Aliyekuwa meneja wa TRC apata dhamana baada ya kukaa mahabusu siku 6

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Jonas Afumwisye alikamatwa na kushikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kwa madai ya kupinga Tozo za miamala kwenye Mitandao ya Kijamii.

Wakili Peter Kibatala anayemtetea mtuhumiwa amethibitisha kuachiwa kwake na kueleza kuwa wamewasilisha #Rufaa Tume ya Utumishi wa Umma wakipinga kufutwa kazi na Shirika la Reli (TRC).

Kibatala amesema “Tumekata rufaa ya kupinga kufukuzwa kazi na TRC tangu Agosti 29 na imepokelewa, sasa tunasubiri maelekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma namna Rufaa itakavyoshughulikiwa,”.
 
Duh Stanger than Fiction....

Kweli tunaishi nchi ya Ajabu Sana......., Wakati kuna watu walishaua kabisa kwa kuendesha gari kwa uzembe na hawakufungwa, walamba asali wanakula keki ya taifa na kuifuja..., wengine wanafanya yale Ndugai ambayo alituonya ila wanapeta na kupigiwa makofi....

Na sasa kuwasema imekuwa kosa...., Kweli Andhaa Kanoon
 
Majitu yamo yanasababishia serikali hadi hasara za billions of money ila yako yanapigwa kiyoyozi Na shangingi za kutosha
 
Ni lini mashehe walitetea wananchi?
Ni kweli na ndio maana hakuna mbunge ni shehe ila maaskofu au sijui wachungaji kibao ni wabunge, shehe akisema ataambiwa usichanganye dini na siasa au watambrand gaidi ila askofu akisema anapambwa na kupewa attention, so unayo haki ya kuhoji safi sana
 
Back
Top Bottom