Wakivuta wao sigara, tukivuta sisi bangi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakivuta wao sigara, tukivuta sisi bangi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Annina, Dec 18, 2009.

 1. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Miaka 2 iliyopita katika pitapita zangu maeneo ya sinza nilikutana na bango lenye ujumbe huu "wakivuta wao sigara, tukivuta sisi bangi". Ujumbe huu ulikuwa umebandikwa kwenye maskani ya vijana wa eneo hilo - maarufu kama kijiweni.

  Leo nimeukumbuka usemi huu na nimeutafakari kidogo. Nimewakumbuka vijana wale wa kijiweni, ambao mara nyingi hakuna anaewapatiliza. Kwenye ujumbe huu wanaonekana kukata tamaa, hawaoni kama haki inatendeka na kwamba kuna matabaka ya "wao" na "sisi" - kwamba "wao" wakiiba kutoka hazina wanaombwa na kubembelezwa kurudisha walichoiba na kupongezwa kama vile ni mashujaa -maana ni "sigara", lakini "sisi" tukiiba kuku wa jirani kwa ajili ya kujikimu sheria inachukua mkondo wake maana ni "bangi"!

  Wao wakisema uongo ulio dhahiri wanaitwa wanasiasa -sigara, sisi tukitoa maoni yetu tunaitwa wehu na kutakiwa kuthibitisha - bangi! Wao wakituingiza kwenye mikataba mibovu yenye dalili ya rushwa na kuliingiza taifa kwenye janga tunaambiwa ni vijisenti tu na pengine tunasumbuliwa na wivu wa kike - sisi tukichukua rushwa ya 5000/= tunaozea segerea!

  Orodha ya wao na sisi ni ndefu... najiuliza kwa matabaka haya tunayoyajenga kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya tupo tayari kupokea matokeo yake?
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hivi ile program ya tido mhando ya kumwanika juani raisi wetu ili tumuulize maswali bado ipo na itakuwa lini?
  Swali hili itabidi ulili serve na kuuliza siku hiyo.Naogopa tu kwamba Tido ninaemjua atatayarisha program hizi tena 2010 karibu na uchaguzi! Anatafuta kumsafisha rafiki yake!
   
 3. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mchukia fisadi,
  asante, natamani ningejibiwa swali hili hata kwa njia ya hotuba za kila mwezi...
   
 4. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hile sio really, huwa wana pre-filter maswali, na mengine huwa wanayatengeneza wao wenyewe.
  Kuna mamluki huwa wanapiga simu kuonyesha kwamba ni live!
   
 5. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  I have liked your version of sigara na bangi. Its true dat. Tabaka la wao na sisi bado ni kubwa sana miongoni mwa sisi Watanzania. Lakini wengi tunalazimika kwamba ndio mfumo halisi wa maisha yetu. Na jamii imeshajengwa kuamini hivyo. Yaani ukiwa kwenye madaraka makubwa, you can get away with anything and nobody will even complain. Just take a simple example ya kifo cha aliyekuwa makamu wa rais Dk. Omary Ally Juma. Runinga zilipoonyesha mandhari ya nyumbani kwake kule Zanzibar, watanzania wengi tulipigwa na butwaa. Kila mtu akawa anahoji, inakuwaje makamu wa rais anaishi maisha duni kiasi hicho? Wengi tulisahau kwamba huende huyu bwana alikuwa mwadilifu na alikuwa anaishi kwa kipato chake halali. Wengi tuliona kwamba si haki kwa kiongozi mkubwa kama yule wa nchi kuishi maisha ya chini kiasi kile. Mifano kama hii iko michache, lakini ipo. So, jamii imeshajijengea kwamba, ukiwa kwenye nafasi fulani kubwa, hasa serikalini, basi lazima uwe na maisha ya hali ya juu, hata kama hayaendani na kipato chako halali.
   
 6. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  bangi na sigara yote ni jamii moja, hakuna yenye unafuu....stop smoking!
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  sikuwahi kuexperience CINSISTENCY kwenye uongozi wa awamu hii!huyu muheshimiwa ana mipango mingiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!mara nitahutubia wazee,mara hotuba,mara maswali mara hivi mara vile mara sijui nin!
  smtmz MKAPA WAS GOOD BANA
   
 8. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Zero,
  Umesema sawa, tatizo jamii inakuangalia kwa ulichonacho bila kujali umekipataje. Utu wa sasa ni kitu hata kama umeiba au kuua ili kupata ulichonacho. ndio maana kuna baadhi yetu linapokuja suala la pesa anaweza kumuuza hata mama yake mzazi mradi itamlipa
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Hii inafanana na ule usemi wa kizaramo
  kunya anye kuku,akinya bata kaharisha,,


  ha ha ha sorry kwa nilio wa boa but ndo methali yenyewe.
   
Loading...