Wakazi wa Mbagala tuna tabu

Wakazi wa Mbagala tuna tabu

manka1

Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
13
Reaction score
25
Habari za asubuhi wanajamvi. Mm nimeona nitoe maoni kuhusu adha ya usafiri wanayoipata wakazi wa Mbagala. Kila mtanzania akitajiwa jina Mbagala anajua ni kuingilia madirishani kwa wasafiri wa Mbagala.

Kwa sasa hali ni mbaya kupindulia ulichukukulia mvua zinazonyesha, mitaro ya maji imebomolewa, mkandarasi anafanya anavyotaka muda wa asubuhi na jioni ambao magari ni mengi ndio wako bzy kufunga barabara.

Jamani kwa nini isitumike mbinu nyingine ambayowni rafiki kwa wasafiri
Kwanini wananchi wasitafutiwe njia mbadala
Ina maana hakuna anayeona jinsi walemavu, wanafunzi wanavyorundikana vituoni hadi usgku wa manane magari hakuna
Wahusika wanataka nn kitokee ndipo wachukue hatua?

Au wanataka mama kama mama atoke ikulu ndio aje asimamie hili
Hamjui kuna watoto wameshaacha shule kwa sababu ya adha hii
Namna gani wagonjwa na wanaokwenda kujifungua.

Najua la kufanyika lipo tafadhali wahusika akili itumike zaidi kuliko hali ilivyo sasa ili kuwanusuru wananchi wanaoteseka sana.
 
Mbagala imesahaurika sana
..



Tushawazoea ndio maisha yenu huko ,tabu ni kwa ajili yenu..
 
Mbangala abiria huko mabingwa wa kuingilia dirishani

Ova
 
Mkandarasi huyu wa ajabu Sana,anashindwa kutengeneza njia za mchepuko za kutosha
 
Mbagala kugumu sana kuishi aisee! Kuna wakati miaka hiyo nasoma chuo niliishi Mbagala Charambe kwa bro wangu mjeda!

Kudadeki nilikoma! Maana ilinilazimu wakati wa mitihani na vile vipindi vya asubuhi, kuamka saa 10 alfajiri. Enzi hizo unakuta gari za pekee ni zile Toyota DCM tu!! Na hapo unakuta kuna wakuda wanazunguka na gari kuanzia maeneo ya Zakhem na kule mbe wapi sijui!!

Kitu kikija unakuta kiko full!! Ni mwendo wa kudandia tu na kupigana vikumbo mlangoni! Wengine wanarukia madirishani!!! Huko mnatakiwa mtengenezewe barabara ya njia 8 maana karibia nusu ya "Wanyonge" wote wa magufuli, wanatokea huko.
 
Back
Top Bottom