Wakazi wa UKONGA waapa kuandamana hadi bungeni

Kisendi

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
699
178
Kulingana na taarifa ya Habari ya Jana ITV inaonyesha wazi mbunge wa Ukonga kupitia CCM amekata tamaa kabisa hana ushawishi, hana uwezo wa kulobby kwenye Serikali za mitaa, hana mvuto, hana ubunifu wa kutatua hata kero ndogo ndogo, hajawahi kukutana na wananchi wake kwa vikao vidogo vidogo kama wabunge wengine kama January Makamba wanavyofanya.

Kwa hiyo basi wana Ukonga wamelalamika sana kuhusu barabara inayotumiwa na Watu wengi ya kuanzia Mombasa mpaka Moshi Bar ilivyo mbaya kupita kiasi, hata leo hii ukienda kuona huwezi kupeleka gari yako ndogo utakoma na service yake maana ni mashimo makubwa ya Ajabu, Je kuchagua mbunge ambaye hana ushawishi ina maana hamuwezi kupata hata greda au kuwekewa kokoto kwa mwaka.

Hii ina maana basi wana ukonga tubadilike mwaka 2015.

La mwisho Namuomba huyu mbunge aje angalau kila kata mara mbili kwa mwaka kutatua kero za wananchi kwa kujadili na kuona mbinu gani zitumike ili kama anaona halmashauri ya Ilala haina jioya basi atuunge mkono tuandamane wiki nzima mfululizo bila kuacha maana hatuma maji ya dawasco hata tone tunatumia ya kuchimba, hatuna masoko mpaka uje buguruni, hatuna huduma nzuri ya mafundi wa Tanesco, Umeme kukatikatika, Mashimo ya taka n.k

CHADEMA MPO JIMBO HALINA KICHWA, KAZI KWENU. ZITTO INGAWA ILIFIKA MAZIZINI, NJOO UKONGA TENA NA DR SLAA
 
Alalaye usimuamshe mkuu, haya majuha wacha yaendelee hivyo hivyo tahamaki 2015 hayana ya kusema.

Ukweli barabara ni mbaya sana ile yaani kama vile barabara ya kuekelea machimbo madogo ambayo serikali haiyatambui!!!!!!!
 
Alalaye usimuamshe mkuu, haya majuha wacha yaendelee hivyo hivyo tahamaki 2015 hayana ya kusema.

Ukweli barabara ni mbaya sana ile yaani kama vile barabara ya kuekelea machimbo madogo ambayo serikali haiyatambui!!!!!!!
Losambo umenena kweli, Hi barabara ya Kutoka pale reli(Njia ya kwenda Kitunda) ni mbaya kupita kiasi, Madaraja yamebomoka, Diwani sijui yuko wapi na anafanya kazi gani na Mbunge ndiyo amelala kabisaaaaaaaaaaaa. Ifike wakati sasa wananchi tuwaajibishe hawa viongozi wetu ambao wamekaa tu na kutunisha matumbo yao huku sisi tukiumia. wewe mama mbunge wetu shem on you
 
Wakazi wa jimbo la ukonga jijini dar wameapa kuandamana hadi bungeni kushinikiza mbunge wao ajiuzulu kufuatia kushidwa kutekeleza ahadi zake ikiwemo barabara kujaa mashimo_itv habari jana usiku.
 
Maeneo ya Kitunda/Kivule/Machimbo watu wanatembea tu kwa miguu sasa hivi daladala haziendi barabara mbaya mno
 
Mbunge aliyepo hana la maana mpaka sasa ukijumlisha na diwani wa ukonga na Mstahiki Jerry Slaa ni tabu tupu,kuna na mbumbumbu mwingine Diwani wa Kivule basi jimbo la ukonga ni kuwapa pole kwa kuweka viongozi wa maslahi.
Kikwete aliwahaidi kuijenga barabara hiyo ya kuanzia Mombasa hadi kwa Mkolemba ndani ya siku 100 sijui bado hazijafika kwa mahesabu yake?
Muda ndiyo huu wa kumuua nyani bila kumuangalia usoni.
:A S 13:
 
Wakazi wa jimbo la ukonga jijini dar wameapa kuandamana hadi bungeni kushinikiza mbunge wao ajiuzulu kufuatia kushidwa kutekeleza ahadi zake ikiwemo barabara kujaa mashimo_itv habari jana usiku.

watajiju kwani nani kawachagulia si wao ndo waliochagua magamba.Hakuna sababu ya kuandamana wasubiri 2015 ndo wapige kura kwa hasira. miaka 50 bado watanzania tumelala,hata kainchi kama malawi walishabadilka ama kweli ukubwa wa pua.........
 
Nimejua jana kupitia itv kuwa kumbe ukonga kuna mbunge? She is very 'down to earth'. Akasema ni ukonga yote barabara mbovu wala si hapo walipokuwa wanalalama pekee! She is very open and desperate
 
Mtakoma!slaa hamkusikia alivyowaambia ccm ni janga la kitaifa.na nyie mnojifanya wajanja wa bongo mmezidiwa na watu wa ukerewe loh!
 
JImbo la Ukonga ni sawa na jimbo lililo wazi...tayari kutwaliwa na anayelitaka!
 
Mbunge aliyepo hana la maana mpaka sasa ukijumlisha na diwani wa ukonga na Mstahiki Jerry Slaa ni tabu tupu,kuna na mbumbumbu mwingine Diwani wa Kivule basi jimbo la ukonga ni kuwapa pole kwa kuweka viongozi wa maslahi.
Kikwete aliwahaidi kuijenga barabara hiyo ya kuanzia Mombasa hadi kwa Mkolemba ndani ya siku 100 sijui bado hazijafika kwa mahesabu yake?
Muda ndiyo huu wa kumuua nyani bila kumuangalia usoni.
:A S 13:
Jerry Slaa kalewa fedha za wizi ktk H. Jiji, Mbunge ndiyo sifuri kabisa amevimbiwa posho za Bunge. Kwa kweli tumeingizwa choo cha kike maana tumechagua mizoga kutuwakilisha. CCM oyeeee! Ni kula tu mwanangu, tena kwa kwenda mbele mwenye wivu akajinyonge.
 
mbunge hakuchaguliwa ndio maana ni mwizi na hawajali ni mnywa gongo

Kuna taarifa kwamba mbunge amehama jimbo, amehamia mbezi. Anakuja ukonga mara moja moja kwenye shule zake za Tumaini kwa ajili ya kuchukua makusanyo. Shughuli za maendeleo ya wananchi hana muda nazo.

Diwani wa ukonga yeye ndiye haonekani kabisa na barabara ya mombasa moshi bar ndiyo anayopita lakini kwakuona aibu siku hizi anapanda gari yenye vioo tinted ili wananchi wasimtambue. Hovyo kabisa huyu mwanamke (inasemekana ni chakula ya kirumbe ng'enda, ndiye alifanya uchakachuaji akapitishwa kugombea, hata magamba wenzake hawamkubali hata kidogo).

Tuna meya wa manispaa ya ilala jerry slaa toka jimbo la ukonga hana msaada wowote kwa wananchi. Naye amehamia upanga na kuitelekeza kata yake ya g/mboto pamoja na jimbo la ukonga, na yuko busy kuutafuta ubunge 2015!
 
Mi sina imanai kama huyu mbunge yupo hai bado. haiwezekani hata hatujawahi kumwona ana jipitilisha ama hata kumwona bungeni misijawahi kumwona. sijui tulichagua jini !! kwasababu ingekua tulichangua binadamu lazima hata sikumoja tungepishana nae ama kumsikia hata anaongelea kitu. kama kweli huyu mbunge anaexist kulitokeam mabomu gongo lamboto kunamtu alimsikia akitoakauli kama mbunge? ama kumwona anatembelea waathirika. kusema kweli niliwasikia wabunge wengine wanatoa kauli na mkuuwamkoa akizungumza lakini kamwe sijamsikia huyumtu

ndo maana inaniaminisha kua huyu simtu nakama nimtu hayupo duniani.
we fikiri yalitokea
1.Mabomu sikumsikia
2.mafuriko sikumsikia
4.barabara zimeharibika sijamsikia
5.waathirka wa mabomu hawajalipwa sijamsikia
6.Machinjio yana hali mbaya .atarisha afya zawalaji pamoja na yanaingiza mamilioni ya shilingi kilasiku
7.ukonga haina maji masafi kama vile hakuishi watu nalo sijamsikia

hindo nafasi ya chadema kujitanua na kuongeza wanachama .Nashukuru wallikuja juzi lakini haitoshi tuandae wagombea mapema
 
Back
Top Bottom