchi.......

Maisha ni fumbo bila support kutoboa sio rahisi
Mkuu huyo unasema alikua ndezi miaka ya mbeleni usichangae ukimuona akiwa Mkuu wa Majeshi au ofisa mkubwa wa ngazi za juu, Jeshini ukiingia na Elimu ya chini ni rahisi kupanda vyeo mpaka ngazi za juu, ni tofauti na yule anayeingia jeshini tayari akiwa na Elimu ya chuo kikuu, mtu kama huyu aliyeingia na Elimu ya juu anakua alijui jeshi vizuri tofauti na yule aliye ingia na Elimu ya kati anakua ameanzia chini.
 
-Aah nawaogopa Kwa sasa, Kwa sababu wengi wao nilikuwa nawadharau kipindi Niko primary kutokana na wao kufanya vibaya Mimi kufanya vizuri (kuwazidi shule) kimsingi nilikuwa nakuwa 1-3 hapo
-wengi wao sasa ni maaskari, police,jw, prison, immigration,tgs,tanapa, raia maafisa kwenye utumishi wa umma
-hata nikiwa na shida ya hela huwa siwapigi mizinga
 
Facing the future... Safari ya mtoto ndio imeanza wakati ya mzazi pengine ndio imefika.. Huyu anaenda kukutana na mengi tuliyojadili hapa
 
Nimetoka muda si mrefu hapo. Kigamboni upepo wa bahari unawapa raha sana. Mwigulu awaangalie nanyi muongezewe kodi.πŸ˜‚πŸ˜‚ Joke.

Niliambiwa marafiki utakaanza nao chuo ndio hao utamaliza nao. Hilo nimeprove.

Familia Yako kwa maana ya mke na watoto ndio watu wako muhimu zaidi.
Ni sahihi kabisa.

Wazazi wako ndio wanaokupenda kutoka moyoni na kamwe hawawezi kukuombea mabaya. Hili dhahiri.

Wakati wa dhiki ndio muda rafiki anapatikana. Sio wadau. Wadau ni muda wa maslahi.

Kuna watu Mungu anaweza pia waleta kwasababu maalum. Aidha washike mkono, wakushike mkono au mshikane mikono mvuke salama.

Shukrani kaka Monetary doctor
Nipe code, Kigamboni safi sana.
 
Naam ujumbe mzurii sana bruh,,

Kigamboni kupo poa na kutulivu kiasi upepo ndo mkali kidogo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…