Wakazi wa Dar, waliozoea Kinyaa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakazi wa Dar, waliozoea Kinyaa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 20, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  M. M. Mwanakijiji
  April 15, 2009 (Tanzania Daima)


  WANAENDESHA magari mazuri ya kifahari; wanavaa nguo nzuri za kupendeza na majengo ya ofisi zao yananguruma viyoyozi vya kuwapoza huku madirisha ya majengo hayo yaking’ara kwa vioo vilivyotiwa giza.

  Ukiangalia kwa mbali Jiji la Dar linaanza kuonekana kama jiji jingine mashuhuri duniani. Ukiwaona wanasiasa wake wakiendesha magari yao yanayopepewa vibendera vya taifa au yale ambayo tunayaita ya kifahari wakielekea kwenye kona za “kujirusha” mwishoni mwa juma, unaweza ukaamini kabisa kuwa Dar yetu hii ni tambarare! Wenyewe wanaamini ni tambarare!

  Tatizo la Dar ni wakazi wake

  Kati ya watu wanaonishangaza kila kukicha ni wakazi wa Jiji la Dar. Nikisema wakazi ninamaanisha watu wote ambao wanafanya Jiji la Dar kuwa makazi yao ya msingi. Miongoni mwao ni rais, waziri mkuu, mawaziri, wabunge na watendaji wa vyombo mbalimbali vya serikali kama JWTZ, Polisi, Usalama wa Taifa, Magereza n.k. Pamoja na hao nawajumuisha mabalozi wa nchi mbalimbali, viongozi wa dini zetu (Sheikh Mkuu, Kardinali Pengo n.k ), pia nawajumlisha wasomi wote wa Chuo Kikuu cha Dar, IFM, madaktari wa Muhimbili Aga Khan na wengine wote ambao wanajitaja kuwa waliwahi kupata elimu rasmi yenye uthibitisho wa cheti!

  Hawa wakazi najumuisha kina mama ntilie, wauza magazeti, wafanyakazi wa kawaida maofisini, watumishi wa majumbani, wauza nyama na wauza karanga. Ninachotaka kusema ni kuwa ninaposema “wakazi wa Dar” najumuisha watu wote wanaoishi Dar na simpi udhuru yeyote. Ninachosema ni kuwa wakazi hawa wa Dar (Jumuisha wote hao hapo juu na wale walioshuka kwenye mabasi na ndege leo!) ni watu waliozoea kinyaa na uchafu kiasi kwamba hawana fikra za kuishi bila ya vitu hivyo!

  Kama wewe ni mmoja wa watu wa Dar unayesoma gazeti hili leo basi wewe ni miongoni mwa watu ninaowazungumzia. Leo sizungumzii mafisadi walioiba fedha Benki Kuu, wala sitaki kuzungumzia hawa wanaotaka kuwaibia watu wetu leo kwa kutumia mradi wa DECI.

  Sitaki kuzungumzia mambo ya CCM wala vita ya TLP. Nazungumzia wakati karibu milioni tatu na zaidi wa jiji kubwa zaidi nchini mwetu la Dar. Hawa wamezoea kinyaa na kuvumilia uchafu!

  Ndiyo! Uthibitisho wa hoja yangu leo ni jambo moja tu (naweza kuchagua mengine mengi) nalo ni mafuriko ya kijinga, yanayosababishwa na uzembe na ambayo yamekuwa yakiendelezwa miaka nenda miaka rudi na watu wasiozoea mazingira masafi na wasioabudu mazingira bora! Mafuriko yaliyotokea wiki iliyopita kama yale yaliyotokea 2008, 2007, 2006, 2005, 2004, 2003, 2002, 2001 n.k ni matukio yanayothibitisha jambo moja ambalo nataka kulisema, wakazi wa Dar hawachukizwi na mafuriko haya, wameyazoea, wanajua jinsi ya kukabiliana nayo kila yanapokuja.

  Wao wamebuni njia mbalimbali za kuyakabili, kubwa ikiwa ni kukunja suruali zao hadi magotini, kushika viatu mikononi, na kuendelea na safari.

  Njia nyingine ambayo wasomi wetu wameibuni ni ile ya kuweka matairi mabovu au maboksi ya mbao ili kutengeneza vivuko mahali ambapo maji yamepungua kwa kiasi. Wataalamu wetu wengine wameamua kupendekeza vivuko vya aina ya kisasa katika kukabiliana na mafuriko haya kwa kutumia usafiri wa enzi za kale wa migongo migongo. Njia hii inadaiwa inatoa ajira kwa wakazi wengine 50,000! Wa jiji letu hili.

  Katika uchunguzi wangu wa hapa na pale nimegundua pia baadhi ya wasomi wenye usafiri wa magari ya kifahari wameamua kutumia njia ya kuhakikisha kuwa madirisha na milango ya magari yao yamefungwa na kwa hakika kujaribu kupita pembeni pembeni.

  Wale wenye piki piki wanajua kuwa baada ya muda maji yatapungua hivyo wanapofika mahali penye maji mengi, basi wanaamua kuzisukuma pikipiki zao hadi mahali watakapoziegesha.

  Mafuriko haya ambayo Rais Kikwete, Waziri Mkuu Pinda, Mkuu wa Mkoa Kandoro pamoja na wakuu wa usalama kina Said Mwema, Mwamunyange na Othman wameyazoea yamekuwa ni alama ya umoja na utulivu wa nchi yetu.

  Ni marufiko ambayo Waziri wa Miundombinu aliyepo sasa (Kawambwa) na wale waliomtangulia (mzee wa Vijisenti) hawana mpango wa kuondokana nayo kwani kuondokana nayo ni sawa na kuvunja urafiki wa muda mrefu.

  Mafuriko haya ambayo baada ya muda yatasababisha mlipuko wa kipindupindu (wilaya za Ilala na Temeke zitashindana nani ataongoza kwa muda mrefu zaidi) yamezoeleka mno kiasi kwamba hakuna mpango wa dhati wa kuachana nayo. Wakati watawala wetu wanajivunia kuinuka kwa majengo makubwa na marefu huku kinachodaiwa kuwa jengo refu kabisa nchini kuanza kujengwa ni wazi kuwa kitu pekee ambacho watawala wetu wameshindwa ni kushughulikia maji ya mvua na maji machafu.

  Huku wakiona fahari wanaendelea kubomoa majengo ya kale, wakitoa vibali kwa majengo mapya, lakini wakishindwa kabisa kufikiria na kuanza mradi wa uhakika wa kujenga mitaro ya kisasa ya kusafirisha maji machafu na ya mvua toka kwenye makazi ya watu. Nimesema wameshindwa kwa sababu wameshindwa.

  Ukiangalia barabara nyingi zinazojengwa katika kile wanachokiita maendeleo pembeni yake utaona wametengeneza mitaro ya aina ya “V” yaani ile ambayo haina mifuniko juu.

  Mitaro hii ni wizi mkubwa wa hela za wananchi kwa sababu kwanza mitaro yenyewe haijaunganishwa, pili kwenye jiji ambalo udongo wake ni wa kichanga kila mvua inaponyesha mitaro hii ndiyo inakuwa ya kwanza kufukiwa.

  Matokeo yake baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar ambao wamezoea kinyaa na kuvumilia uchafu wameamua kugeuza mitaro hii kuwa mashimo ya takataka kama alivyolalamika mkazi mmoja kwenye TBC mwishoni mwa juma.

  Majiji yote ya kimataifa duniani ambayo yamejijenga na kujiboresha kitu kikubwa na cha kwanza cha msingi ni kuhakikisha maji machafu na maji ya mvua hayatuwami kwa muda mrefu aidha kwenye makazi ya watu maofisini.

  Hivyo kwa kutumia mifereji au hata kuchimba mto usio wa asili wamefanya hivyo na kusababisha ukusanyaji wa maji yote machafu na ya mvua kuyaelekeza baharini au kwenye maeneo ya kukusanyia maji hayo.

  Miji mikongwe kama London, Paris, na New York yamekuwa yakitumia mifumo mbalimbali ya enzi na enzi na wamekuwa wakiiboresha kwa kadiri ya mahitaji.

  Hata hivyo miji mipya hasa kule Marekani ambapo miji mingi bado ni mipya mfumo wa maji taka na ya mvua inapangwa mapema kabisa katika ujenzi wa miji hiyo na pale inapobidi ujenzi wa nyumba na majengo mbalimbali huzingatia kwanza uwepo wa usafirishaji wa maji machafu. Katika nchi yetu na hususan kwa jiji letu la Dar, wazo hili limebakia vitabuni na kwenye hotuba za bajeti!

  Ripoti mojawapo ya Timu ya Wanasheria wa Mazingira (LEAT) ya mwaka 2001 ilidokeza hivi kuhusu Jiji la Dar kuwa “ni asilimia 5 tu ya wakazi wa Dar ambao wameunganishwa na mfumo wa maji taka”. Na kwa kiasi kikubwa makazi mengi ya watu bado wanatumia vyoo vya shimo ambavyo uchafu wake hatimaye huishia baharini bila kuwekewa dawa (untreated).

  Tatizo kubwa ni kuwa Jiji la Dar halifuati na haliwezi tena kufuata ile “Master Plan” yao ya miaka ile! Jiji letu limekuwa kwa kasi mno na watu wameongeza mno na sasa majengo pia.

  Bila kuwa na uongozi wenye maono ya mbali tutajikuta tunakabana makoo hivi hivi.

  Wao wenyewe (watawala wetu) wanafikiria kuleta barabara za juu kwa juu na vitambulisho vya smart card! Wakazi wa Dar waliozoea uchafu hawaoni kitu kisicho sawa hapo!

  Wao wapo wapo tu; hawaandamani kupinga halmashauri zao na wasomi wao hawapigi kelele kupinga miradi isiyo na kichwa wala miguu!

  Matokeo yake tunataka kuendesha magari ya kisasa kwenye barabara za juu kwa juu tukizungukwa na takataka! Katika akili zao watawala wako tayari kutumia bilioni 200 kwenye vitambulisho na hakuna anayefikiria kujenga mitaro ya kisasa ya ukusanyaji na utupaji wa maji machafu na ya mvua.

  Hawezi kufanya hivyo kwa sababu wameshazoea. Unajua mtu ukikaa na uchafu muda mrefu hata mwisho husikii harufu yake?

  Sasa, ninachosema si kigeni; wao wanajikua na Watanzania wanakijua na wakazi wa Dar wanakijua. Lakini hayuko mtu mwenye kupima gharama ya kiuchumi inayopatikana wakati mvua inasababisha mafuriko.

  Watu wangapi wanachelewa kazini? Wangapi hawaendi kabisa? Miradi mingapi inabidi isimame kwa sababu ya mafuriko? Magari mangapi huharibika baada ya mvua hiyo?

  Tukiwaambia watasema tunawaonea wivu, na ya kuwa watawahi kuuliza ‘kwanini hamrudi basi kama mnajua sana?’ Tukisema wamezoea uchafu watasema ‘mbona anatutukana huyu?’ tukisema unahitajika uongozi bora ambao haulei uchafu watalia ‘huyu ni mpinzani, CCM nambari wani!’

  Wakazi wa Dar kwa kifupi wanastahili uchafu wote wanaoupata na mafuriko yote yanayokuja na yale yatakayokuja. Wanastahili kipindupindu na vingine vinavyowapindua; wanastahili harufu mbaya na mlipuko wa magonjwa ya matumbo na kichocho!

  Wanastahili kwa sababu ni wao wenyewe wasiolalamika, wasiondamana kusimama sasa inatosha na ni wao ndiyo wanaendelea kuwachafua watu kutoka chama kile kile wakiamini kuwa siku moja watakumbukwa!

  Matokeo yake wamebakia kusoma udaku, kula mahindi ya kuchoma, kwenda kujirusha na kucheza ‘ngwasuma’. Nani anajali?

  Kitu pekee wanachokumbuka ni kuwa hii mvua ni ya muda tu na jua litatoka maji yatakauka, majengo yatapendeza tena na magari yatasafishwa na kurembeshwa. Na kila mkazi atasahau mafuriko ya wiki iliyopita na wote watakuwa wanafikiria suala la DECI!

  Rais ataendelea na shughuli zake, Waziri Mkuu na safari zake, Meya na mikutano yake na wananchi wa kawaida na shughuli zao. Mpaka yake mafuriko mengine! Kwa sababu wakazi wa Dar wamezoea kinyaa, nani anawashangaa?
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  I know..
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Umenena mwanakijiji ni juu yetu kutafakari na kuchukua hatua!
   
 4. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Wakazi wa dsm tutegemee majonzi zaidi ikiwa kutatokea dhahama kubwa la mafuriko, kila mmoja anajitahidi kuhakikisha anaweka miundo mbinu ya kuondoa maji machafu kwenye neo lake bila kujali haya maji yanaelekea wapi? We have to consider the situation at totality!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  halafu watu hao hao kesho utawasikia wamejipanga mstari "CCM nambari wani!"!! NIkisema kuna watu wamerogwa wengine wanasema natukana. Nadhani matatizo ya Tanzania tuwabebeshe watu wa Dar ambako tuseme ndio wana taarifa zaidi, elimu zaidi, n.k Kwanini hawajali?
   
 6. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kama maeneo yaliyo karibu kabisa na Bahari (maeneo ya Posta) hukumbwa na mafuriko huo ni uzembe ulio wazi, manake ilitakiwa iwepo mitaro maji yaende baharini. Tokea nasoma pale shule ya msingi muhimbili, kuna eneo kati ya Tambaza sekondari na shule ya Muhimbili ikinyesha mvua basi linapatikana bwala la samaki barabarani. Pale ni karibu kabisa na baharini, sasa walio Manzese, Tandika nk itakuwaje.

  Tukirudi hili la kulalamika sio jiji la Dar tu, ni waTZ wote tunatakiwa kulalamika. Yani hakuna pa kushika kwa mtu wa kipato cha chini. Watoto wanakaa chini shuleni, tena shule nyingine hata Waalimu hawatoshi, wakina Mama wanajifungua katika mazingira magumu mno, hospitalini wagonjwa wanalazwa kitanda kimoja wawili (hii nikuwafanya waambukizane maradhi), wakulima wanalima na kukopwa huku malipo yao inakuwa mbinde, wazee walioahidiwa kutibiwa bure wananyanyaswa vibaya mno wanapofuata hiyo huduma, vijana waliojiajiri kwa kuchimba madini wanaondolewa na makapuni makubwa yanachukua ardhi yao bila hata kutafutiwa kitu cha kufanya, wavuvi hawafanyiwi mpango wowote kusaidiwa zaidi wanadhulumiwa peupe kabisa kupitia mizani, masoko yanahamishwa na kule yanapojengwa mapya walio madarakani ndio wanahodhi nafasi na kuzipangisha nk.

  Hivyo Tanzania imekuwa ni uwanja wa bora liende kila kona. CCM wanatenda walitakalo kwakuwa wanajua ukifika uchaguzi watafanya wafanyayo na watashinda, wananchi wako kimya. Zambia gusa tu unga wa sembe, muda huohuo watu wako mabarabarani.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Mfumwa, unajua nimefikiria sana na hatimaye nimegundua kuwa kuna tatizo la watu wa Dar! Katika nchi nyingi mabadiliko makubwa ya kisiasa hayaanzishwi kijijini yanaanzia kwenye JIji lao kuu. Angalia Kiev, Ukraine, Paris Ufaransa, London, Uingereza; Washington Dc, Marekani, na hata Nairobi, Kenya. Ukija Tanzania, Dar ni ziii!!!
   
 8. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Hapa umegonga penyewe kabisa...Dar ni mji pekee unaoweza kuwa na wapiga kura "waliokuwa informed" wa kutosha kuinyima CCM ushindi katika majimbo yote. Lakini unaopoona hata Ritha Mlaki ni mbunge Dar...nashindwa kuelewa matumaini ya mabadiliko yatatoka wapi Tanzania.
   
 9. P

  Preacher JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani sio kwamba Wa-Dar tunapenda uchafu - ila kuchukua action ya jambo lolote inabidi kuji-mobililize (kujikusanya/kujipanga) mtu mmoja mmoja ni ngumu kwa kweli - na mobilization inahitaji leader/wahamasishaji etc. Tupe ushauri - how to start - otherwise we are ready for maandamano etc. Najua inatakiwa kupata kibali cha kuandamana au tunaishia kupigana risasi/mabomu ya machozi etc. - this is typical third world countries - hawaruhusu maandamano hata kama ni peaceful ones - TULISHASEMA VIONGOZI WETU KWA KWELI HAWAFANYI CHOCHOTE - SIJUI TUKIANDAMANA WATEELEWA KWELI??
   
 10. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You can take an African out of the filth, but you can't take the filth out of the African.
   
 11. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Aliwahi kuzungumza Mch. Anthon Lusekelo kwenye kipindi kimoja cha "Je, Tutafika?" pale Ch. 10. Alisema tatizo la nchi hii ni kutofuata vipaumbele (priorities). Akafananisha na mtu asiye na nguo kabisa, lakini akienda dukani anaanza kununua kofia, halafu litafuatia shati (ikibidi siku nyingine), halafu ndio itakuja suruwali (ikibidi siku nyingine pia). Ndivyo Bongo inavyofanyiwa, ndege ya rais, radar, vitambulisho vya taifa etc. huku mitaro inaziba !!! Ni aibu sana jiji kuu mtu anavushwa kwa mkokoteni kukwepa maji !!

  Nilikuwa Kuala Lumpur juzi tu, ni nchi ya ulimwengu wa tatu kama sisi, lakini sidhani kama wanatakiwa wawe kwenye category yetu!! Kule huwezi kujua mtu anafagia barabara muda gani, lakini hakuna takataka barabarani, wakazi wake ni wasafi mno. Sisi Bongo utakuta njemba imekosa seat kwenye daladala, inakula muhindi humo humo ikiwa imesimama, halafu ikimaliza inakuomba ufungue dirisha ili atupe kigunzi barabarani!! au unakuta dereva wa daladala ananunua miwa na kuanza kula, huku akitupa makapi barabarani bila wasi wasi!!! Huwa naogopa kuwakosoa watu wa hivyo kwa kuwa ninahofu kukosa sapoti !!!
   
 12. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,887
  Trophy Points: 280
  MMJ umewahi kusikia kiongozi yeyote wa kitaifa (maana wanaishi Dar) au wa kimkoa akilivalia njuga suala hilo mpaka kila raia akafahamu kuwa huyu anakerwa kabisa na huu uozo? HAKUNA. Viongozi ndio wanaopandikiza fikra hizo za uchafu kwa watu wake kwavile nao ni wachafu pia.

  Dar huwezi kuilinganisha na jiji la Mwanza kwa nini? Angalau Mwanza watu wanaujua usafi na ni aibu kwa mtu kutupa taka hovyo. Makampuni yanayofanya usafi nayo yanadhibitiwa na hayajapewa tenda kifisadi au kujuana bali uwezo wa kazi.

  DAR ILIYOOZA NI AIBU KWA WATU WAKE,VIONGOZI NA SERIKALI YOTE. Wakazi wa Dar kama hawawezi kuona uchafu kwa macho yao na pua zao hazisikii uvundo wa uchafu huo, sio rahisi kutambua uchafu wa kimaadili wa viongozi wao na kudhibitisha hilo subiri wakati wa uchaguzi uone maamuzi yao.
   
 13. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati Mrema akiwa Makamu Waziri Mkuu (Awamu ya pili) nakumbuka alilivalia njuga hili suala na alipata mafanikio mazuri tu. Hata Keenja (awamu ya tatu) nae alifanikiwa na usafi wa barabarani. Awamu hii ndo sijasikia wala kuona.
   
 14. M

  Magehema JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  MM please assist, tuanzie wapi??? Kwanza; ili jamii ya watu wa DSM kutambua kwamba tatizo lililopo whether mafuriko, pindupindu, ujambazi wa mchana mchana etc linatokana/linachangiwa na uongozi (watendaji) waliopo madarakani, pili; jamii ya DSM itambue kwamba ina maamuzi na uwezo wa kuhoji utendaji wa mamlaka husika na ikibidi kubadilisha uongozi au kuwawajibisha wanaohusika, tatu; jamii ya watu wa DSM iwe na uthubutu wa kukemea, kuhoji, na kuchukua hatua stahili pale inapobidi. Tatizo nilionalo MM ni kwamba kila mtu anashika hamsini zake, hatuna jambo ambalo linatukutanisha pamoja kama wanaDSM. Tufanyaje?
   
 15. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  e bwana ee, MM ngoja wenyewe wakusikie
  -- Anajifanya msafi sana kwa kuwa yupo ughaibuni, kwani yeye katoka wapi.
  --Tuletee ushahidi kwamba jiji ni chafu.
  -- Unataka kuvuruga amani, umoja na mshikamano wetu.
  --Si unajua hata US kuna recession, itakuwa sisi bwana !!
  -- Anaandika magazetini anataka tunyimwe misaada.
  blah blah blah......
   
 16. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Excellent thread!!.

  Kwa kuangalia tu baadhi ya maoni katika thread hii utajua tatizo liko wapi. Kila mtu anataka uongozi uchukue hatua, je uongozi huu ni upi? Hivi kweli kusafisha na kuhakikisha mazingira ya nyumbani kwako, sehemu yako ya biashara au mtaani kwako ni jukumu la viongozi wa mtaa, kata, tarafa, wilaya, mkoa, nchi?

  Hebu tuweni wastaarabu, tujaribu kutake initiative hata katika vitu vidogo tuwezavyo kuvifanya sisi wenyewe. Uchafu huu waathirika wake ni sisi wenyewe na sio viongozi wanaokaa Oysterbay na Masaki.

  Hii attitude ya kivivu ya kutaka kupass the buck whenever an ounce of responsibility is required of us inasikitisha na ndio inayotumaliza katika mambo mbalimbali.

  Usafi ni jukumu letu sisi wananchi na jamii kwa ujumla.
   
 17. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2009
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haya yote yasingekuwepo kama tungekuwa na a very daring leader kama Mrema au Sokoine.
  Lakini haya yote yana mwisho lini haijulikani. Shida ya wakazi wa jiji ni kuwa kila mtu anasubiri nani aanze,sote tumeoza.Kura sidhani kama ndio jibu sahihi,sisi wenyewe ndio jibu la yote.
   
 18. M

  Magehema JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  There is no way you can exclude leaders or responsible authorities in this case. Just a simple example, mimi nimefagia nyumbani kwangu, nimekusanya takataka vizuri, nakwenda kuzitupa wapi? Ni jukumu la mamlaka husika kuandaa/kutenga madampo ya kutupa hizo taka. Ni mara ngapi kumekuwa na malalamiko kwamba hakuna madampo ya kutupa takataka? Kulikuwa na kesi moja kule tabata, dampo kwenye makazi, hapo unamlaumu mwanachi wa kawaida kwa lipi? Huwezi kuwaondoa viongozi katika hizi lawama, hasa suala la mafuriko DSM, its crystal clear kwamba mifumo ya maji ni mibovu. Who's responsibilities is that!!!!
   
 19. Kilinzibar

  Kilinzibar Senior Member

  #19
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 6, 2008
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shukrani mwanaKijiji, ishu nyingine ni hizi kodi tunazo lazimishwa kulipa zinafanya kazi gani? mana si mitaro tu mfumo mzima wa maji safi na taka tangia mkoloni sidhani kama tumesha wahi weka mfumo mpya sisi kama watz!!!
   
 20. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kila idara nchi hii imevunda kama si kuvurunda

  sasa wapi tuanzie??? maana matata ni mengi wakuu.

  Kuna ishu pale KIVUKONI na kivuko kipya

  Kwanza: Mpaka yatokee maafa ndipo wahusika watastuka, ni kwamba yale mabanda ya kusubiria pantoni hayana tofauti na mahabusu za segerea kwani watu wanajazana na outlet ni moja kisha waliobuni hawajaweka escaping routes kama kutatokea dharura, maana ukisema utegemee mfungua geti wakati wa dharura ni sawa na kumpatia mtoto achezee bastola. watu wanajazana kupita kiasi na naamini wengi wameshaambukizwa na wengine wapo mbioni kuambukizwa TB na magonjwa jirani zake.

  Pili: Ile pantoni mpya si lolote ni mapangaboi tu. Nilishuhudia fundi akiingia chumba cha injini kurekebisha mitambo wakati chombo kipo majini njiani. pia pantoni hiyo imekuwa ikisuasua sana katikati ya maji na mara nyingine injini hutoa moshi mzito mnene ambapo sidhani ni dalili njema.

  Tatu: funga kazi ni kwamba LIFEJACKETS zimepigwa kufuli ambapo kama ikitokea dharura majini basi itakuwa watakao kosa kushikilia yale maboya makubwa basi ndo itakuwa kwaheri. Nasikia wansema kuwa wameyafungia kwa kuwa wabongo watayaiba. Hivi nyie vichwa maji mnawazaga nini lakini? mbona hamko progressive? toeni elimu na muwe na usimamizi mzuri hakuna kitakachoharibika. halafu lile pantoni limeanza mchezo wa kudelay zaid ya dk 40 upande wa feri dar ilhali kuna shehena ya abiria upande wa pili ambapo likifika halichukui zaidi ya dk kumi baada ya kushusha abiria utasikia HONI halafu hiloooo lipo katikati ya maji.

  Nne: sielewi kwa mantiki na sera ipi mnawalipisha wananchi wale kuvuka huku mnajua kuwa watu wanaoishi kule ni walalahoi ambao kwa kuwasaidia mnaishia kuwapora ardhi yao? Je hamtajenga daraja kwa kuwa kila siku mnakusanya mahela mengi pale kwenye kivuko??? Haiingii akilini kwamba hata kukusanya mapato anatumika wakala ambapo TRA wangeweza kuratibu makusanyo na tukapata hela nyingi? mbona kivuko kikiharibika huyo wakala ahusiki ktk kutengeneza?????

  Kile kivuko kidogo nawashauri mkakiweke makumbusho ya taifa kwani kimetumika sana tangu uhuru mpaka leo kinadunda. Kivungo kile kinafikia wakatimwingine kinazunguka kama pia ktk maji mpaka inatia huruma na hasira at the same time. Mpaka kiharibu maisha ya watu na mali zao ndipo mtasema kuwa sasa tukiondoe majini?? Hapana IMETOSHA.

  Kule upande wa kigamboni sielewi wahusika wana maana gani kufunga mageti ya njia ya kushoto ya waenda kwa miguu wanaposhuka chomboni?? mlijenga ile njia ya nini?? ya makumbusho au ya waheshimiwa kupita? watu wanasongamana na kugombania njia moja na magari, nadhani maafa yakitokea ndipo mtaanza kuchukua tahadhari??? ACHENI uvivu wa kufikiri. Bila ya kuwastaarabisha watu hawatastaarabika milele.

  Halafu kwa nini msitafute wakala wa usafi ili angalau kupiga deodoranti pale feri maana soko la samaki linanuka vibaya mno. au mpaka mpate takwimu za wanaoathirika na hali ile ndipo mchukue hatua???

  Eee Mungu kwa nini usiwapige dafrao hawa viongozi na watawala wetu vipofu? waonao GIZANI lakini wanakuwa vipofu mchana.
   
Loading...