Wakatisha tamaa (Downers)

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,694
58,763
Downers.
That's what I call the people that are constantly trying to put others down.

Watu kama hawa wako kila mahali,majumbani, mashuleni, makazini na hata mitaani. Wanawashushia wenzao ari ya kusoma,kutafuta maendeleo, kufanya kazi, kukuza na kuendeleza vipaji vyao kwa sababu ya madhaifu yao wenyewe au woga wa kuwaona wengine wakifika mbali.

Muda sio mrefu nilitokea kuangalia kipindi cha mashindano ya kuimba, kabla ya kuimba dada mmoja (umrimiaka 37 kama sikosei) akawa anaelezea kwanini imemchukua muda mrefu kujaribu bahati yake. Alikua na mpenzi ambae kila akiimba alikua anamwambia hana sauti nzuri na maswala ya kuimba hayawezi kumfikisha popote kwasababu hana kipaji. Dada wa watu alisikia hayo maoni so many times mpaka na mwenyewe akaanza kuamini kwamba ni kweli hana kipaji japo wakati anakua aliamini anacho. Akapoteza kujiamini mpaka alipokuja kuachana na yule bwana na ndio akaona aende kwenye hayo mashindano.

Honestly yule dada alipoimba tuchozi tulinitoka pamoja na watu wengine wengi tu waliokuwepo kwenye hicho kipindi.Her voice was simply AMAIZING.

Wapo watu wengi sana wanaonyang'anywa kujiamini kwa namna hii..wakubwa kwa wadogo.Wakati mwingine hata mzazi anaweza akachukua nafasi hiyo ya kumshusha mwanae...yaweza isiwe kwa makusudi bali kwa yeye kuamini kwamba mwanae hawezi hicho anachojaribu ila inatokea na inaathiri.

So next time ukisikia mtu anakwambia''huwezi hichi...huwezi kile'' usichukulie hayo maneno kama sheria. Usikubali kuaminishwa huwezi wakati unaweza...hutofika mbali wakati matumaini yapo...WASHANGAZE watu waliodhani hutofika,hutoweza kwa kupigania na kufikia malengo yako.

Jifunze kutofautisha criticism nadiscouragement.
…..Criticism imejikita kwenye kujenga na kuboresha zaidi. Kukupa moyo nakukuimarisha...UKIPEWA CHUKUA NA TUMIA VIZURI KWA FAIDA YAKO.

…..Discouragement imejikita kwenye kubomoa msingi wa kujiamini kwenye mambo au jambo fulani.Kukuonyesha kwamba huwezi na hata ufanye nini hutoweza HII USIRUHUSU IKUTAWALE.

Kama wewe ni mzazi...jitahidi kumkosoa mwanao pale inapobidi ili kumjenga(critisism is good ) ila usimkatishe tamaa. Kwa wengine wote....usiruhusu madhaifu yako...kutokujiamini kwako...chuki...wivu au hata mtazamo wako kuhusiana na maisha uathiri watu wengine. Kosoa kwa nia ya kujenga ...kama huwezi acha!!
 
Lizzy, Mzima wewe? Sijui kama hapo kwenye blue unamzungumzia huyu dada hapa chini. Alijijua ana kipaji cha kuimba miaka mingi, lakini kila alipotaka kupiga hatua ili ajaribu bahati yake kama muimbaji boyfriend wake alikuwa anamkatisha tamaa kwamba umri umeenda sana na pia sauti yake si nzuri. Wiki chache zilizopita nilimuona akiimba kwenye kipindi kinachoitwa X Factor na uimbaji wake ulinigusa sana na nadhani akitulia basi muda mfupi ujao anaweza kujipatia umaarufu mkubwa sana duniani kwa uimbaji wake na pia kujiingizia pesa nzuri sana.

Last edited by a moderator:

Yeahhh huyu ndie BAK....
Asante kwa kunikumbusha jina lake..amejaaliwa kwakweli.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
She is amazing.

She sure is.....

Mie hadi muda huu sijakutana na hao Downers, nimekutana na Lifters tu.

Au kwa kuwa siruhusu Downer yoyote kunikaribia?!
Inawezekana circle yako ni ''clean'' au hata kama wapo wanajua wewe sio mtu wa kutikisika kirahisi kwahiyo hawajisumbui.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Inawezekana circle yako ni ''clean'' au hata kama wapo wanajua wewe sio mtu wa kutikisika kirahisi kwahiyo hawajisumbui.

Nadhani kama kuna tabia mtu anazoweza kuwa nazo ili hao downers wamuepuke, ni bora tukakumbushana hizo kuliko kumtegemea downer aache tabia yake
 
Hii kitu inafanywa hata na wazazi au walezi bila kujua; including house girls. Mi nshapiga mkwara home hamna mtu yeyote kumwambia mwanangu 'mjinga' au 'hujuhi' (especially katika umri mdogo wa kujifunza kuongea na vitu vingine). Maneno kama haya huwa yanakatisha watoto tamaa ya kujifunza kuogopa kuchekwa.

Ukianza kumjengea mtoto confidence home ya huko mtaani wala hayata mtisha kwani he/she will need no body to tell him/her whether she can/can't.

Wewe chunguza hata enzi za utoto mashuleni, kuna watoto ni leaders always wengine ni followers always.
Utasikia kama ni kuchagua monitor basi ni fulani na wengine hakuna anayeweza wafikiria kwani tayari wanaonekana hawawezi.

Ukijikubali basi utakubalika.
 
Nadhani kama kuna tabia mtu anazoweza kuwa nazo ili hao downers wamuepuke, ni bora tukakumbushana hizo kuliko kumtegemea downer aache tabia yake
Well baadhi ni
....kutokua mtu wa kupeperushwa kamabendera na maoni ya watu wengine.
....Kujiamini.
....Kuwaelewa watu wa aina hii na kuwakwepa..
it's all on the first post.
Hii kitu inafanywa hata na wazazi au walezi bila kujua; including house girls. Mi nshapiga mkwara home hamna mtu yeyote kumwambia mwanangu 'mjinga' au 'hujuhi' (especially katika umri mdogo wa kujifunza kuongea na vitu vingine). Maneno kama haya huwa yanakatisha watoto tamaa ya kujifunza kuogopa kuchekwa.
Kudos for that....
Inatokea sana kwenye jamii....
 
Kinyume na hao kuna wazazi ambao wanalazimisha watoto wao wawe "leaders" japo watoto wenyewe hawataki, hivyo kuwaongezea stress zisizolazima
 
Kinyume na hao kuna wazazi ambao wanalazimisha watoto wao wawe "leaders" japo watoto wenyewe hawataki, hivyo kuwaongezea stress zisizolazima

Unamaanisha kuwaelekeza kwenye direction ambayo iko nje ya interest ya mtoto??
 
Unamaanisha kuwaelekeza kwenye direction ambayo iko nje ya interest ya mtoto??

Sometimes inakuwa kwenye interest sometimes inakuwa kumlazimisha wakati uwezo hana.

Mtu atataka mwanawe lazima awe daktari au lawyer while in reality mtoto Hana interest hiyo

Pia unawezakukuta mzazi anataka mwanawe lazima awe katika top 5 darasani wakati uwezo hana.
 
Yeahhh kama mtoto hana uwezo wa kufika mzazi anapotaka na akalazimishwa anaweza akapoteza hata ule mdogo au alio nao. Na badala ya kuelekea kule ambapo anaweza akafanikiwa anaelekezwa kusiko na matumaini matokeo yake anakosa vyote.

Ni vizuri wazazi wakajitahidi kuwasoma na kuwaelewa watoto wao kwakweli.
 
Heck..those so called 'downers' I call them haters. The best way to deal with them is to make them your motivators.

I've done it throughout and it has worked. They've always brought the best out of me.

I love it when people doubt me. I like it when people talk junk about my abilities.

I love haters because they inspire me to maximize my potential. I am a self-motivated guy but I love to have haters around.

Thus I say, make your haters your motivators.
 
lizzy sijui umewaza nini!

Hawa watu wapo sana, utasikia huwezi hiki huwezi kile.

Watu wa namna hii mie naita negative attitude(sijui kama sahihi sana) ni kutoyapa uzito mkubwa maneno yao, la sivyo hutoendelea/fanikiwa kamwe.
 
I hope people will read and make use of this maana most of them don't know they can take the negativity and use it to their advantage.
Thanks NN!
 
lizzy sijui umewaza nini!

Hawa watu wapo sana, utasikia huwezi hiki huwezi kile.

Watu wa namna hii mie naita negative attitude(sijui kama sahihi sana) ni kutoyapa uzito mkubwa maneno yao, la sivyo hutoendelea/fanikiwa kamwe.

BT mawazo tu ya hapa na pale..
Hua wanajua kweli kushawishi wale wepesi wa kuamini na kuchukua maoni ya wengine kama yalivyo!!!
 
good thread lizzy

had downers but defied all... So if i am a downer, i pray for people to defy me

mara nyingi huwa hatujijui
 
good thread lizzy

had downers but defied all... So if i am a downer, i pray for people to defy me

mara nyingi huwa hatujijui

That's the way to go MTM.
Kweli kuna watu hawajitambui/hawafanyi kwa makusudi maana ndivyo walivyo tu....wanaona makosa kwenye kila kitu hata pale ambapo hayapo!!
 
Lizzy,
Hebu labda unifafanulie, hawa watu huwa wanakukatisha tamaa kwenye jambo moja tu au mambo mengi?
Nikiangalia mfano wa huyo dada ulioutoa, huyo mpenzi wake yaelekea labda alikuwa hataki aingie kwenye hiyo career ya uimbaji. Hizi zipo sana! Assume kijana una gf wako ambaye ni mzuri sana na ana kila quality ya kuwa mlimbende wa sehemu flani, unajua madhara ya Gf wako akienda kwenye hayo mashindano. Utategemea usimdiscourage?
Wakatisha tamaa ambao naona niwakuavoid ni wale ambao kila jambo unalolifanya wanaona hujafanya vizuri.
 
Similar Discussions

14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom