Wakili maarufu mbaroni kwa rushwa

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Taarifa za hivi punde ni kuwa wakili maarufu wa kujitegemea katika mikoa ya kanda ya ziwa Bw Aaron Kabunga amekamtwa na Takukuru akiwa katika harakatib za kuwahonga mashahidi katika kesi ya ufisadi inayowakabili watumisi 10 wa Halmasjhauri ya wilaya ya Karagwe mkoani kagera.

taarifa kutoka mkoani kagera ni kuwa kabunga ambaye ni tajiri mkubwa wa mahotel alikuwa akiwatetea watumishi hao na ilipangwa leo kuanza usikilizaji kwa mashahidi kuto Ushadi wao lakini Takukuru walipata taarifa za Kabunga kukutana na mashahdfi hao pamoja na mtuhumiwa mmoja ambaye ni afisa elimu wa wilaya hiyo.

walibambwa wakiwa katika hotel ya Clasic katika chumba namba 27 wote wamekamtwa,hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo bw magana amejitoa

kabunga,mashahidi,na mtuhumiwa bado wako lupango karagwe,kesi imepigwa kalenda

watumishi wanatuhumiwa kutafuna zaidi ya sh milioni 30 za halmshauti hiyo
 
Kazi nzuri...ila tu mbona mnachagua kazi...au zile zingine hazina ushahidi?
 
Wala asiwe na wasi wasi, Tanzania magereza yapo kwa ajili ya wanyonge. Kama yeye anamiliki mahoteli n.k, magereza sio mahali pake, labda kupitia tu ili mwanaharamu afunike kombe.
 
hakuna kitu hapo ni siasa tu, wanataka kumharibia kazi huyu wakili, PCCB washenzi sana.
 
Taarifa za hivi punde ni kuwa wakili maarufu wa kujitegemea katika mikoa ya kanda ya ziwa Bw Aaron Kabunga amekamtwa na Takukuru akiwa katika harakatib za kuwahonga mashahidi katika kesi ya ufisadi inayowakabili watumisi 10 wa Halmasjhauri ya wilaya ya Karagwe mkoani kagera.

taarifa kutoka mkoani kagera ni kuwa kabunga ambaye ni tajiri mkubwa wa mahotel alikuwa akiwatetea watumishi hao na ilipangwa leo kuanza usikilizaji kwa mashahidi kuto Ushadi wao lakini Takukuru walipata taarifa za Kabunga kukutana na mashahdfi hao pamoja na mtuhumiwa mmoja ambaye ni afisa elimu wa wilaya hiyo.

walibambwa wakiwa katika hotel ya Clasic katika chumba namba 27 wote wamekamtwa,hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo bw magana amejitoa

kabunga,mashahidi,na mtuhumiwa bado wako lupango karagwe,kesi imepigwa kalenda

watumishi wanatuhumiwa kutafuna zaidi ya sh milioni 30 za halmshauti hiyo

Hizi taarifa ni za kweli. Nimeongea sasa hivi na mshikaji wangu aliyeko Karagwe na kuniambia kuwa walikamatwa Ijumaa katika mazingira ya kutatanisha. Lakini Kabunga aliandika maelezo polisi na kuachiwa. Washitakiwa wote bado wako lupango. Huyo mshikakiwa alikuwa afisa elimu kabla ya kufunguliwa mashtaka. Afisa elimu wa sasa hahusiki nakesi hiyo.
 
Kesi iende mahakamani watashinda Tanzania tambarare!

Mkuu tumepewa ruhusa ya kufanya lolote tupendalo Tz. Kama kubaka ruksa, kuiba ndo usisema na tukitaka twanyonga tu! Kesho tunakutana club na kugonga bilauli! Natamani nijilaani! Sina hamu na macho yangu. Kichwa ndo kimebaki kama zezeta vile!:confused::rolleyes:
 
Kwa kweli mimi nimechoka hapo, pamoja na kuwa mimi sijui sheria lakini mambo mengine yananiacha hoi na hawa wataalamu wa sheria, mahakimu, na majaji....nataka nianze kushughulika na wanafunzi wa sekondari wasichana nione kama nitafungwa nikipelekwa kwa pilato.......wale akina Liyumba, Yona, Mramba et al waachiwe huru mapema wasiendelee kumaliza kodi zetu bure!
 
Hii ni kesi ndogo sana!!! Ashinde Zombe aliyetoa roho atashindwa tajiri wa mamotel anayejua kugawa chapaaaaa??? Itafutwa muda si mrefu, subiri.
 
Kwa kweli mimi nimechoka hapo, pamoja na kuwa mimi sijui sheria lakini mambo mengine yananiacha hoi na hawa wataalamu wa sheria, mahakimu, na majaji....nataka nianze kushughulika na wanafunzi wa sekondari wasichana nione kama nitafungwa nikipelekwa kwa pilato.......wale akina Liyumba, Yona, Mramba et al waachiwe huru mapema wasiendelee kumaliza kodi zetu bure!

Mwanawane,

Leo nimefanya ugunduzi kama wa wale wazungu wa miaka 1800! Kwa Tanzania ya sasa hakuna biashara inayolipa kama jinai (crimes)! Kwani unaweza kutengeneza pesa, jina na kila kitu unachohitaji kuwatesa mabwege. Itabidi nianze ku-explore upya interests zangu! Hakuna sababu ya kufa masikini wakati kila kitu kina ulinzi wa hali ya juu (first class protection)! Wajinga ndio tunaoliwa!
 
Hakika sheria inachotaka ni UTHIBITISHO PASI NA SHAKA kuwa mtuhumiwa alitenda na si vinginevyo.

sasa tusubiri pasi na shaka sheria itachukua mkondo wake
 
Ni kweli ila hiyo pasi na shaka inawategemea mashahidi. Sasa kama mashahidi watapotezwa kwa njia yoyote ile hata kama ni mtutu au slow poison tutapata ushindi mahakamani? Kwa nini tusirudi kweye utaratibu wetu wa kutumia wazee kutoa hukumu kama walivyofanya mababu zetu? Au tukaacha kila mtu achukue hamsini zake?
 
Ebo! Wamwachie haraka wasichezee hela zetu kuendesha kesi, hana hatia yes kama Zombe. PCCB waache nchi ujiendeshe yenyewe
 
inaonyesha mwenendo wa kesi nyingi ni wa style hii. mashahidi kuhongwa, mahakimu na majaji nao?
 
Mnaonaje tukipropose Shariah Laws na tukawaita askari wa kusimamia wawe Boko Haram? :D
 
Labda iwe shariah kwa mfumo wetu wenyewe lakini siyo ule ninaousikia! Tunaweza kukubaliana kuwa na mfumo wetu na kwa kutazama huko nyuma tulivyokuwa tunashughulikia mashauri yetu! Huu utaribu wa pasi na shaka umeniacha njia panda.
 
Back
Top Bottom