Setuba Noel
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 426
- 210
- Thread starter
- #21
Asante sana kwa kuleta rekodi hiyo.
Sijajua msukumo wao wakati ule ulikuwa ni nini kwa vile bado kulikuwa na matumani ya kufikia lengo la kuwa na serikali moja. Inawezekana walishayaona mapema mambo haya ambayo tunayaona leo kuwa serikali ya Muungano ilikuw inapotzea nguvu huko Zanzaibar na vile vile wazanzibar walikuwa wakishika madaraka ndani ya serikali ya Muungano kushughulika na mambo ya Tanganyika ambayo hayakuwa ya muungano.
Mambo hayo ya ukiukwaji wa katiba hasa ndiyo yalisababisha. Hadi kufikia mwaka huu, ukiukwaji huo umeongezeka zaidi, lakini nguvu ya kudai Tanganyika imezidi kuwa dhaifu, hasa kwa sababu hakuna aliyeko mstari wa mbele waziwazi, wengi wanajificha nyuma ya rasimu ya Warioba, na wamesababisha waonekane kama vile hawana hoja kwa kuwa hawataki hata kujulikana, wanataka "kura ya siri". Hii tabia ya ulafi na unyemelezi (opportunism) ndiyo itakayodidimiza Tanganyika kwenye bunge la katiba.
Mwalimu Nyerere aliweza kusimama peke yake dhidi ya hoja ya G55 ambayo ilishavuka hatua ya kuandikiwa azimio la bunge, na kilichokuwa kimebaki kilikuwa ni utekelezaji wa azimio hilo la kuandaa utaratibu wa kuanzisha serikali ya Tanganyika ndani ya muungano. Wanaodai Tanganyika sasa wanaonekana dhahiri ni dhaifu sana ukilinganisha na wale G55 wa mwaka 1993, na hata tunaona jinsi walivyosambaratishwa kirahisi sana na hotuba ya Kikwete ya kufungua bunge. Huko kwenye vikao vya kamati hawafurukuti, na kwenye kura ya kupitisha vifungu wanaogopa kuonesha misimamo yao ya ndani, mwisho wake ni kuwa Kikwete na wanaCCM wenzake watafanikiwa tena kuisambaratisha hoja kwenye hatua ya bunge la katiba. Nafasi pekee iliyobaki ni ya kuikataa rasimu kwenye kura ya maoni baada ya kupitishwa na bunge la katiba.