Wako wapi G55?

Asante sana kwa kuleta rekodi hiyo.

Sijajua msukumo wao wakati ule ulikuwa ni nini kwa vile bado kulikuwa na matumani ya kufikia lengo la kuwa na serikali moja. Inawezekana walishayaona mapema mambo haya ambayo tunayaona leo kuwa serikali ya Muungano ilikuw inapotzea nguvu huko Zanzaibar na vile vile wazanzibar walikuwa wakishika madaraka ndani ya serikali ya Muungano kushughulika na mambo ya Tanganyika ambayo hayakuwa ya muungano.

Mambo hayo ya ukiukwaji wa katiba hasa ndiyo yalisababisha. Hadi kufikia mwaka huu, ukiukwaji huo umeongezeka zaidi, lakini nguvu ya kudai Tanganyika imezidi kuwa dhaifu, hasa kwa sababu hakuna aliyeko mstari wa mbele waziwazi, wengi wanajificha nyuma ya rasimu ya Warioba, na wamesababisha waonekane kama vile hawana hoja kwa kuwa hawataki hata kujulikana, wanataka "kura ya siri". Hii tabia ya ulafi na unyemelezi (opportunism) ndiyo itakayodidimiza Tanganyika kwenye bunge la katiba.

Mwalimu Nyerere aliweza kusimama peke yake dhidi ya hoja ya G55 ambayo ilishavuka hatua ya kuandikiwa azimio la bunge, na kilichokuwa kimebaki kilikuwa ni utekelezaji wa azimio hilo la kuandaa utaratibu wa kuanzisha serikali ya Tanganyika ndani ya muungano. Wanaodai Tanganyika sasa wanaonekana dhahiri ni dhaifu sana ukilinganisha na wale G55 wa mwaka 1993, na hata tunaona jinsi walivyosambaratishwa kirahisi sana na hotuba ya Kikwete ya kufungua bunge. Huko kwenye vikao vya kamati hawafurukuti, na kwenye kura ya kupitisha vifungu wanaogopa kuonesha misimamo yao ya ndani, mwisho wake ni kuwa Kikwete na wanaCCM wenzake watafanikiwa tena kuisambaratisha hoja kwenye hatua ya bunge la katiba. Nafasi pekee iliyobaki ni ya kuikataa rasimu kwenye kura ya maoni baada ya kupitishwa na bunge la katiba.
 
Hayo ni majembe. Nimepitia majina yote sijaona hata mmoja aliye kwenye bunge la katiba kwa wale ambao bado wapo hai. Kama wapo basi tujulishane na watusaidie kuipigania Tanganyika yetu
 
Asanteni mlionipa updates. Naombeni wenye taarifa za kujazia kuhusu hao ambao taarifa zao hazijatosheleza mchangie kwenye huu uzi, nafikiria kuwa zikikamilika nitoe makala kabisa kwa faida ya wengi, wakiwamo wale wasio na fursa ya kutumia hii mitandao.
 
Safi sana mkuu!!
maana nililkuwa naumiza sana kichwa kuhusu G55, niliuliza hapa jamvini , nikajibiwa eti mie ni tunda la shule za kata.
pia umenikumbusha Mh Sebasstian Kinyondo.
 
Asante sana kwa taarifa. Hawa watu walithubutu kusema kwa uhuru. JK Nyere aliwajubu kwa hoja, ila JMK anatumia nguvu na vitisho kufifisha fikra pevu. Anadanganya, anahadaa, anauma kuwili, anatisha..na mambo yanayofanana na hayo. Tanganyika.....inakuja tu!
 
Back
Top Bottom