Wakili: 'Mke' wa Dk. Slaa mjamzito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakili: 'Mke' wa Dk. Slaa mjamzito

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Chloe O'brian, Apr 29, 2011.

 1. Chloe O'brian

  Chloe O'brian Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesikia kwenye taarifa ya habari itv kwamba sababu iliyomfanya bi. Josephine Mushumbusi (mchumba / mke wa Dr. Slaa) ashindwe kutinga kortini ni kwamba ni mjamzito so ana maternity leave.

  Napenda kumpongeza dr. Slaa na bi. Josephine na mungu awabariki mpate baby ambaye ni kichwa kama baba ake.

  Nadhani baada ya hapa lile jina la "mchumba" litakuwa limezikwa rasmi.
   
 2. THE GEEK

  THE GEEK Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mmmmh.. Mungu???
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  hahaaaa..source plzeeeeeee!! coz mi nilisikia amehongwa na ndio maana hakuja,sosi yangu ni JF..!!
   
 4. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  si kasema itv au source gani unaitaka hapo.
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Mungu akamjaze rehema mama huyu wa rais wetu
   
 6. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Naomba kuuliza jamani, hivi Dr. Wetu wa ukweli hana watoto na mke mkubwa? Au Mungu kamjalia mtoto kama Abrahamu kwenye bible?
   
 7. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kweli cdm ni makamanda wa ukweli km wazee wanauwezo wa kutengeneza babyz vijana wao c balaa teh teh wakikudunga lzm mapacha LOL
   
 8. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Kuwa makini sana kila post uionayo jf, usisome kama gazeti la udaku! Kashasema atv!!!
   
 9. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ndo walewale na unga mkono hoja we subiri tu jombaaaa wako wengi hao..
   
 10. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio uanaume huo unapanda mbegu zinazaa matunda,mwanachama mpyaa huyoooo!! Anakuja.
   
 11. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2011
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  huyu mzee si anamiaka zaidi ya 60. sasa hivi ale pensheni tu na mke mambo ya kulea watoto muda wake ulishapita hahahahahha
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,519
  Likes Received: 19,940
  Trophy Points: 280
  mbona mkulu ana wake wanne na watoto hatuulizi
   
 13. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  KESI inayowakabili viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wafuasi wao, jana ilishindwa kuendelea baada ya kutokea mvutano wa kisheria wa kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo ama kutosikilizwa kutokana na baadhi ya washitakiwa kutokuwepo mahakamani hapo.

  Miongoni mwa waliokosekana mahakamani hapo ni Josephine Mushumbusi Slaa, `mke’ wa sasa wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa aliyeibuka naye na kuzunguka naye karibu nchi nzima wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

  Vuta nikuvute ya vifungu vya kisheria iliibuka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Arusha, baada ya upande wa mashitaka kutaka kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake 18 kuahirishwa huku upande wa utetezi ukitaka kesi hiyo ianze kusikilizwa maelezo ya awali.

  Kutokana na utata huo wa kisheria ilifanya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kukwama kusikiliza maelezo ya awali baada ya Hakimu Mfawidhi wa Mkoa wa Arusha, Charles Magesa kukubaliana na hoja za upande wa mashitaka kuwa isingekuwa vema kwa mahakama kuendelea kusikiliza maelezo ya awali wakati baadhi ya watuhumiwa hawakuwepo mahakamani hapo.

  Mvutano huo ulidumu kwa saa mbili ambapo hakimu Magesa aliahirisha kwa muda ili kuweza kutoa maamuzi ya mabishano hayo na aliporejea tena na kusoma uamuzi wa utata uliokuwepo.

  Kukwama huko kulikuja baada ya jopo la mawakili wa upande wa mashitaka likiongozwa na Rehema Ringo, kuiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe nyingine itakayopangwa baada ya baadhi ya watuhumiwa kushindwa kufika mahakamani hapo.

  Mawakili wengine wa upande wa mashitaka ni Awamu Mbagwa na Mwahija Ahmed.
  Mapema Hakimu Magesa, aliwaita kwa majina watuhumiwa wote na ndipo ilipobainika kuwa wanne kati yao hawakuwepo.

  Wakili wa upande wa utetezi, Method Kimomogolo aliieleza mahakama kuwa, mtuhumiwa namba nane Josephine Slaa ni mgonjwa na ametakiwa daktari wake kupumzika, wakati watuhumiwa Samson Mwigamba na Dadi Igogo walipitia hospitali kupata matibabu na walikuwa njiani kufika mahakamani hapo.

  Akifafanua zaidi, wakili Albert Msando aliieleza baadaye mahakama kuwa Josephine ni mjamzito na ametakiwa na daktari wake kupumzika.

  Mtuhumiwa mwingine namba 16, Mathias Valerian, hakuwa na maelezo yoyote ya kutokuwepo kwake.

  Awali Ringo alitaka mahakama itoe hati ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kufikishwa mahakamani, kwa kile alichoeleza kuwa baadhi yao hawakuwa na sababu za msingi za kutohudhuria mahakamani.

  Akiunga mkono hoja ya kuahirisha, wakili mmoja wa upande wa mashtaka, Awamu Mbagwa, alisema kwa mujibu wa kifungu cha 192(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinataka watuhumiwa wote kuwepo mahakamani kabla ya kusomewa maelezo ya awali.
  Alisema sharti hilo ni muhimu kwa kuwa watuhumiwa wanatakiwa kukubali au kukataa maelezo hayo na kisha kusaini.

  Hata hivyo, wakili mwingine wa utetezi, Msando, alipinga hoja hizo kwa kusema kuwa kifungu hicho cha sheria kimefanyiwa marekebisho mwaka 1992, ambapo pamoja na ulazima huo pia kinaruhusu kuendelea kusikilizwa kwa maelezo ya awali iwapo mtuhumiwa anaye mtu wa kumwakilisha kama wakili.

  Alisema , lengo la marekebisho hayo ni kutaka kesi iendelee kusikilizwa bila kuahirishwa pasipokuwa na sababu za msingi.

  “Kifungu hicho kilikwisharekebishwa na sasa kinaruhusu mahakama kuendelea kuchukua maelezo ya awali kwa kuwa watuhumiwa ambapo wameshindwa kufika mahakamani wanawakilishwa na mawakili,” alidai.

  Alidai pia kuwa kutokana na idadi kubwa ya watuhumiwa walifika mahakamani hapo ni sababu nyingine ambayo inaweza kuishawishi mahakama kuendelea kusikiliza maelezo ya awali.

  Wakati mabishano hayo yakiendelea, wakili kiongozi wa upande wa utetezi, Kimomogolo, aliitaarifu mahakama kuwa watuhumiwa Mwigamba na Igogo walikuwa wameshafika mahakamani hapo kuungana na wenzao.

  Akiendelea kutoa ushawishi wa mahakama kutoahirisha kesi hiyo, Msando alisema uamuzi wa kuendelea kusikilizwa kwa kesi katika hatua hiyo ya maelezo ya awali bila ya kuwepo kwa watuhumiwa wote mahakamani, ulikwishatolewa katika moja ya kesi ya rufani ya Ephraim Mtambi dhidi ya Jamhuri iliyosikilizwa na Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya mwaka 1996.

  Hata hivyo, Msando alisema uwepo wa mshtakiwa katika usikilizaji wa maelezo ya awali ni lazima kwa kuwa mshtakiwa mwenyewe ndiye anayepaswa kuieleza mahakama ni maelezo gani anayokubali na yapi anayoyakataa.

  “Lakini kwa kuwa mahakama moja ya shughuli zake ni kutafsiri sheria, hivyo katika kesi hiyo ilikwishafanya hivyo,” alisema.

  Kufikia hatua hiyo, Hakimu Magesa alilazimika kuahirisha kesi kwa muda ili mahakama ikajipange kutoa uamuzi wa msuguano huo wa kisheria.

  Aliahirisha kesi kuanzia saa 3:56 hadi 5:07 alipoingia tena na kusoma uamuzi ambapo alisema mahakama haikubaliani na hoja iliyotolewa na Msando.

  Alisisitiza kuwa uwepo wa mtuhumiwa katika kusikiliza maelezo ya awali ni lazima kutokana na umuhiwa wa yeye kutamka iwapo anakubali au la na aweze kusaini kwenye hati hiyo ya maelezo.

  Alitaja mfano wa kesi ya MT 7479 Benjamin Holela, kuwa pale maelezo ya awali yanaposomwa, mtuhumiwa lazima awepo mahakamani.

  Hivyo, Hakimu Magesa alikubaliana na upande wa mashitaka kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe nyingine na baada ya kuwasiliana na pande mbili za utetezi na mashitaka walikubaliana kuwa kesi hiyo itajwe Mei 27, mwaka huu, na kwamba siku hiyo ndipo itakapopangwa tarehe ya kuanza kusikiliza maelezo ya awali.

  Wakili Kimomogolo aliwaombea udhuru wa kutofika tarehe hiyo kwa watuhumiwa ambao ni wabunge kwa kuwa watakuwa kwenye vikao vya Kamati za Bunge.

  Kabla ya kuahirisha, Hakimu Magesa aliwaonya watuhumiwa ambao hawatafika mahakamani kuwa wanaweza kunyang’anywa udhamini na hivyo kuwekwa ndani hadi kesi hiyo itakapomalizika.

  Mapema Januari mwaka huu, viongozi wa Chadema wanadaiwa kufanya maandamano ambayo hayakuruhusiwa na polisi, na hivyo kusababisha vurugu kubwa iliyopelekea polisi kuua watu watatu.

  Ilidaiwa kuwa maandamano hayo yalipangwa kwa lengo la kupinga kuchaguliwa kwa Meya wa Jiji la Arusha katika uchaguzi ambao awali Chadema walisusia, lakini wenzao wa Chama Cha Mpinduzi (CCM) na TLP waliufanya na kumchagua Gaudence Lyimo wa CCM.

  Source: Gazeti la Habari Leo, Aprili 30, 2011
   
 14. b

  batamaji Member

  #14
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 5, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Josephine Mushumbusi Slaa, `mke’ wa sasa wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa aliyeibuka naye na kuzunguka naye karibu nchi nzima wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu hivi sasa ni mjamzito refer habari leo.
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu hivi gazeti la serekali kazi yake inapofanana na magazeti ya udaku unajisikiaje.Nilitegemea habari ya aina hii kuikuta kwenye magazeti ya Uwazi,Ijumaa na nk ?.
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hongera Josephine, mtoto ni zawadi toka kwa Mungu, wengi sana humu duniani wanafikia hata kukufuru Mungu kwa kukosa mtoto... omba upate afya bora zaidi na ujifungue salama. Akizaliwa mtoto mlee kimaadili zaidi na umlinde pamoja na baba wa mtoto

  MUNGU NI MWEMA
   
 17. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Pongezi za pekee kwa Josephine na Dr. najua wote ni members humu JF na mtazipata pongezi hizi.....
   
 18. only83

  only83 JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ................All the best Dr and your wife,God be with you..
   
 19. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #19
  May 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  sina uhakika
  lakini nilisikia anawatoto wawili
  wanaishi nchi za nje ...
  walizaliwa sehehmu moja inaitwa Basutu


  ps. sintojibu swali zaidi..
   
 20. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hongera Dr. Slaa kwa kazi inayofanana na jina langu.
   
Loading...