lord atkin
Senior Member
- Sep 30, 2018
- 197
- 683
Nimeona taarifa zikisambaa kule Twitter kwamba Wakili Msomi Peter Kibatala amesema yupo tayari kumtetea mahakamani meneja wa TRC kanda ya Dar Es Salaam ndugu Jonas Afumwisye Mwangunga alitefukuzwa kazi Kwa kupinga tozo Whatsapp group.
Nikajiuliza ni mahakama gani hiyo? Ina maana Wakili Kibatala hajui kwamba mahakama za kawaida na hata Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) haina mamlaka ya kusikiliza migogoro ya wafanyakazi wa Umma?
Ndugu Jonas Afumwisye Mwangunga option aliyonayo kwa Sasa si kwenda mahakamani bali ni kukata rufaa kwenda Tume ya Utumishi wa Umma na kama hataridhika na maamuzi ya Tume ya Utumishi wa Umma atatakiwa kukata rufaa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na maamuzi ya Rais kuhusiana na migogoro ya wafanyakazi wa Umma ni final (ya mwisho).
Mfanyakazi wa Umma hawezi kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya Rais kumfukuza kazi wala hawezi kupeleka mgogoro wa kikazi mahakamani wala kokote nje ya utaratibu hapo juu.
Kwa maelekezo haya ambayo pia yalielezwa wazi na mahakama ya rufani ya Tanzania kupitia kesi ya rufaa ya madai CIVIL APPEAL NO. 12 OF 2022 TANZANIA POSTS CORPORATION VERSUS DOMINIC A. KALANGI mahakama hiyo ya juu zaidi ya Tanzania ilisema migogoro ya wafanyakazi wa umma inatakiwa kuishia ndani ya Serikali,
Ninamshangaa wakili Kibatala kusema atamtetea mMhakamani ndugu Jonas Afumwisye Mwangunga, ni ama Kibatala anataka kujitwalia umaarufu wa bei rahisi katika hili suala.

Mahakama ya Rufani: Maamuzi ya Rais kuhusu Wafanyakazi wa Umma ni ya mwisho
MAHAKAMA YA RUFANI: CMA HAINA MAMLAKA WAFANYAKAZI WA UMMA Mahakama ya Rufani ya Tanzania imesema Tume ya Usuluhishi ya wafanyakazi (Commission for Mediation and Arbitration-CMA) haina mamlaka ya kusikiliza na kutolea maamuzi kesi zinazohusu migogoro ya wafanyakazi wa umma. Kupitia kesi ya...
www.jamiiforums.com