Wakina mama: Chungeni sana kauli zenu

Wakina mama: Chungeni sana kauli zenu

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,883
Reaction score
40,053
Habari za wakati huu ndugu zangu.....natumaini sote tu wazima na baadhi waliopungukiwa uzima Mungu atawasaidia........

Kila mmoja wetu anafahamu ni jinsi gani ndoa zilivyojaa changamoto na mahangaiko mengi yanayozifanya ndoa kuwa ni muunganiko mgumu sana kuuingia......pengine wewe hapo msomaji unashughulikia moja ya changamoto hizo muda huu.....

Wakati mwingine mikiki mikiki ya ndoa hupelekea wanandoa kutofautiana kauli....utofauti unaowafanya wanandoa warushiane maneno.....na hapa ndipo hasa paliponifanya nitoe duku duku.....kwani hawa ndugu zetu sijui huwa wanakumbwa na ibilisi gani kwa muda huo kwani huwa hawachagui neno la kusema ilimradi tu liwe lenye kukuumiza wewe unayejibishana naye........

Ni maneno ambayo huamsha upya ugomvi na migogoro kila yakikumbukwa na yule aliyeambiwa....kwani ni mazito mmo na yanafedhehesha.....mfano; mwanamke anaweza akakuambia mbele ya kadamnasi kuwa..." Eti katika wanaume nawe ni mwanaume, umebakiwa kuvaa magauni tu" hii ni kauli mbaya sana na yenye kufedhehesha kama sio kudhalilisha...... Utasikia " kwanza hawa watoto sio wa kwako".........hizi ni baadhi ya kauli zinazolisha mengine kwani ni wanaume wachache wenye uwezo wa kuhimili kuziacha hizi kauli zipite hivi hivi ingawa zinachoma kama mtu aliyemeza kaa la moto......

Ndio maana matukio ya kuuwawa wanawake kinyama yanashamiri kila uchao....wanawake wanaopata ulemavu kutokana na vipigo vya waume zao wanaongezeka kila uchao.....ukichunguza kwa makini chanzo ni kauli mbovu za wanawake.......sio kwamba naunga mkono matukio ya ukatili wa kijinsia la hasha bali nawaasa wakina mama wawe makini na kila wakitoacho mdomoni mwao.....kwani bila ya kujua huleta matokeo mabaya sana.....kwani si kila mtu ana uwezo wa kustahimili kauli za kizalilishaji kama hizo.....kuna wale wanaume mashujaa wanaoweza kufunika kombe ili mwanaharamu apite na kuna baadhi wanaoonyesha hasira zao....hapo ndipo matokeo ya kauli chafu yanavyoonekana..........

N;B
WANAMUME WENZANGU TUJITAHIDI KUWA WASTAHILIMILIVU KATIKA NDOA KWANI KWA KUISHI NA MWANAMKE NI MTIHANI MKUBWA AMBAO MUNGU AMETUPA.......

Inapotokea umepishana kauli na mkeo usikae eneo.....ondoka uende mbali na eneo hilo lakini usiende bar kunywa pombe......
 
Kunapokuwa na ugomvi ndani ndoa na hasira ikiwa imetawala pande zote naamini hakuna anaekuwa anamwambia mwenzake maneno ya kufurahisha Mume atatupa hili Mama naye atatafuta la kukupa ili mradi aone tu amekushinda..Na sisi wanaume huwa hatuna uvumilivu unakuta unaambiwa neno moja unasahau na wewe pia ulikuwa unamwambia maneno kama hayo tu...Mahali tunamalizwa nguvu kabisa ni pale wewe unajua mke wangu ni mwaminifu sana kwenye ndoa then kupitia ugomvi huo anaamua kukuambia...''Ndiyo maana niliamua kutembea nje ya ndoa kwa tabia hizi zako'' Kauli hii huingia moja kwa moja mpaka ndani ya moyo kabisa na kufanya mwili wote kupatwa na baridi ya ghafla...Kitakachofuata hapo mwanamke ni atimue mbio sana.
 
Ukitaka kushinda vita ya maneno na mwanamke hilo usahau ndugu yangu KikulachoChako hawa viumbe hujihisi kila mara wanaonewa sasa tahadhari ya kwanza ni kutoruhusu vita ya maneno.Sisemi tusijadiliane nao la hasha kuna mwisho wa mjadala kisha inaanza vita nae atajaribu kutumia silaha hiyo aone kama itakuumiza huenda mbali na kukwambia hata hawa watoto sio wako ilhali ni wa kwako ila anataka uumie si mpo vitani.
 
Kuna jamaa yetu anatokea lile kabila la wababe,ambako wilaya tuu ni kanda maalum ya kipolisi, kwa sasa yuko jela

Alipewa kauli kama hzo, kilichofuata ni kumtenganisha yule mwanamke viungo vyote kwa panga, na aka jisalimisha polis mwenyew

Kwa kweli usipo kuwa mvumilivu unaweza kuta mnagawana majengo ya serikali, mmoja mochwari au hospital ,mmoja jela

Wanawake mbadilike kwa kweli na wanaume ukiambiwa kama hvo tuliza mzuka uskurupuke
 
Lakini ni vema mwanaume kukaa kimya au kuondoka kwa muda japo lisaa li1 ili kuepusha ugomvi kushamiri.Mara nyingi ukiwa na hasira unaweza kutoa speech mbaya sana hapa ndio uvumilivu unatoweka.
 
Jamani hata wanawake ni wastahamilivu tena sana,tuna mengi sana ya kwenu tunayabeba..tunaficha aibu zenu mno. Ukikuta mwanamke ameongea kauli ya 'udhalilishaji' pengine ni tabia yake kuropoka au amechoka na mambo yako ambayo yamekuwa yakijirudia...ama kweli mavi anye kuku akinya bata kahara jamani.
 
Sijui kwanini nimefungua huu uzi aiseeee....
Nimejikuta nakumbuka neno ambalo nilikua nikilitumia sana (nahitaji private time).
Lakini chakushangaza ndipo ilikua kama nachochea kuni kwenye kijinga cha moto agghhhh...[emoji16]
Niliposema nitoke, basi nilifuatiwa na SMS, MMS za maneno na matusi kama mvua......
Mwisho nikaona nitafute pakua napata pumziko aiseeee.....
Ebu ngoja niishie hapa maana nahisi mapigo moyo kuanza kunienda kwa kasi
 
"utafute utakapokuwa unapata pumziko"
Aaah mkuu umekitendea haki Kiswahili , lugha adhimu.
 
Kuna wakati mwengine hao wanaume nao ndio wanaanza wanakufanya uchefukwe na roho,mfano unaweza kukuta sms au mwanamke anakutumia sms kwenye cm yako na kukutukana au umefumani na sms ukimuliza anakwambia humfiki kwa lolote huyu mwanamke na wewe sinimekuo hiyo basi tuu,mwanamke utakua wewe? sasa hapo jamani mwanamke hakutolewa nyongo lazima akawambia na "na wewe sinakustahmilia tuu service mbovu hata huyo malkia anakulia pesa yako
lakini mbele huchezi nyuma hutisiki ebu nipishe mie kwenye wanaume nawewe unajiita mwanamme eeh? ebu nyamaza nikustiri babu weeeeeeeeeee.." lol
 
Kabisa...tena anakujibu kwa dharau na kiburi kiasi kwamba anampa kichwa hata yule mchepuko. Matokeo yake unadhalilika..
Hawaoni hilo. Kuna mwanaume mwingine ni mlevi mbwa kila akirudi ni matusi kwenda mbele..kipigo sasa balaa,anamdhalilisha Mkewe mpaka wazazi wa Mkewe. Lakini mama wa watu hatoacha kumtengea mumewe chakula wala haachi kumjali japo moyoni anasononeko.
 
Uzi huu umetonesha maumivu niliyoyashuhudia kwa mtu wangu wa karibu alipatwa na madhila kama haya
Wanawake (baadhi) roho zao ni zaidi yA paka
Paka ana roho nzuri sana. Ukimpigia mfano huo utakuwa hujatenda haki. Tuvumilieni na mtuhurumie,maana sisi ndo wake zenu,mama zenu na mabinti zenu,tafuteni njia nzuri ya kuamiliana na sisi.
 
Kabisa...tena anakujibu kwa dharau na kiburi kiasi kwamba anampa kichwa hata yule mchepuko. Matokeo yake unadhalilika..
Hawaoni hilo. Kuna mwanaume mwingine ni mlevi mbwa kila akirudi ni matusi kwenda mbele..kipigo sasa balaa,anamdhalilisha Mkewe mpaka wazazi wa Mkewe. Lakini mama wa watu hatoacha kumtengea mumewe chakula wala haachi kumjali
hahah Mwanamke ukimchokonoa utampa undani wake,sema wengine hawagombeleki nature yao wamezowea ugomvi..
 
Habari za wakati huu ndugu zangu.....natumaini sote tu wazima na baadhi waliopungukiwa uzima Mungu atawasaidia........

Kila mmoja wetu anafahamu ni jinsi gani ndoa zilivyojaa changamoto na mahangaiko mengi yanayozifanya ndoa kuwa ni muunganiko mgumu sana kuuingia......pengine wewe hapo msomaji unashughulikia moja ya changamoto hizo muda huu.....

Wakati mwingine mikiki mikiki ya ndoa hupelekea wanandoa kutofautiana kauli....utofauti unaowafanya wanandoa warushiane maneno.....na hapa ndipo hasa paliponifanya nitoe duku duku.....kwani hawa ndugu zetu sijui huwa wanakumbwa na ibilisi gani kwa muda huo kwani huwa hawachagui neno la kusema ilimradi tu liwe lenye kukuumiza wewe unayejibishana naye........

Ni maneno ambayo huamsha upya ugomvi na migogoro kila yakikumbukwa na yule aliyeambiwa....kwani ni mazito mmo na yanafedhehesha.....mfano; mwanamke anaweza akakuambia mbele ya kadamnasi kuwa..." Eti katika wanaume nawe ni mwanaume, umebakiwa kuvaa magauni tu" hii ni kauli mbaya sana na yenye kufedhehesha kama sio kudhalilisha...... Utasikia " kwanza hawa watoto sio wa kwako".........hizi ni baadhi ya kauli zinazolisha mengine kwani ni wanaume wachache wenye uwezo wa kuhimili kuziacha hizi kauli zipite hivi hivi ingawa zinachoma kama mtu aliyemeza kaa la moto......

Ndio maana matukio ya kuuwawa wanawake kinyama yanashamiri kila uchao....wanawake wanaopata ulemavu kutokana na vipigo vya waume zao wanaongezeka kila uchao.....ukichunguza kwa makini chanzo ni kauli mbovu za wanawake.......sio kwamba naunga mkono matukio ya ukatili wa kijinsia la hasha bali nawaasa wakina mama wawe makini na kila wakitoacho mdomoni mwao.....kwani bila ya kujua huleta matokeo mabaya sana.....kwani si kila mtu ana uwezo wa kustahimili kauli za kizalilishaji kama hizo.....kuna wale wanaume mashujaa wanaoweza kufunika kombe ili mwanaharamu apite na kuna baadhi wanaoonyesha hasira zao....hapo ndipo matokeo ya kauli chafu yanavyoonekana..........

N;B
WANAMUME WENZANGU TUJITAHIDI KUWA WASTAHILIMILIVU KATIKA NDOA KWANI KWA KUISHI NA MWANAMKE NI MTIHANI MKUBWA AMBAO MUNGU AMETUPA.......

Inapotokea umepishana kauli na mkeo usikae eneo.....ondoka uende mbali na eneo hilo lakini usiende bar kunywa pombe......

Mkuu unatonesha madonda yalioisha anza kupona hawa watu acha kabisa
 
Jamani hata wanawake ni wastahamilivu tena sana,tuna mengi sana ya kwenu tunayabeba..tunaficha aibu zenu mno. Ukikuta mwanamke ameongea kauli ya 'udhalilishaji' pengine ni tabia yake kuropoka au amechoka na mambo yako ambayo yamekuwa yakijirudia...ama kweli mavi anye kuku akinya bata kahara jamani.

Nadhani hujaelewa msingi wa mada....si kwamba wanawake wanalaumiwa la hasha bali wanashauriwa kuwa breki kwenye midomo yao.....kuna baadhi ya kauli zinaweza kukusababishia mabalaa kwani zinachoma mno....chungeni midomo yenu.....
 
Kuna wakati mwengine hao wanaume nao ndio wanaanza wanakufanya uchefukwe na roho,mfano unaweza kukuta sms au mwanamke anakutumia sms kwenye cm yako na kukutukana au umefumani na sms ukimuliza anakwambia humfiki kwa lolote huyu mwanamke na wewe sinimekuo hiyo basi tuu,mwanamke utakua wewe? sasa hapo jamani mwanamke hakutolewa nyongo lazima akawambia na "na wewe sinakustahmilia tuu service mbovu hata huyo malkia anakulia pesa yako
lakini mbele huchezi nyuma hutisiki ebu nipishe mie kwenye wanaume nawewe unajiita mwanamme eeh? ebu nyamaza nikustiri babu weeeeeeeeeee.." lol

Mpwa kwa jinsi ulivyoyatamka kwa ustadi hayo maneno inaonyesha...una uzoefu kwenye kuyatumia mara kwa mara....hongera....
 
Back
Top Bottom