Wakazi wa Moshi (Pasua & Majengo) tuna shida...

Wakazi wa Moshi (Pasua & Majengo) tuna shida...

NKUU SINDE KWETU

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
830
Reaction score
91
Ukija majengo utadhani kuna machimbo ya madini jinsi kulivyo na vumbi na ndio kuna wananchi wengi, hakuna hata dalili za kuisha matatizo, hakuna hata kituo cha afya.

PASUA ndio utadhani haiko kwenye manispaa ya Moshi, na kibaya zaidi ndiko anakotoka Meya wa manispaa ya Moshi Ndugu Jaffery. Kwa ambao hamjawahi kufika mtaona ni siasa ila natamani mabadiliko yafanyike ili wapiga kura wapate haki yao.
 
Ukija majengo utadhani kuna machimbo ya madini jinsi kulivyo na vumbi na ndio kuna wananchi
wengi, hakuna hata dalili za kuisha matatizo, hakuna hata kituo cha afya.

PASUA ndio utadhani haiko kwenye manispaa ya Moshi, na kibaya zaidi ndiko anakotoka Meya wa
manispaa ya Moshi Ndugu Jaffery. Kwa ambao hamjawahi kufika mtaona ni siasa ila natamani mabadiliko
yafanyike ili wapiga kura wapate haki yao.
Barabara za pasua zimepigwa greda zote tatizo la vumbi unataka barabara zimwagiwe maji? Majengo huo ni uzushi wako!
 
Ukija majengo utadhani kuna machimbo ya madini jinsi kulivyo na vumbi na ndio kuna wananchi
wengi, hakuna hata dalili za kuisha matatizo, hakuna hata kituo cha afya.

PASUA ndio utadhani haiko kwenye manispaa ya Moshi, na kibaya zaidi ndiko anakotoka Meya wa
manispaa ya Moshi Ndugu Jaffery. Kwa ambao hamjawahi kufika mtaona ni siasa ila natamani mabadiliko
yafanyike ili wapiga kura wapate haki yao.

Meya wenu Jaffery ni diwani; wa chama gani?
 
Hilo la kituo cha afya majengo ni uongo, pale 4 ways ukishuka kama unatoka polisi kipo kimoja, kuna kwa Kishamba mitaa hiyo ... kuhusu vumbi ni kwel, ila Mosh ni wap hamna vumbi... nenda mpaka Soweto.. kuhusu pasua kuna changamoto zake lakni zaid na nyie mbadilike bwana...mna vitabia vya uvivu hvi, wiz, ukabaji, kunywa gongo na kujisahau kabisa kufanya shughul za maendeleo.... we nenda mitaa ya njoro hata Huko pasua ukitokea soko la mbuyuni huwez katiza na kagiza kigiza, utadhani hamko Manispaa ya mosh kweli... Badilikeni msiwe kama watu wa Daslam, kulalama tu, c mchana c usiku.
 
Moshi umekaa kama mji wa kishirikina. Watu ni wale wale, maendeleo hakuna, pesa hakuna. Wachagga wakifunga maduka yao hao wanakimbilia migombani na majani ya ngombe
 
Kaka natamani ungekuwa unaishi maeneo hayo na upate hiyo kadhia.
Na hizo kata ziko manispaa ya moshi..

Mbona hauilalamikii ile ya kwenda Nkuu Sinde/Ndoo/Kimbushi/Nkweshoo/Lyamungo/Nkweseko/Muwe nk. kutokea Makoa ambayo haina Lami tangu UHURU???
 
Mimi nimebahatika kuish pasua , soweto , naweza kusema vumbi la soweto na pasua ni sawa kabisa tofauti iko kwa wakaaji wa maeneo hayo
 
Tatizo mnajenga ki-dar es salaam....style za buguruni.....poleni sana muwe mnamwaga maji barabarani.....ni baadae sana hizo chocho za pasua kupigwa lami kwanza mtabomolewa sana!
 
Ukija majengo utadhani kuna machimbo ya madini jinsi kulivyo na vumbi na ndio kuna wananchi wengi, hakuna hata dalili za kuisha matatizo, hakuna hata kituo cha afya.

PASUA ndio utadhani haiko kwenye manispaa ya Moshi, na kibaya zaidi ndiko anakotoka Meya wa manispaa ya Moshi Ndugu Jaffery. Kwa ambao hamjawahi kufika mtaona ni siasa ila natamani mabadiliko yafanyike ili wapiga kura wapate haki yao.

nimepata shida sana ktk huu uzi wako,
mosi PASUA ndio anapotoka meya wa manispaa ya moshi...sasa ulitaka iwe kama soweto.?
pili unadai kwamba wapiga kura wapate hao yao... swali langu ni hili: KABLA YA DIWAN KUWA JAFFARY PASUA KULIKUWA NA LAMI..? ni haki gan unayotaka wewe kwa niaba ya wapiga kura wa kata ya PASUA..?

MAONI YANGU:
Tatizo la vumbi PASUA haliwez kutatuliwa na Diwan peke yake, wewe, mimi pamoja na yule kwa pamoja ndio tunaoweza kuwa mfano wa kufikia PASUA tunayoitaka.
Ahsante
Mwananchi Mwandamiz
 
Kwakua halmashauri ina magreda na gari za kumwaga maji, napendekeza barabara za vumbi zimwagiwe changarawe na ziwe zinarashiwa maji, itasaidia kupunguza vumbi hasa kwa Pasua na Majengo ambapo mtoa mada anapalalamikia zaidi. Hili lipo ndani ya uwezo wa Meya na Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi.
 
Moshi umekaa kama mji wa kishirikina. Watu ni wale wale, maendeleo hakuna, pesa hakuna. Wachagga wakifunga maduka yao hao wanakimbilia migombani na majani ya ngombe

Mkuu,umenichekesha kweli!
 
Mi sipajuwi vizuri hizo sehemu lakini nilichofurahishwa nacho ni jinsi gani wachangiaji wa Uzi huu wanavyosutana wao wenyewe bila kuweka maslahi ya chama Mbele.

Lakini nimeamini kuwa tukiweka itikadi pembeni michango inakuwa so productive n constructive. Lakini Mie ningependa kujua huyo diwani wa Pasua ambae ni Lord Mayor anatoka chama gani? Naanza pata taabu maana swali Hilo halijibiwi, any way Lord Mayor wenu mpeni ushirikiano na mumweleze haya yote kwa pamoja mtapata majibu......
 
Back
Top Bottom