Wake zetu Shida ni nini?

Wake zetu Shida ni nini?

Sikupenda kufikia hatua hiyo, lakini kila mtu ana kiwango cha uvumilivu.
Nilitafuta njia ya amani kwa muda mrefu, lakini dharau, matusi na kutojali vilivuka mipaka.
Hata hivyo, najua kutumia nguvu siyo suluhisho bora , lakini wakati mwingine mtu akichokozwa kupita kiasi, hutokea.
Sitetei kosa, lakini pia siwezi kuruhusu nidhalilishwe kila siku kama sina thamani.
Soma Uzi huu halafu unambiankama ana sifa kama hizii Mahusiano na narcissist unaweza kufa!!
Naona kama siku hizi hakuna maadili ya ndoa, ni maslahi tu, kama hakuna maslahi ndoa huyumba na kuvunjika
Mkuu vaaa viatu vya muhusika tafadhali
 
Halafu isijeikawa huko anapokimbilia hakosi wa kumkanda na maji ya moto baada ya kipigo. Kuna ile miguno yao hutoa akiwa anakandwa mapajani akijifanya inauma.
 
Sikupenda kufikia hatua hiyo, lakini kila mtu ana kiwango cha uvumilivu.
Nilitafuta njia ya amani kwa muda mrefu, lakini dharau, matusi na kutojali vilivuka mipaka.
Hata hivyo, najua kutumia nguvu siyo suluhisho bora , lakini wakati mwingine mtu akichokozwa kupita kiasi, hutokea.
Sitetei kosa, lakini pia siwezi kuruhusu nidhalilishwe kila siku kama sina thamani.
Au huna hela? Maana ndoa za sikuhizi mwanaume kama huna hela utateseka sana...yaan nje mkeo atasifiwa ni mvumilivu kumbe wewe ndiyo unavumilia jeuri na kejeli ndani
 
utaweza kuvumilia kuishi peke yako au utatafuta mke mwingine? Mind kuwa wanawake hawafanani baadhi ya tabia usije ukapata mwingine mbaya zaidi kuliko huyo. Kama vipi mbembeleze myamalize muendelee kuishi
Ahsante kwa ushauri wako wenye busara.

Najua kuishi peke yangu sio jambo rahisi, lakini pia kuishi na mtu asiyeheshimu ndoa na mchango wako ni mateso makubwa zaidi.

Ndio maana kabla ya kufanya uamuzi wowote, natathmini kwa kina.

Siwezi kuruka kutoka tatizo moja na kuingia jingine kwa pupa, lakini pia siwezi kulazimisha mtu kubaki kwenye ndoa kama hana mapenzi ya kweli wala heshima.
Kwa sasa najipa muda wa kutafakari kwa utulivu.
 
Kama ni mke wako kaa nae chini myamalize muulize shida nini kwa upole sana ila kama ni mpenzi tu na hauna malengo yoyote piga chini endelea kutafta hela.
Wanaopitia matatizo ni watu ambao walijitolea kuwasitiri hawa wanawake.
 
Umesema ana hiyo tabia ya kukudharau, shida iko kwako. Unaachaje tabia inajenga mazoea? Pale anapoanza tabia isiyokubalika ungeanza kumkanya. Umesubiria imeota mizizi akakupanda kichwani.

Ulipompiga angenyooka, sasa hivi ungekuwa unaongea mengine. Usiwe na tabia ya kumpiga yeyote, watu wanatembea na umauti, sababu utakuwa niwewe kumbe ahadi yake imefika. Mapenzi hayashauriwi, ila mlipofikia kwanza kila mtu, atawanyike, hasira zikiisha na mkijiona bado mnapendana mtatafutana. Poleni ndiyo mahabati hayo...
 
Au huna hela? Maana ndoa za sikuhizi mwanaume kama huna hela utateseka sana...yaan nje mkeo atasifiwa ni mvumilivu kumbe wewe ndiyo unavumilia jeuri na kejeli ndani
ukweli kabisa.
Siku hizi mwanaume ukikosa hela unakosa heshima hata ndani ya nyumba yako.
Lakini kwa upande wangu, siyo kwamba sina hela ila hata kama ningekuwa sina, heshima ni kitu cha msingi ambacho hakitakiwi kutegemea pesa.
Mke anajengwa na moyo wa heshima na uvumilivu , si kwa sababu ya unene wa pochi.
Ndoa ni kuvumiliana na kujengana, si kushindana au kudharauliana.
Kwa hiyo kama mtu hawezi kuvumilia wakati wa changamoto, si mtu sahihi kuwa sehemu ya maisha yangu.
 
Mnaoshauri waachane mnakosea sana mapenzi hisia jaman utakuta mtoa mada hii kapenda kaoza na pia mngepata wasaa wa kusikiliza pande zote mbili kisha kutoa wazo sio kusema waachane.
 
Ingekuwa Mwaka 47 na Wazee wetu wanatumia hasira za hivyo, nahisi wote tungelelewa na Single Parent

Ili kusolve hilo jambo lako, ulipaswa ujishushe

Ukiona Mkeo/Mumeo amekasirika Kwa kiwango hicho, hakuna budi mmoja wenu ajishushe ili kuweza kuhimili atmosphere ya wakati huo

Otherwise Ndoa zetu wote zingekuwa zimeshavunjika kitambo.

Huenda Mkeo amegundua usaliti unaomfanyia at her back, hivyo akapandwa na hasira hadi kufikia huko mlikofikia

Lazima Kuna sababu kubwa nyuma ya hasira za mkeo

Sio vibaya kujishusha na kuongea naye Kwa upole ili kutafuta suluhu
 
ukweli kabisa.
Siku hizi mwanaume ukikosa hela unakosa heshima hata ndani ya nyumba yako.
Lakini kwa upande wangu, siyo kwamba sina hela ila hata kama ningekuwa sina, heshima ni kitu cha msingi ambacho hakitakiwi kutegemea pesa.
Mke anajengwa na moyo wa heshima na uvumilivu , si kwa sababu ya unene wa pochi.
Ndoa ni kuvumiliana na kujengana, si kushindana au kudharauliana.
Kwa hiyo kama mtu hawezi kuvumilia wakati wa changamoto, si mtu sahihi kuwa sehemu ya maisha yangu.
Ni kweli usemayo mkuu,lakini kwenye kizazi hiki Cha nyoka,kilichojaa dharau na kiburi....ni nani utampata mtakatifu asilimia zote... Mwenyezi Mungu awapiganie sana...tupo kwenye nyakati ngumu sana
 
Umesema ana hiyo tabia ya kukudharau, shida iko kwako. Unaachaje tabia inajenga mazoea? Pale anapoanza tabia isiyokubalika ungeanza kumkanya. Umesubiria imeota mizizi akakupanda kichwani.

Ulipompiga angenyooka, sasa hivi ungekuwa unaongea mengine. Usiwe na tabia ya kumpiga yeyote, watu wanatembea na umauti, sababu utakuwa niwewe kumbe ahadi yake imefika. Mapenzi hayashauriwi, ila mlipofikia kwanza kila mtu, atawanyike, hasira zikiisha na mkijiona bado mnapendana mtatafutana. Poleni ndiyo mahabati hayo...
Nimeelewa na shukrani kwa ushauri wako. Kweli, tabia mbaya ikiachwa bila kukemewa inajenga mizizi, na ndiyo maana sasa mambo yamefikia hapo.

Siwezi kujitetea kwa kumfanya mtu kuwa mtumwa wa hasira zangu, na napokea makosa yangu.
Lakini pia, siwezi kuendelea kuvumilia dharau.
 
Huku nilipo nako nasikia makelele mme na mke ugomvi, sio tuliokimbia ndoa tunalala kwa amani
 
Nimeelewa na shukrani kwa ushauri wako. Kweli, tabia mbaya ikiachwa bila kukemewa inajenga mizizi, na ndiyo maana sasa mambo yamefikia hapo.

Siwezi kujitetea kwa kumfanya mtu kuwa mtumwa wa hasira zangu, na napokea makosa yangu.
Lakini pia, siwezi kuendelea kuvumilia dharau.
Mwenyezi Mungu akutangulie, mtu anayekubali makosa yake ni mtu mwema sana. Wachache sana hukubali na kuvumilia matusi na dharau. Kama ulivyoweza kuvumilia hayo yote, nakuombea upate wa kuendana naye mtakayeishi maisha ya amani na upendo.
 
Ingekuwa Mwaka 47 na Wazee wetu wanatumia hasira za hivyo, nahisi wote tungelelewa na Single Parent

Ili kusolve hilo jambo lako, ulipaswa ujishushe

Ukiona Mkeo/Mumeo amekasirika Kwa kiwango hicho, hakuna budi mmoja wenu ajishushe ili kuweza kuhimili atmosphere ya wakati huo

Otherwise Ndoa zetu wote zingekuwa zimeshavunjika kitambo.

Huenda Mkeo amegundua usaliti unaomfanyia at her back, hivyo akapandwa na hasira hadi kufikia huko mlikofikia

Lazima Kuna sababu kubwa nyuma ya hasira za mkeo

Sio vibaya kujishusha na kuongea naye Kwa upole ili kutafuta suluhu
Ahsante kwa ushauri wako. Nimejifunza kuwa wakati mwingine ni muhimu kujishusha ili kuepuka migogoro, lakini pia heshima ni jambo la msingi.
 
Ni kweli usemayo mkuu,lakini kwenye kizazi hiki Cha nyoka,kilichojaa dharau na kiburi....ni nani utampata mtakatifu asilimia zote... Mwenyezi Mungu awapiganie sana...tupo kwenye nyakati ngumu sana
Nashukuru Mkuu, ni kweli tunapitia nyakati ngumu, lakini tukijitahidi kwa pamoja na kumtegemea Mungu, tunaweza kupata amani na suluhu. Mungu atupatie njia.
 
Back
Top Bottom