Wakili: 'Mke' wa Dk. Slaa mjamzito

Wakili: 'Mke' wa Dk. Slaa mjamzito

Imeandikwa na John Mhala, Arusha; Tarehe: 29th April 2011 @ 23:57 Imesomwa na watu: 954; Jumla ya maoni: 0

KESI inayowakabili viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wafuasi wao, jana ilishindwa kuendelea baada ya kutokea mvutano wa kisheria wa kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo ama kutosikilizwa kutokana na baadhi ya washitakiwa kutokuwepo mahakamani hapo.

Miongoni mwa waliokosekana mahakamani hapo ni Josephine Mushumbusi Slaa, `mke’ wa sasa wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa aliyeibuka naye na kuzunguka naye karibu nchi nzima wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Vuta nikuvute ya vifungu vya kisheria iliibuka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Arusha, baada ya upande wa mashitaka kutaka kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake 18 kuahirishwa huku upande wa utetezi ukitaka kesi hiyo ianze kusikilizwa maelezo ya awali.

Kutokana na utata huo wa kisheria ilifanya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kukwama kusikiliza maelezo ya awali baada ya Hakimu Mfawidhi wa Mkoa wa Arusha, Charles Magesa kukubaliana na hoja za upande wa mashitaka kuwa isingekuwa vema kwa mahakama kuendelea kusikiliza maelezo ya awali wakati baadhi ya watuhumiwa hawakuwepo mahakamani hapo.

Mvutano huo ulidumu kwa saa mbili ambapo hakimu Magesa aliahirisha kwa muda ili kuweza kutoa maamuzi ya mabishano hayo na aliporejea tena na kusoma uamuzi wa utata uliokuwepo.

Kukwama huko kulikuja baada ya jopo la mawakili wa upande wa mashitaka likiongozwa na Rehema Ringo, kuiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe nyingine itakayopangwa baada ya baadhi ya watuhumiwa kushindwa kufika mahakamani hapo.

Mawakili wengine wa upande wa mashitaka ni Awamu Mbagwa na Mwahija Ahmed.

Mapema Hakimu Magesa, aliwaita kwa majina watuhumiwa wote na ndipo ilipobainika kuwa wanne kati yao hawakuwepo.

Wakili wa upande wa utetezi, Method Kimomogolo aliieleza mahakama kuwa, mtuhumiwa namba nane Josephine Slaa ni mgonjwa na ametakiwa daktari wake kupumzika, wakati watuhumiwa Samson Mwigamba na Dadi Igogo walipitia hospitali kupata matibabu na walikuwa njiani kufika mahakamani hapo.

Akifafanua zaidi, wakili Albert Msando aliieleza baadaye mahakama kuwa Josephine ni mjamzito na ametakiwa na daktari wake kupumzika.

Mtuhumiwa mwingine namba 16, Mathias Valerian, hakuwa na maelezo yoyote ya kutokuwepo kwake.

Awali Ringo alitaka mahakama itoe hati ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kufikishwa mahakamani, kwa kile alichoeleza kuwa baadhi yao hawakuwa na sababu za msingi za kutohudhuria mahakamani.

Akiunga mkono hoja ya kuahirisha, wakili mmoja wa upande wa mashtaka, Awamu Mbagwa, alisema kwa mujibu wa kifungu cha 192(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinataka watuhumiwa wote kuwepo mahakamani kabla ya kusomewa maelezo ya awali.

Alisema sharti hilo ni muhimu kwa kuwa watuhumiwa wanatakiwa kukubali au kukataa maelezo hayo na kisha kusaini.

Hata hivyo, wakili mwingine wa utetezi, Msando, alipinga hoja hizo kwa kusema kuwa kifungu hicho cha sheria kimefanyiwa marekebisho mwaka 1992, ambapo pamoja na ulazima huo pia kinaruhusu kuendelea kusikilizwa kwa maelezo ya awali iwapo mtuhumiwa anaye mtu wa kumwakilisha kama wakili.

Alisema , lengo la marekebisho hayo ni kutaka kesi iendelee kusikilizwa bila kuahirishwa pasipokuwa na sababu za msingi.

“Kifungu hicho kilikwisharekebishwa na sasa kinaruhusu mahakama kuendelea kuchukua maelezo ya awali kwa kuwa watuhumiwa ambapo wameshindwa kufika mahakamani wanawakilishwa na mawakili,” alidai.

Alidai pia kuwa kutokana na idadi kubwa ya watuhumiwa walifika mahakamani hapo ni sababu nyingine ambayo inaweza kuishawishi mahakama kuendelea kusikiliza maelezo ya awali.

Wakati mabishano hayo yakiendelea, wakili kiongozi wa upande wa utetezi, Kimomogolo, aliitaarifu mahakama kuwa watuhumiwa Mwigamba na Igogo walikuwa wameshafika mahakamani hapo kuungana na wenzao.

Akiendelea kutoa ushawishi wa mahakama kutoahirisha kesi hiyo, Msando alisema uamuzi wa kuendelea kusikilizwa kwa kesi katika hatua hiyo ya maelezo ya awali bila ya kuwepo kwa watuhumiwa wote mahakamani, ulikwishatolewa katika moja ya kesi ya rufani ya Ephraim Mtambi dhidi ya Jamhuri iliyosikilizwa na Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya mwaka 1996.

Hata hivyo, Msando alisema uwepo wa mshtakiwa katika usikilizaji wa maelezo ya awali ni lazima kwa kuwa mshtakiwa mwenyewe ndiye anayepaswa kuieleza mahakama ni maelezo gani anayokubali na yapi anayoyakataa.

“Lakini kwa kuwa mahakama moja ya shughuli zake ni kutafsiri sheria, hivyo katika kesi hiyo ilikwishafanya hivyo,” alisema.

Kufikia hatua hiyo, Hakimu Magesa alilazimika kuahirisha kesi kwa muda ili mahakama ikajipange kutoa uamuzi wa msuguano huo wa kisheria.

Aliahirisha kesi kuanzia saa 3:56 hadi 5:07 alipoingia tena na kusoma uamuzi ambapo alisema mahakama haikubaliani na hoja iliyotolewa na Msando.

Alisisitiza kuwa uwepo wa mtuhumiwa katika kusikiliza maelezo ya awali ni lazima kutokana na umuhiwa wa yeye kutamka iwapo anakubali au la na aweze kusaini kwenye hati hiyo ya maelezo.

Alitaja mfano wa kesi ya MT 7479 Benjamin Holela, kuwa pale maelezo ya awali yanaposomwa, mtuhumiwa lazima awepo mahakamani.

Hivyo, Hakimu Magesa alikubaliana na upande wa mashitaka kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe nyingine na baada ya kuwasiliana na pande mbili za utetezi na mashitaka walikubaliana kuwa kesi hiyo itajwe Mei 27, mwaka huu, na kwamba siku hiyo ndipo itakapopangwa tarehe ya kuanza kusikiliza maelezo ya awali.

Wakili Kimomogolo aliwaombea udhuru wa kutofika tarehe hiyo kwa watuhumiwa ambao ni wabunge kwa kuwa watakuwa kwenye vikao vya Kamati za Bunge.

Kabla ya kuahirisha, Hakimu Magesa aliwaonya watuhumiwa ambao hawatafika mahakamani kuwa wanaweza kunyang’anywa udhamini na hivyo kuwekwa ndani hadi kesi hiyo itakapomalizika.

Mapema Januari mwaka huu, viongozi wa Chadema wanadaiwa kufanya maandamano ambayo hayakuruhusiwa na polisi, na hivyo kusababisha vurugu kubwa iliyopelekea polisi kuua watu watatu.

Ilidaiwa kuwa maandamano hayo yalipangwa kwa lengo la kupinga kuchaguliwa kwa Meya wa Jiji la Arusha katika uchaguzi ambao awali Chadema walisusia, lakini wenzao wa Chama Cha Mpinduzi (CCM) na TLP waliufanya na kumchagua Gaudence Lyimo wa CCM.

HTML:
Wakili: 'Mke' wa Dk. Slaa mjamzito

Hivi Habari Leo wanapomwita mke wa Dr. Slaa" kwenye mabano wanamaanisha ya kuwa kuna utata wao yanawahusu nini?
 
Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Willbroad Slaa (pichani), sasa anatarajia kupata mtoto baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kujulishwa kuwa mchumba wake, Josephine Mushumbusi ni mjamzito.

Aminiel Mahimbo ambaye anadai kuwa Josephine ni mkewe alimfungulia kesi ya madai Dk. Slaa na kuitaka mahakama kumzuia kufanya naye tendo la ndoa.

Tangu atoe madai hayo mahakamani sasa ni miezi nane imepita, hali inayotafsiriwa na wataalamu wa mambo ya uzazi kuwa, inawezekana wakati anatoa ombi hilo tayari Josephine alikuwa mjamzito.

Kesi hiyo ya Mahimbo ambayo ilivuta macho na masikio ya Watanzania wengi ilinguruma Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana ambapo Dk. Slaa alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema.
http://api.ning.com/files/K1Ds2dG05...*GYPWSNuvyWieuPatAZywwCB6BDt83l*E/DkSlaa2.jpg
Haijajulikana Mahimbo ataamua nini baada ya habari hiyo ya ujauzito kusambaa. Gazeti hili lilimtafuta mwishoni mwa wiki iliyopita bila mafanikio na liliambiwa kuwa, sehemu ambayo alikuwa akiishi, Victoria, Kijitonyama amehama siku nyingi na simu yake ya kiganjani ilipokuwa ikipigwa ilikuwa haipatikani.

Katika kesi inayowakabili viongozi na wafuasi 19 wa Chadema jijini Arusha, Josephine na Dk. Slaa wakiwemo, pamoja na mambo mengine wanatuhumiwa kufanya mkutano usio halali na kuendesha vitendo vya kichochezi, madai ambayo wameyakanusha. Walifunguliwa mashitaka hayo Januari 5 mwaka huu.

Alikuwa ni wakili wa upande wa utetezi, Method Kimomogolo aliyeiarifu Mahakama ya Arusha mbele ya Hakimu Mkazi, Charles Magesa Ijumaa ya wiki iliyopita kuwa, mteja wake Josephine amepewa ruhusa ya kupumzika na madaktari kutokana na ujauzito wa miezi nane na wiki tatu alionao.

“Mheshimiwa, Josephine amepewa ruhusa na daktari wake kupumzika kutokana na kuwa na ujauzito wa miezi nane na wiki tatu,” alisema Wakili Kimomogolo na kufanya umati wa watu waliokuwa mahakamani humo kunong’ona.

Hata hivyo, Hakimu Magesa alisita kukubaliana na maelezo ya wakili na ndipo aliposema: “Tunaomba vyeti vya daktari, si taarifa ya mdomo, mahakama itajiaminisha vipi katika hili?”

Wakili wa Josephine hakukosa jibu, aliiambia mahakama kuwa daktari wa Josephine hakuwepo na yeye ndiye anayehusika na uandikishaji wa ruhusa yake, jibu ambalo Hakimu Magesa alimkumbusha mtetezi huyo kuwa alikuwa akijua kuwa wana kesi siku hiyo na alishangaa kwa nini hawakuiandaa taarifa hiyo mapema.

Hakimu Magesa alisema kuwa, ili kesi hiyo iweze kuendelea na hatua ya usikilizwaji wa awali ni lazima watuhumiwa wote wawepo mahakamani kwani kuendelea bila baadhi yao kuwepo kutasababisha siku wakija awasomee tena maelezo hayo ili wakubali au wakatae, hivyo aliahirisha shauri hilo hadi Mei 27, mwaka huu.

Nukuu : Slaa amekiuka amri ya mahakama, asizae na huyu mwanamke mpaka kesi ya msingi itakapo kwisha
 
mahakama gani ili amuru hivo?
acha ushambenga wewe zaa nae sasa,...we vipi?
 
Kwa wazungu "all male relatives" wanaitwa "Uncle" hivyo Mahimbo ajiandae kuitwa Uncle na hicho kiumbe kitakachozaliwa
 
Nimesikia kwenye taarifa ya habari itv kwamba sababu iliyomfanya bi. Josephine Mushumbusi (mchumba / mke wa Dr. Slaa) ashindwe kutinga kortini ni kwamba ni mjamzito so ana maternity leave.

Napenda kumpongeza dr. Slaa na bi. Josephine na mungu awabariki mpate baby ambaye ni kichwa kama baba ake.

Nadhani baada ya hapa lile jina la "mchumba" litakuwa limezikwa rasmi.

Duh, hivi hili nalo ni la kumpa mtu pongezi? watoto na vijana wet wanajifunza nn kwenye hili ? halafu baadae tuseme taifa halina maadili kumbe wazee kama wakina Slaa ambao wanatakiwa wafunze maadili , ndio wao wa kwanza kuvunja maadili. Hili taifa linahitaji maombezi maalum kama padri km Slaa anaweza fanya hivi
 
Huu ni ujumbe kwa wanajamvi wote kwamba maisha hayapoka katika dimension zote. Maisha ni pamoja na familia iliyokamilika. Vijana ili muwe viongozi bora zaidi wasiokuwa na presha ni vema mukaoa. Mama Josephine nakutakia kila lakheri na mungu akubariki sana.
 
Duh, hivi hili nalo ni la kumpa mtu pongezi? watoto na vijana wet wanajifunza nn kwenye hili ? halafu baadae tuseme taifa halina maadili kumbe wazee kama wakina Slaa ambao wanatakiwa wafunze maadili , ndio wao wa kwanza kuvunja maadili. Hili taifa linahitaji maombezi maalum kama padri km Slaa anaweza fanya hivi

Kumbe ulifikiri unamshitaki jamvini lakini imekuwa tofauti na unashangaa kweli. Afadhari umesema msimamo na malengo ya kuleta hii thread hapa. Kwa taarifa yako watoto ni baraka katika familia na jamii kwa ujumla.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom