Wake wenza, nyumba moja kitanda kimoja

Wake wenza, nyumba moja kitanda kimoja

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2016
Posts
15,214
Reaction score
21,635
Nilipoenda Tabora kumtembelea mdogo wangu, nilistaajabu kushuhudia ninayoyasimulia leo.

Bwana mdogo kaanza karibuni maisha ya kujitegemea, kapanga chumba kimoja na sebule maeneo ya chemuchemu.

Pale pia kuna jamaa mmoja mpangaji mwenziye kapanga chumba na sebule lakini akiishi na wanawake wawili mitala kwa kutumia chumba kimoja.

Wake zake hao wanaishi kwa upendo mkubwa huku wakiitana dada. Kazi na hadi kula wanakula pamoja!

Ndugu zangu wataalamu wa saikolojia, jambo hili sijawahi kuliona popote Tz.
Maana kama ni ukewenza, ni lazima mwanaume awajengee nyumba zao tofauti, ama kama ni kupanga atawapangia nyumba tifauti.

Ni maarifa gani yanayosaidia mwanamme kuwamudu, kuweza kuishi nao kwa ukitumia chumba kimoja na wanawake wakaelewana kama kulwa na doto, kiasi cha kuwa ni mfano wa kuigwa?
 
Hiyo kawaida tu pia kuna jamaa namfahamu kaoa wake wawili na anakaa nao pamoja, ingawa tofauti kidogo .
Yeye anakaa chumba chake wake zake wanakaa kila mmoja na chumba chake wanapokezana kumfata mume chumbani.kule ktk vyumba vya wake wanataka na watoto.
Pia mwingine yupo namjua kaoa watatu sasa anakomaje wanapokezana mmoja kumfata kazini miss wa kutoka ili asiende kwa hawara wanasema bora aongeze wewe wanne
 
nikiwa nasimamia mradi wa matofali wa mzee wangu nilisikia hili toka kwa mmoja wa wadada (alikuwa anahusika kukandika tanuri) nikashangaa pia, wake wawili chumba kimoja

basi nikawa namdodosa ananambia jamaa anapiga shoo huku mmoja anasubiri zamu yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom