Tetesi: Wakenya wanataka waruhusiwe kufanya kazi Tanzania bila Vibali, rais asikubali

Waruhusiwe tu, nina uhakika wataokuja ni wale wenye capital zao za kutosha kufanya biashara na kutuajiri. Wakija choka mbaya kutafuta kazi watajuta wenyewe kwenye awamu hii ya uhakiki.
 
Naomba ombi hili limfikie raisi wetu Mh. John Pombe Magufuli.

Kesho Jumatatu Raisi wetu ataanza ziara ya siku mbili ya kiserekali nchini Kenya na atatembelea viwanda mbalimbali ikiwemo kiwanda cha Maziwa cha Brokies Diaries kinachomilikiwa na Familia ya Mzee Kenyatta.Hio sio ishu kwetu kabisa.
Kuna habari za kuaminika Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta ana maombi makuu mawili kwa Raisi Magufuli.

Ombi la Kwanza
Raisi Kenyatta atawasilisha ombi la kuungwa mknono na Tanzania ili waweze kupata uenyekiti wa Africa Union Commission ambapo mwanamama na Waziri wa mambonyq nje wa Kenya Bi Aminq Mohamed anapigiwa chapuo achukue nafasi hiyo.Watanzania hatuna shida na ombi hili na tuko pamoja na Raisi wetu akiamua kuunga mkono jambp hili.

Ombi la Pili
Inasemakana Raisi Uhuru Kenyatta ataomba Tanzania ifute sheria zinazowataka raia wa kenya kuwa na vibali vya kufanya kazi hapa nchini yaani work permits.Hapa ndio kuna shida ikumbukwe tumekua na tatizo la wakenya kuja hapa nchini kuchukua fursa ambazo mungu aliwaumbia watanzania sasa kama Raisi Magufuli ataingia kwenye mtego huo basi sina shaka soko la ajira litavamiwa na wakenya ambao kila siku mate ya yanawatoka na ajira zetu.Najua raisi wetu wewe ni mtu wa kufanya maamuzi ya hapo kwa hapo ila kwa hili naomba usiingie kwenye mtego wa Uhuru Kenyatta.
Watanzania wenzangu naomba tupaze sauti na kuhakikishia ujumbe huu unamfikia Raisi wetu haraka iwezekenavyo tusambaze ujumbe huu whats app,twitter,facebook kila kona jamani.

[HASHTAG]#ChochondeMagufuli[/HASHTAG]
6400a90d9136a9fb54299bfb7783f4d2.jpg
raisi yupi ur creze
 
Fatilia mkuu acha kuwa mvivu....

Wa Mexico wanaishije USA?
Walio wengi wanaishi kama wahamiaji haramu mkuu, na Marekani haina mpango wa kuwaruhusu kufanya kazi bila vibali wamexco. Kwahiyo mnaojaribu kutushawishi kuwa Tz iondoe work permit lazima msupport na hoja za msingi. Hakuna taifa lolote linalotaka kuruhusu wageni kujiingilia kiholela kufanya kazi bila kuangalia maslahi ya nchi husika.
 
Aone viwanda kama majirani wana viwanda vya wazungu au vya waafrika mimi sijui cha msingi aone viwanda vinafananaje..

Kwani sisi hatukuwa na viwanda?
May be those time alikuwa Mtoto so hakujua viwanda vinafananaje.

Hainiiingii akilini kama mtu mzima mtanzania hujui viwanda viko vipi kwa sababu tulidhakuwa na viwanda vya kutosha hapa Tz.

Let me tell u, kuna watu tayari wana upeo(vision) so hawa watakupa muongozo wa kuendeleza wengine ndiyo maana Nyerere kipindi kile alikuwa anachanganya watu kila kona ili wale wasiokuwa na uelewa, elimu, maendeleo yawapate from hao waliokuwa na vision.

Sasa huyu Juma anawagawa watu kwa hasira zake na uselfish.
Nyerere angekuwa hivyo tungekuwa hapa Leo?
Kwanza unakosea ukisema rais akajifunze viwanda vinaendeshajwe. Rais sio msimamizi wa viwanda wala msajili wa viwanda. Hizo kazi za kujifunza ni za makamisha wa viwanda na wakaguzi wa viwanda. Na hatuna uhaba wa hao wataalamu. Kama ulivyo sema mwenyewe, na sisi tulikuwa na viwanda, lakini kwa bahati mbaya vyakwetu vikafa, wafanyabiashara wa Kenya wakaviendeleza vyao. Lakini ukumbuke viwanda vingi vya Kenya vina umri usiopungiwa miaka thelathini 30, mashine wanazotumia zinaanza kuisha muda wake. Wakati sisi tunaanza kufufuwa vya kwetu tukiweka machine mpya na utaalamu mpya. Mfano Dangote, Mo dewji, Bakhresa hata kwenye uchimbaji wa madini na gesi tunatumia utaalamu wa kisasa. Sasa sijui tukajifunze nini ambacho wataalamu wetu hawavijui, kwanza Tanzania inaanza kugeuza uwiano wa kuuza bidha nyingi Kenya kuliko tunavyo nunua.
 
Twendeni shule aisee.....

Kabla ya kuuliza jiulize kwanza watanzania wangapi wako nje ya nchi na wanafanya kazi......

Sometime tuache uvivu....

Kila siku kulalamika....

Ajira zenyewe ziko wapi mnazosema mnanyanganywa?

Bila kuchanganyikana hatuwezi kuendelea lazima tukubali ushindani angalia us kila RAIA wa nchi zote duniani yupo pale ndio maana wenzetu waliendelea,wanaendelea na wataendelea..........
Mkuu sijui kama unaijua Marekani vizuri kua walianza na nini.. Ref.. To Isolation policy@protectionism policy wakati ule
Kwani unaweza kufanya kazi USA bila kua na RP na WP? Mbona sisi tukienda Kenya, Rwanda na Uganda lazma uwe na hivyo vitu
Ata bila ya kuomba mbona wapo wakenya na waganda wanafanya kazi bila hivyo vibali.. Tusiende kwa mkumbo
 
Lazima tukubali walimu waKenya wanafanya kazi nzuri sana ,yaani huwezi kuwafananisha na hawa v.ilaza wetu
 
Mkuu nakuambia kama kuna watu wana Roho mbaya East Africa basi ni KENYA. Mwaka juzi niliajiriwa na NGO flan duty station NAIROBI. Ngoma ikaanza niliporipoti pale,

Yaani niliambiwa na country manager kuwa inabidi ashughulikie work permit kwanza, sasa kimbembe, ili upewe permit ni lazima kazi hiyo iwe imetangazwa Kenya na wamekosa mtu mtu huko, ikaonekana mambo hayaeleweki.

Nimekaa miezi mitatu sioni kinachoendelea ikabidi niwasiliane tena na NGO President SWEEDEN, alipowapigia pale wakasema nimekosa work permit, baada ya mwezi uliofuata nikawa sina jinsi nikabeba begi langu kurudi Bongo land.

KENYANS ARE FOOLS KWAKWELI
Ni kweli wana roho mbaya...wachoyo mnooooo ila ya fools mi sijui looo
 
Hivi tutajitenga tenga na kuwa wanyonge wanyonge hadi lini...

Watanzania tuna tatizo la UVIVU na Wakenya wakijaa watatu outcompete kwenye ajira nyingi maana wanachapa kazi...

Mi namshauri raisi aruhusu waje wapige kazi ili tuamke...
 
Swala la permit Raisi Magufuli hatakiwi kukubali, mimi nilipata nafasi ya kufanya kazi Kenya zaidi ya miaka mitano, Kenya wanasema wanatoa kibali cha kufanya kazi ( work permit) kwa wananchi wa jumuia ya afrika mashariki kumbe sio, ukiwa katika kampuni yeyote Kenya utapewa documents zote za ku apply work permit, baade utazipeleka uhamiaji pale nyayo ,kinachofanyika maafisa wa uhamiaji watapokea zile documents zako na kuzitunza au kuzitupa kabisa, utakaa unasubiri work permit hata miaka miwili hautapata permit, hii ilinitokea mimi kwa kujifanya kuwa ni member of east Africa, nilisubmit documents zangu zikaa zaidi ya mwaka mmoja bila kupata permit, ndipo nikaulizia dada mmoja ambae ana deal na visa/permits katika kampuni niliokuwa nafanya kazi akaniambia ndugu ( Kenya wanatumia sana hili neno wanapoongea na wtz) bila pesa hutapata permit hata kama wew umetoka katika jumuia hii ya afrika mashariki, akaniambia permit Kenya kuna watu /staff wa immigration wanao control the whole process na wanakampuni zao nje ( Agents) bila kupitia kwao huwezi pata permit, na hao huamua nani apate permit nani asipate hivyo ikawa imekula kwangu.

Niliendelea kuongea nae huyo mdada akaniambia andaa 90k Kenyan shillings equivalent to mil 1na laki 8 ya tz ,ujaze form then nipatie documents zako nikusaidie kupata permit, nikamuuliza hiyo 90k ya nini akaniambia hii napatiana agent na watu wa immigration uweze kupata then nitakupatia receipt uweze to claim back ur money to the company, ila akaniambia kabisa katika 90k hii, 10k inakwenda kwa government iliyobaki ni mlungula kwa agent na wahusika wakuu ndani. Kweli nilifanya vile na nikakaa ndani ya miezi miwili au mitatu nikapata permit ya miaka miwili. Kwa hiyo nilikuwa nafanya hivyo pindi nikiwa Kenya kwa zaidi ya miaka sita kwa interval ya two yrs two yrs, wengine wtz ambao hawakuwa na 90k hadi leo sijui kama waliweza kupata permit Kenya, hiyo kampuni tulikuwepo wtz lakini ni mimi pekee ndo nilipata permit kwa njia ya kutoa pesa wenzangu waliotegemea free permit kwa watu wa EAC walisota miaka yote bila kupata permit, hivyo uhuru kama anataka kuleta usawa na anapigania sana permit kwa wananchi wake Tanzania basi kwanza aende pale Kenya immigration awaambie maafisa wake mchezo wanaoucheza kwa wananchi wa EAC, aweke dawati/help desk kwa ajiri ya wananchi wa EAC kupata huduma za business visa/work permit bila kupitia kwa agents na bila kulipa 90k,akifanikiwa hili basi ahamasishe viongozi wa EAC kufuta permit katika nchi husika.

Business visa, ukienda Kenya kufanya kazi ndani ya miezi mitatu hadi sita kabla hujapata permit kuna utapewa kibali cha muda cha kufanya kazi ( business visa) ,hii business visa bila kujali wew umetoka EAC unalipa 5K Ksh, na unapewa miezi mitau, ikiisha unapewa tena business visa ya miezi mitatu kwa kulipa tena 5K ksh, ikifika miezi mitatu hupati unaambiwa apply for permit, hapo ndo shida inaanza, hivyo utaona kuwa Kenyan permit ni ngumu sana kupata kuliko nchi yeyote wanachama wa EAC, kama kuna mtanzania yeyote au mganda au Rwandese amepata permit Kenya bila pesa aseme hapa, sio swala la mchezo kupata permit Kenya , kwa hiyo magufuli awaambie kabisa wao wabadilike, na watoe permit bure kwanza ndani ya miaka mitatu kwa wananchi wa EAC then baadae nchi zingine zifuate, au la sivyo tuendelee hivi hivi kwa Wtz na nchi nyingine kulipa 90k na wao waendelee kulipa gharama za permit nchini tz au kwingineko, wahusika wa magufuli mfikishieni mheshimiwa hii taarifa.
Kutatua hili tatizo ndio hapo hitaji la permit liondolewe... na business visa isiwe miezi mitatu... iwe at least miaka 3...
 
Vipi kwa wabongo, ukienda Kenya unafanya kazi bila kibali? Labda ttuanzie hapo.
 
Twendeni shule aisee.....

Kabla ya kuuliza jiulize kwanza watanzania wangapi wako nje ya nchi na wanafanya kazi......

Sometime tuache uvivu....

Kila siku kulalamika....

Ajira zenyewe ziko wapi mnazosema mnanyanganywa?

Bila kuchanganyikana hatuwezi kuendelea lazima tukubali ushindani angalia us kila RAIA wa nchi zote duniani yupo pale ndio maana wenzetu waliendelea,wanaendelea na wataendelea..........
Sasa kabisa. Tuache uvivu tuchanganyike tuendelee
 
Kuhusu Hilo Ombi Lako Namba 2:KABLA HUJAMSHAURI RAIS KULINDA AJIRA ZA WATANZANIA, WASHAURI KWANZA WATZ WAJUE KUWA UANAHARAKATI WA MASUALA YA SIASA SIYO TAALUMA,UJUZI WALA AJIRA SANA SANA WATATUMIKA KAMA RUBBER STAMP YA WANASIASA NA KUTUPWA.NASEMA HILI KWA KUWA SASA NAONA KILA MTU MWANAHARATI WA SIASA,MCHAMBUZI,MKOSOAJI WA MASUALA YA KISIASA NA KIJAMII. JAMBO LA PILI WASHAURI WABONGO WAACHE UVIVU NA WAFANYE KAZI MAANA HAKUNA KAMPUNI ITAKAYOKUKUBALI KAMA WEWE KUANZIA JUMATATU MPAKA IJUMAA UNAOMBA RUHUSA MARA MAMA ANAUMWA,MARA UNA MSIBA WA BABU MZAA BIBI YAKO MARA UNAUMWA.HAPO NDO PENYE TATIZO HAYO MENGINE POROJO.SI AJABU KUMKUTA KIJANA WA KIBONGO MWENYE MIAKA MPAKA 3O NA WALA HANA HATA UJUZI WALA TAALUMA YA KUTENGENEZA BAISKELI-APATE WAPI MUDA WA KUSOMA WAKATI TANGU ASB MPAKA SAA 12 YUPO MAHAKAMANI ANASUBIRI KUFANYA MAANDAMANO KWENYE KESI YA LISSU.NAHISI HATA VIWANDA VIKIJENGWA WATAJAA WAKENYA - XENOPHOBIC HUKO MBELENII.
Kama makampuni yanaona Watanzania ni wavivu na wakenya ndio wachapa kazi kwanini wasihamishie makampuni yao huko Kenya kwa wachapa kazi?
 
Hivi mnataka muungano wa Africa mashariki halafu bado mnataka kuwekeana vikwazo vya kipuuzi?

Wewe kama huna connection hata wamikoani waambiwe kuja Dar kwa kibali na bado utaendelea kulialia tu.

Watanzania mmekalia wizi tu ndio maana watu serious wanawaajili Wakenya, badilikeni kwanza badala ya kulialia.
 
Twendeni shule aisee.....

Kabla ya kuuliza jiulize kwanza watanzania wangapi wako nje ya nchi na wanafanya kazi......

Sometime tuache uvivu....

Kila siku kulalamika....

Ajira zenyewe ziko wapi mnazosema mnanyanganywa?

Bila kuchanganyikana hatuwezi kuendelea lazima tukubali ushindani angalia us kila RAIA wa nchi zote duniani yupo pale ndio maana wenzetu waliendelea,wanaendelea na wataendelea..........
Waafrika wanaopiga kazi USA ni kazi uchwara tu kama za kutunza wazee, kudeki, kufua na ukuli, kazi ambazo hazifanywi na wamarekani wenyewe tofauti nw bongo ambapo unakuta mkenya au mnyarwanda anapewa ajira kwenye kampuni na kuwa kwenyr top management, si ushenzi huo, watu kama hao ni kuwafata na kuwatoa ofisini kwa nguvu, wasubiri ajira ziwe za kutosha Tanzania ndo wapewe kazi za kufagia stend na kuwa makuli huku watanzania wakichezesha kipanya na ma-file ofisini. Hatutaki ujinga.
 
Back
Top Bottom