sexologist
JF-Expert Member
- Dec 5, 2010
- 2,276
- 976
Unakuta unaingia sehemu ya starehe, unamkuta mshkaji wako amekaa na manzi wake, kwa kuwa mna ukaribu unaamua kusogea na kwenda kumsalimia.. Kama kawaida yetu watanzania unamsalimia kwa sauti na kwa kumshika mkono. Sasa baada ya hapo unaamua kumsalimia hivyo hivyo mrembo aliyekaa nae.. Dada anaitikia kwa dharau na kwa sauti ya chini, kwa kuwa umehisi ni shemeji unaamua kumpa na mkono kama heshima.. Demu anaangalia pembeni..
Mshkaji kwa aibu anakutambulisha, e bwana kiongozi huyu ndo shemeji yako anaitwa Sophy.. Na we unaitikia kwa kutikisa kichwa.. Mara jamaa na ye anakutambulisha, bebi huyu anaitwa Johnson ndio boss wangu, hata ile gari niliokwambia ndio muheshimiwa alisema angeniazima twende nayo Njombe, maana haka ketu si unajua na barabara..
Kusikia hivyo mdada anaona aibu, anasema ok shem nashukuru kwa kukufahamu.. kaa tujumuike pamoja.. ila shem we ni mpambanaji sana, bebi amenihadithia kuhusu wewe.. Na mi unipe hata kazi ya kukufagilia ofisi...
Dada amechanganyikiwa kusikia jamaa ndio bosi wa bebi wake na sifa kede kede alizosikia, sasa ndo anajishaua..
Wadada acheni tabia hii.. Ni ujumbe kwa baadhi yenu..
Hii imetokea kweli nikiwa karibu na hao wahusika meza jirani tarehe 01/01/2015..!!!