Wakazi wa Mbagala tuna tabu

Wakazi wa Mbagala tuna tabu

Ukiwa na SUV kama yangu kunapitika vizuri kabisa. Wenye Saloon nadhani ndio wanapata shida kidogo.
Kama hakuna mvua hata saloon zinapita bila shida ni bonge moja ya shortcut ya ukwel Sana... daily napita hiyo njia asubuh inatusaidia sana
 
Chanika>Mvuti>Msongola>Kitonga

then unafika Kisewe>Mbande>Chamazi>Maji Chai


then Maji Matitu>Charambe>Rangi Tatu

masaa karibia mawili kmmmmmk
 
Subiri waje!

Mbagala kugumu sana kuishi aisee! Kuna wakati miaka hiyo nasoma chuo niliishi Mbagala Charambe kwa bro wangu mjeda!

Kudadeki nilikoma! Maana ilinilazimu wakati wa mitihani na vile vipindi vya asubuhi, kuamka saa 10 alfajiri. Enzi hizo unakuta gari za pekee ni zile Toyota DCM tu!! Na hapo unakuta kuna wakuda wanazunguka na gari kuanzia maeneo ya Zakhem na kule mbe wapi sijui!!

Kitu kikija unakuta kiko full!! Ni mwendo wa kudandia tu na kupigana vikumbo mlangoni! Wengine wanarukia madirishani!!! Huko mnatakiwa mtengenezewe barabara ya njia 8 maana karibia nusu ya "Wanyonge" wote wa magufuli, wanatokea huko.
 
Mimi naomba kama kuna wakazi wenzetu wa mbagala tusimame tuwe kitu kimoja juu ya adha ya usafiri....
tupaze sauti zetu kupitia majukwaa ya jamiiforum mpaka tweeter ili serikali walione Hilo maana kama ni adhabu basi huku mbagala imefika shingoni
Jana majira ya saa 11 jioni nimetoka kunuanua dawa Nakiete pale Mwenge nikapita juu Kijazi one way mpaka 80 kph mpaka Mfugale. Pale nikawazaaaaaa kabla taa hazijaruhusu nipite wapi?.......nikajipa moyo nipite Mbagala. Daah kilichonikuta sitasahau.

Huwa nakunja mfugale, Lumo, Buza, Kwa Mparange, Kilungule mpaka Matitu.

Aisee! Hii kazi iliyonileta huk iishe nihamie nnakokutaka.
 
Juzikati nipo asubuhi nipo pale Kilungule kushukia bonde la Kwampalange, kuna jamaa kigari chake kimezima mlimani. Tuliokuwa tunakuja nyuma tukawa tumepagawa tutashukaje......watu wakaanza kutoka ndani ya magari. Nilishangaa, kumbe kuna watu na mavyeo ya kijeshi makubwa makubwa wanakaa Chamazi.

Wengine ndo wanajuana pale pale. Hee kumbe nawe unapitaga huku. Dah ile njia iishe tu. Bonge la shortcut.
 
Jana majira ya saa 11 jioni nimetoka kunuanua dawa Nakiete pale Mwenge nikapita juu Kijazi one way mpaka 80 kph mpaka Mfugale. Pale nikawazaaaaaa kabla taa hazijaruhusu nipite wapi?.......nikajipa moyo nipite Mbagala. Daah kilichonikuta sitasahau.

Huwa nakunja mfugale, Lumo, Buza, Kwa Mparange, Kilungule mpaka Matitu.

Aisee! Hii kazi iliyonileta huk iishe nihamie nnakokutaka.
Mkuu pole Sana hiyo barabara ya mbagala ni jehanamu ya wakazi wa mbagala....
Haya mateso yametokana na ujenzi pia nakusihi usichoke ndiyo maisha yalivyo na baada ya muda mfupi tutashau machungu.
Karibu Sana kwetu Chamazi mkuu
 
Huu uzi unanikumbusha mwaka 2014 nikisoma UD, kuvuka Ubungo mataa wakati wa ujenzi wa mwendokasi. Kila mkipita ni mwendo wa road blocks halafu wajenzi hata hawana kazi inayoendelea. Kwa kweli mateso Yale siwezi kuyasahau. Halafu cha kushangaza Mfugale ilivyoanza kujengwa hata hakukuwa na foleni Kama tulivyotarajia.
 
Temeke hakuna sehemu inayoitwa mparange
Ukishatoka kiburugwa unaingia kwa mparange ambayo imepakana na buza na nyantira ule mto ndio uliotenganisha hii miji na kuna daraja pale linajengwa ambalo litatokea kiburugwa......so ukiwa buza pale chini unaiona mparange juu ya mto vizuri tu
 
Hivo karibuni tena diwani wa mbagala kuu kafa kishujaa.....poleni sana wakazi wa mbagala.
Tunashukuru....huku mbagala ni Kama mkoani kwa Sasa ...ukitoka kariakoo saa tano, unafika zakhiem saa kumi..sehemu ya dakika ishirini tunatumia masaa kibao...huyo diwani wetu shoga angu alikuwa swala tano. Lkn ndio hivyo tena kafa kishujaa
 
Back
Top Bottom