Wakimbizi 20 wa Burundi wafariki kigoma

Wakimbizi 20 wa Burundi wafariki kigoma

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,571
Reaction score
53,586
wakimbizi-burundi-559x520.jpg

Ugonjwa wa kuhara umeingia kwenye baadhi ya kambi za wakimbizi huko mkoani kigoma na kusababisha vifo vya watu saba huku wengine wakiwa kwenye hali mbaya.

Wakimbizi hao ni wale wanaotokea nchini Burundi, ambao wameingia kwenye kambi hizo kutokana na madhara ya fujo na vurugu zilizosababishwa na maandamano ya kumpinga rais Pierre Nkurunzinza ili asigombee tena kiti cha urais kwa awamu ya tatu.

Tayari Shirika la kuhudumia la wakimbizi UNHCR limesema watahakikisha watashirikiana kwa ukaribu zaidi na serikali ya Tanzania kuhakikisha wagonjwa wengine wanapona na pia kuthibiti kabisa ugonjwa huo usiendelee kusambaa na kupotea kabisa.

Tangu kutokeee maandamano nchini Burundi trayari maelfu ya raia wan chi hiyo wameikimbia nchi yao na kuelekea nchi za jirani kama Tanzania, Rwanda, Kongo na Uganda ili kutafuta hifadhi.
Wakimbizi wa Burundi wafariki Kigoma
 
Weka picha ya waliokufa, WEWE mukenya wewe unapenda habari kama hizi lol.
 
Jamani Nkurunzinza kwani asipongombea tena atakufa au?miaka kumi yote hajatosheka kula misaada kutoka USA,UBELGIJI NA EU?Poleni sana warundi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Viongozi wa Afrika wengi ndio wako hivyo. Tamaa ya madaraka na woga wa matendo yao ya kinyama walipkuwa madarakani mara nyingi huwafanya watake kung'ang'ania madaraka milele ili kuedelea kuficha madhambi yao na kuendeleza unyama wao ikiwemo wizi na ufisadi wa hali ya juu. Ndio sababu wengi tulimpongeza sana yule Jonathan kule Nigeria kuondoka madarakani kwa amani bila kuleta vurumai ya aina yoyote na hivyo kukabidhi madaraka kwa njia ya amani. Hili hata kwetu haliwezi kutokea kwa sababu pale MACCM watakaposhindwa kamwe hawawezi kuachia madaraka kwa amani ndio sababu tumeshaanza kusikia kauli za kidhalimu na zilizojaa ufedhuli wa hali juu kwamba, "Hatuwezi kukabidhi madaraka kwa wahuni" Sasa kama upinzani ni wahuni imekuwaje katika nchi ambayo wahuni hawatakiwi wakaachiwa kuunda vyama vyao vya kihuni miaka yote hii na kuruhusiwa kuwepo Bungeni na wakati mwingine hata kukaribishwa Ikulu na kusafiri nchi za nje na Viongozi mbali mbali wa Serikali, lakini ikija kwenye kukabidhiwa madaraka MACCM wanakuja juu na kung'aka hawa wahuni hatuwezi kuwakabidhi madaraka!

Jamani Nkurunzinza kwani asipongombea tena atakufa au?miaka kumi yote hajatosheka kula misaada kutoka USA,UBELGIJI NA EU?Poleni sana warundi
 
Duh!! kwani wewe ni dracula ama vampire, mapicha ya maiti unataka ya nini.
Yaani huyu Nkurunzinza anakera kishenzi.

We MK254 kwani kuangalia maiti hadi uwe vampire????????

Tatizo sio Nkurunzinza mimi naona tatizo ni walio mchagua ndio walioanzisha vurugu. sipendi hii mambo inatutesa wamama na watoto.
 
Last edited by a moderator:

Nimtrhani mungu awa poke ningependa watanzania tuwasaidie
 
Huruma lakini!,.....hivi huyu Nkuruwhatever anavo lazimisha akiona hivi sijui anasikiaje!

Hehehe!! hata mimi huwa na matatizo ya kulitamka hilo jina lake.
King'ang'anizi balaa...
 
  • Thanks
Reactions: kui
Hivi hawajifunzi nao kuanzisha anzisha mavurugu? Kwani akiwa PN au asipokua huyo wao wanafaidika kipi?
Hizi vita za kisiasa ni kutumiwa tu na wanaotaka madaraka.
 
Hivi hawajifunzi nao kuanzisha anzisha mavurugu? Kwani akiwa PN au asipokua huyo wao wanafaidika kipi?
Hizi vita za kisiasa ni kutumiwa tu na wanaotaka madaraka.

Da Pretty;
Ulikuwa unawaza au? Wao watafaidika nini!!! Mawazo ka yako ndo yametufikisha hapa tulipo. Tunajiwazisha kuwa; Nipige kura au nisipige kwani kuna tofauti gani??
Maandamano yao ni muhimu. Badala ya kukimbilia Tz na kuja kufa kwa Kipindupindu angetoka akaenda kumpinga NKuruwhatever ingekuwa ni bora zaidi. Mtu unakimbia nchi yako unayaachia manyang'au yairarue, No No man, I will fight tooth and nails mpaka kieleweke.
Maandamano sio kwa ajili ya wanasiasa ni kwa ajili ya kuwaambia hao wanasiasa zao kuwa wasituone mabwege tuko macho
 
Duh! wewe ni mtu muhimu sana Afrika hii.
 
Niliposikia Burundi ni ya pili kwa umasikini duniani nilichoka...sa jamaa anang'ang'ania nini?????
Napata mashaka hata hawa wakimbizi kama kweli wanakimibia vita (maana) haijakolea..isije kuwa wanakimbia umasikini...hopping tutawapa uraia siku za usoni...
 
hata wewe mama kweli? unakuwa kama haujazaa! yani unafikiria kweli eti labda wamekimbia njaa? kusudi waje kufa kwa kipindupindu ktokana na uchafu na matibabu duni yaliyopo Tanzania? nakuhakikishia kuna wengi ambao ni majasiri, wenyewe wamedindisha mpaka kieleweke(ama Nkurunziza ama wao) kuliko kuja kufa kwa uchafu... shukuru Mungu haujawahi kuwa mkimbizi tena na enyewe ni kutokana na uwoga wenu tu lakini kiukweli hata kwenu mambo yanaenda kushoto tena sana... ukweli mnaujuwa sema ndio hivyo mlishaamua kukenuliana milele na kubakia mkicheka warundi kwa ujasili wao wa kupambana na adui wao wa maendeleo... game mtakuja kulishtukia too late.
 
Acha kabisa kutukana Tz wewe!....hapa ndio kunaitwa mtakuja..iwe kwa njaa au kwa kukimbia kuchinjana na roho zenu MBAYA!!!

Back
Top Bottom