Wakazi wa Mbagala tuna tabu

Wakazi wa Mbagala tuna tabu

Tunashukuru....huku mbagala ni Kama mkoani kwa Sasa ...ukitoka kariakoo saa tano, unafika zakhiem saa kumi..sehemu ya dakika ishirini tunatumia masaa kibao...huyo diwani wetu shoga angu alikuwa swala tano. Lkn ndio hivyo tena kafa kishujaa
Habari za siku nyingi Demba...

Poleni na kero zote, alale pema peponi kamanda wa mbagala.
 
Slum huwa zina shida sana siku zote
 
Habari za asubuhi wanajamvi. Mm nimeona nitoe maoni kuhusu adha ya usafiri wanayoipata wakazi wa Mbagala. Kila mtanzania akitajiwa jina Mbagala anajua ni kuingilia madirishani kwa wasafiri wa Mbagala.

Kwa sasa hali ni mbaya kupindulia ulichukukulia mvua zinazonyesha, mitaro ya maji imebomolewa, mkandarasi anafanya anavyotaka muda wa asubuhi na jioni ambao magari ni mengi ndio wako bzy kufunga barabara.

Jamani kwa nini isitumike mbinu nyingine ambayowni rafiki kwa wasafiri
Kwa nini wananchi wasitafutiwe njia mbadala
Ina maana hakuna anayeona jinsi walemavu, wanafunzi wanavyorundikana vituoni hadi usgku wa manane magari hakuna
Wahusika wanataka nn kitokee ndipo wachukue hatua?

Au wanataka mama kama mama atoke ikulu ndio aje asimamie hili
Hamjui kuna watoto wameshaacha shule kwa sababu ya adha hii
Namna gani wagonjwa na wanaokwenda kujifungua.

Najua la kufanyika lipo tafadhali wahusika akili itumike zaidi kuliko hali ilivyo sasa ili kuwanusuru wananchi wanaoteseka sana.

Poleni sana wasisitizeni viongozi wenu wawasumbue dc,rc kuweza kupush mradi wa mwendo kasi umalizike kwa haraka,kipande cha kuanzia uhasibu hadi BP round about ya kwenda k/koo ni shida sana foleni kama YOTE.
 
Mkuu pole Sana hiyo barabara ya mbagala ni jehanamu ya wakazi wa mbagala....
Haya mateso yametokana na ujenzi pia nakusihi usichoke ndiyo maisha yalivyo na baada ya muda mfupi tutashau machungu.
Karibu Sana kwetu Chamazi mkuu
Asante sana. Chamazi ipi ulipo wewe. Huwa nafika sana maeneo ya kuanzia magengeni Chamazi Pub, Chagga Bite, last card mpaka Mikumi.

Na pia hufata maziwa kwa vendor mmoja pale Magengeni.
 
Tushaishi Sana huko komaeni mpaka mtoe vumbi kwenye vipara tulikuwa tunakimbizana na magari yanapoingia stendi rangi tatu ni kama vietnam...magari ya ubungo,makumbusho,kariakoo,stesheni,ni vita ya dunia,maisha ya dar kwa maskini ni mateso.
 
Asante sana. Chamazi ipi ulipo wewe. Huwa nafika sana maeneo ya kuanzia magengeni Chamazi Pub, Chagga Bite, last card mpaka Mikumi.

Na pia hufata maziwa kwa vendor mmoja pale Magengeni.
Duu umetisha mkuu..
Nipo mitaa ya Chamazi Kwa masista yaani ukishuka Tu hapo magengen kama unatokea upande wa mjini unaingia kulia
 
Back
Top Bottom